Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Josiah ameanza kuonja matunda ya juhudi

JOSIAH Pict

Muktasari:

  • Josiah ndiye amepewa jukumu la kuinoa timu hiyo baada ya uongozi wake kuamua kutomuongeza mkataba Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ aliyemaliza nayo msimu uliopita.

KATİKA msimu ujao, Mashujaa FC itakuwa na mkuu mpya wa benchi lake la ufundi ambaye ni kocha wa mpira Amani Josiah.

Josiah ndiye amepewa jukumu la kuinoa timu hiyo baada ya uongozi wake kuamua kutomuongeza mkataba Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ aliyemaliza nayo msimu uliopita.

Kwanza kijiwe kinampongeza sana Amani Josiah kwa kupata shavu pale kwa Maafande wa Mashujaa FC maana kinafahamu kwamba mabosi wa timu hiyo ya Kigoma, walikoshwa na kazi aliyoifanya pale Dodoma Jiji.

Amani Josiah aliifanya Dodoma Jiji kuwa miongoni mwa timu shindani katika Ligi Kuu Tanzania Bara na kuwezesha imalize katika nafasi ya tisa kwenye msimamo wa ligi msimu uliomalizika.

Hadi anaamua kujiunga na Mashujaa FC, maana yake amepata maslahi makubwa zaidi ya yale ambayo alikuwa akiyapata kwa walima zabibu wa Dodoma Jiji vinginevyo angebaki.

Na kitendo cha Mashujaa kuamua kuachana na makocha wengi ambao hawana timu za kufundisha licha ya urahisi wa kupatikana kwao na kuamua kumfuata Amani Josiah ambaye alikuwa na timu, kinamaanisha kwamba alichokifanya kimeonekana.

Hapa anatoa fundisho kwamba kazi yoyote katika soka haichezwi chumbani bali uwanjani ambako inaonwa na wengi hata kama isipopigiwa promo na wahusika au watu walio karibu na timu.

Kocha akiinoa timu na ikacheza soka la kueleweka, watu wa mpira wataona na watasifu kile anachokifanya na mambo yakiwa tofauti, watu wataona na watakosoa.

Amani Josiah hakuamua kulalamika kwamba makocha wa kigeni wanapendelewa na wanapewa fursa kubwa hapa nchini. Aliamua kuiacha kazi yake ndani ya Dodoma Jiji izungumze.