Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Joto la ubingwa WPL, Simba, Yanga zavutana

WPL Pict

Muktasari:

  • Hadi sasa Simba inaongoza kwa pointi 31 baada ya mechi 11 ikiwa haijapoteza mechi, huku Yanga ikiwa na pointi 30 ikitofautiana pointi moja na mabingwa watetezi JKT wakiwa na pointi 23.

APRILI 3 Ligi Kuu ya Wanawake Bara itarejea ikiwa ni mzunguko wa pili kufuatia mapumziko ya mwezi wa kalenda ya Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) kwenye mashindano ya WAFCON na Kombe la Dunia la Wanawake chini ya miaka 20.

Sasa ligi inarejea ikiwa na ushindani mkali kwani ndio mzunguko wa mwisho wa kufahamu nani  anachukua ubingwa, wanaomaliza nafasi za juu na zile za kushuka daraja.

Hadi sasa Simba inaongoza kwa pointi 31 baada ya mechi 11 ikiwa haijapoteza mechi, huku Yanga ikiwa na pointi 30 ikitofautiana pointi moja na mabingwa watetezi JKT wakiwa na pointi 23.

Raundi hiyo kila mechi sasa ni kama fainali, na Mwanaspoti linachambua kulingana na msimamo na pointi walizokusanya vigogo hao watatu yaani Simba, Yanga na JKT ni mechi ngapi wanahitaji kushinda ili kujihakikishia ubingwa mapema?

WP 01

SIMBA QUEENS

Ikumbukwe mabingwa hao mara nne wa Ligi Kuu ya Wanawake msimu huu hadi mzunguko wa kwanza unatamatika hawajapoteza mechi wakiweka rekodi ya kuwa timu pekee ambayo haijaonja kichapo.

Hilo ni faida kwao kwani kutopoteza mechi hata moja ina maana kuwa wako kwenye nafasi nzuri zaidi ya kuchukua taji hilo kama watakuwa na mwendelezo mzuri wa kushinda mechi zilizosalia.


HESABU ZA UBINGWA

Simba wana pointi 31 na bado wana mechi 11 zenye jumla ya pointi 33 watakazokusanya (iwapo watashinda zote). Kama wataendelea kushinda mechi zao nyingi wana uwezekano mkubwa wa kutwaa ubingwa.

Hesabu ziko hivi. Kwenye mechi hizo 11 kama wakishinda nane watakuwa wamefikisha jumla ya alama 55 ambazo ni pointi za ubingwa.

Hii mara nyingi huwa ni kiwango cha juu ambacho ni kigumu kufikiwa na timu nyingine

Lakini, lililo muhimu zaidi kama watashinda mechi sita mfululizo za mwanzo (dhidi ya Bilo, Bunda, Fountain Gate, Ceasiaa, Yanga, Ruangwa), watafikisha pointi 49. Na hapo wataisikilizia Yanga na JKT wakipoteza mechi mbili katika kipindi hicho, basi Simba wanaweza kutangazwa mabingwa mapema baada ya wapinzani wao hao wanaotofautiana pointi moja kuangusha sita na watakuwa na tofauti ya pointi saba.

WP 02

MECHI MUHIMU SIMBA

Sasa Mnyama kwenye mzunguko huo ana mechi ngumu zaidi mbili kama atashinda dhidi ya Yanga April 24 inaweza kumpa nafasi nzuri zaidi kutokana na ushindani wa timu hizo mbili.

Nyingine ni dhidi ya JKT Queens (22 Mei). Mechi ya mzunguko wa kwanza walipokutana waligawana pointi moja baada ya sare ya 1-1. Wapinzani wao hao licha ya kwamba wako nafasi ya tatu lakini ndio mpinzani mgumu zaidi kwa mnyama.

Hivyo Simba wakipiga hesabu zao vizuri kwenye mechi saba hadi nane zinatosha kuwapa ubingwa na wanaweza kutwaa taji hilo kabla hata ya mwezi Juni.


WP 03

YANGA PRINCESS

Tangu waanze kushiriki ligi hiyo 2018 hawajawahi kuchukua ubingwa yaani kiufupi timu hiyo haijawahi kushiriki mashindano ya Cecafa kufuzu Ligi ya Mabingwa Afrika.

Mafanikio makubwa kwao ni kuchukua Kombe la Samia Women Super Cup kama sehemu ya kusheherekea Siku ya Wanawake Duniani ambapo huadhimishwa kila Machi 8.

Nje na hapo imekuwa ikimaliza nafasi ya tatu karibu kila msimu lakini tangu uliopita timu hiyo imeonekana kubadilika kiuchezaji, ikileta ushindani mkubwa kwa Simba na JKT ambazo awali walikuwa wanaonekana ngumu kuwafunga.

Tangu msimu jana na huu timu hiyo imefanya mabadiliko makubwa ya kiuchezaji na ongezeko la wachezaji wenye ubora imewafanya timu hiyo kumaliza mzunguko wa kwanza ikiwa nafasi ya pili tena kwa tofauti ya pointi moja na Simba inayoongoza.

Kwa upande wa Yanga kuwa nyuma kwa pointi moja na anayeongoza ligi ni presha kubwa zaidi kwani washapoteza mechi moja na hawana nafasi ya kufanya makosa.

Mahesabu ya ubingwa

Yanga ina pointi 30 na hesabu ziko hivi: Wakishinda mechi tisa kati ya 11 watafikisha pointi 57 hii itawapa ubingwa hata kama Simba wataangusha pointi.

Lakini wakipoteza dhidi ya Simba (24 Aprili) na JKT Mei 31, hali inakuwa ngumu zaidi kwao. Ili Yanga wachukue ubingwa lazima washinde mechi nyingi angalau nane hadi tisa na wafanye vizuri zaidi dhidi ya Simba na JKT kisha wasubiri timu hizo zipoteze au kutoa sare mechi mbili hadi tatu itafikisha pointi 54.

Hizi zinaweza kuamua kabisa hatma ya ubingwa wao na zinaonekana kuwa ngumu zaidi kwa wananchi ni Fountain Gate, Tausi FC, Alliance Girls, Simba na JKT.

WP 05

JKT QUEENS

Msimu huu haijaanza vizuri kwani rekodi zinaonyesha ndani ya misimu mitano mfululizo nyuma timu hiyo ilimaliza mzunguko wa kwanza ikiwa kileleni.

Hadi sasa kwenye mechi 11 JKT imeshinda saba, sare mbili na kupoteza moja dhidi ya Yanga Princess ambayo miaka ya nyuma ilionekana kuwa vibonde kwao.

Ina jumla ya pointi 26 na wako kwenye mbio za kuwania ubingwa kwani wanatofautiana pointi tano hadi nne na wanaongoza juu kwenye msimamo wa ligi.

Wakishinda mechi zote zilizosalia watafikisha pointi 59 ambazo kimahesabu wana nafasi ya kuchukua ubingwa lakini wakisubiri Yanga na Simba wafanye vibaya.


WASIKIE WENYEWE

Kocha wa JKT, Kessy Abdallah anasema: “Msimu huu kuna ushindani mkubwa sana hivyo kama hujajiandaa ni ngumu kupata matokeo kama JKT mzunguko wa pili tunajipanga vilivyo kuhakikisha mambo yanakuwa sawa.”

Kwa upande wa Simba, kocha msaidizi, Mussa Hassan ‘Mgosi’ anasema: “Tunafahamu ugumu wa ligi ndio maana tumeongeza baadhi ya wachezaji dirisha dogo ili kuhakikisha yale mapungufu yaliyotokea mzunguko wa kwanza tunayatatua.”