Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kariakoo Derby isiharibiwe jamani

DABI Pict

Muktasari:

  • Kwa sisi wazoefu tunajua kwamba hii mechi huwa inakuwa na mambo mengi hasa ya nje ya uwanja ambayo mengine yanaiongezea mvuto na kuna ambayo yanaipunguzia.

NI kesho tu hapo kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam kunapigwa Kariakoo Derby inayokutanisha miamba ya soka nchini Simba na Yanga.

Kwa sisi wazoefu tunajua kwamba hii mechi huwa inakuwa na mambo mengi hasa ya nje ya uwanja ambayo mengine yanaiongezea mvuto na kuna ambayo yanaipunguzia.

Hata hivyo tunawaomba wote ambao wanashiriki kwa mchezo huo wa Kariakoo Derby kuhakikisha hawaiharibu kwa nna yoyote ile na waache mbungi lipigwe vizuri tu kwa dakika zote 90.

Watu wa kwanza ambao tunawakumbuaha ni marefa ambao watapangwa kuchezesha mechi hiyo. Wao wana mchango mkubwa katika kufanya mechi iishe au isiishe salama.

Wacheze kwa kufuata sheria na kanuni za mchezo. Wahakikishe haki inatendeka na wanaostahili wapate ushindi au droo badala ya kulazimisha mambo.

Safari hii hawana cha kujitetea kwa vile kuna teknolojia ya video ambayo inawapa nafasi ya kurejea tukio na kulitolea uamuzi tofauti na zamani ambapo hicho kitu hakikuwepo.

Na pia hizo timu nazo zinatakiwa ziende kucheza mpira na sio kuleta mambo yao ya ajabu ajabu. Zifuate kanuni na maelekezo ambayo wasimamizi wa mchezo watawapa kama taratibu zilivyo.

Mambo ya kuvunja kanuni kwa makusudi kisa tu zinajiona ni kubwa na zinaweza kulipa faini au hazitopewa adhabu nzito sio wala nini. Ukubwa ni kuonyesha mfano mzuri sio kufanya mambo ya ovyo.

Sisi tunataka dabi ya viwango bhana ambayo ikiisha tutaanza kujadili kilichotokea uwanjani kwa dakika 90 badala ya vituko visivyo na tija.