Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Jinsi timu EPL zinavyowatumia mabeki wa pembeni

PATAMU Pict
PATAMU Pict

Muktasari:

  • Kupanda pembeni, kuingia ndani, kucheza kama kiungo au kubaki katika majukumu ya kawaida ya ulinzi. Nafasi ya beki wa pembeni imepitia mabadiliko makubwa katika soka la kisasa.

COVENTRY, ENGLAND: MAJUKUMU ya mabeki wa pembeni (full-backs), yamebadilika kwa kiasi kikubwa katika soka la kisasa, huku timu mbalimbali zikibuni mbinu tofauti za kuwatumia wachezaji hao katika maeneo ya pembeni. Hivi ndivyo namna timu zote 20 za Ligi Kuu England zinavyowatumia mabeki wao wa pembeni katika msimu huu wa 2026/27.

Kupanda pembeni, kuingia ndani, kucheza kama kiungo au kubaki katika majukumu ya kawaida ya ulinzi. Nafasi ya beki wa pembeni imepitia mabadiliko makubwa katika soka la kisasa.

Awali, ilikuwa nafasi iliyolenga zaidi majukumu ya ulinzi, huku mchezaji akisaidia mashambulizi kwa kiasi fulani. Hata hivyo, sasa nafasi hiyo imepanuka na kuwa na majukumu mengi zaidi kuliko ilivyokuwa ikitarajiwa.

Muangalie beki wa kulia wa Arsenal, Ben White, ambaye kwa kushirikiana na Riccardo Calafiori, anayekipiga upande wa kushoto, wamekuwa miongoni mwa wachezaji muhimu katika mwanzo mzuri wa Arsenal msimu huu.

Kibongobongo muangalie Nathaniel Chilambo wa Simba anavyocheza? Unaweza kuamini kwamba huyo ni beki au kiungo? Kocha Steve Barker katika mkeka wake anamtambulisha kama beki wa kulia, lakini angalia anachokitafa pale kati?

Akizungumza na Sky Sports msimu wa 2023/24, White wa Arsenal alisema: “Unapocheza nafasi ya beki wa pembeni kwa namna ambayo kocha (Mikel Arteta) anaitaka, nadhani ni tofauti kabisa na namna makocha wengine wanavyotaka nafasi hiyo ichezwe.

“Ili uweze kucheza beki wa pembeni chini yake, unatakiwa kuwa kiungo wa kati, beki wa kati, winga na kiungo mshambuliaji namba 10.”

Ingawa kauli hiyo ilitolewa miaka kadhaa iliyopita, kiwango cha majukumu ambayo mabeki wa pembeni wa Arsenal wanayatekeleza hakijabadilika. Kwa pamoja, White na Calafiori tayari wamechangia mabao sita ya Arsenal katika Ligi Kuu England 2026/27. White ametoa asisti tatu, wakati Calafiori amefunga bao moja na kutoa asisti mbili.

Ni Josko Gvardiol wa Manchester City pekee mwenye mchango wa mabao manne, aliyefanikiwa kufanya vizuri zaidi ya wawili hao miongoni mwa mabeki.

Wawili hao wa Arsenal ni mfano mzuri wa namna mabeki wa pembeni wanavyoweza kuwa na mchango mkubwa katika soka la kisasa sawa na Chilambo wa Simba alivyo. Lakini, kutokana na majukumu ya nafasi hiyo kuongezeka, kila timu ya Ligi Kuu England inawatumiaje mabeki wake wa pembeni?


PATA 01

WENYE KAZI YAO

Zipo timu ambazo mabeki wake wa pembeni hugusa mpira, kwa kuzingatia umbali wao kutoka langoni na upana wa uwanja, lakini zipo zile ambazo mabeki wake hugusa mpira katika maeneo ya juu zaidi ya uwanja hadi zile zinazofanya hivyo katika maeneo ya chini.

Jambo linalojitokeza wazi ni kwamba mabeki wa pembeni wa Arsenal wana wastani wa kugusa mpira katika maeneo ya juu zaidi ya uwanja kuliko timu nyingine yoyote ya msimu huu. Wastani wao ni mita 58.2 kutoka kwenye lango lao.

Hali hiyo inaonyesha siyo tu namna Arsenal inavyotawala maeneo ya uwanja, bali pia uhuru wanaopewa White na Calafiori kujiunga na safu ya ushambuliaji.

White ana wastani wa kugusa mpira mara 3.4 ndani ya eneo la hatari la wapinzani kwa kila dakika 90, idadi kubwa zaidi kwa beki yeyote wa pembeni au wing-back katika ligi hiyo. Calafiori anashika nafasi ya tatu akiwa na wastani wa miguso 2.9.

Mabeki hao wa Arsenal pia wana wastani mdogo zaidi wa upana wa maeneo wanayogusa mpira ikilinganishwa na timu nyingine. Hii inasisitiza jinsi ambavyo wameachana na jukumu la jadi la mabeki wa pembeni kubaki katika maeneo ya nje ya uwanja ili kutoa upana wa mashambulizi.

Badala yake, wanahimizwa kuingia ndani na kufanya kazi katika maeneo ya kati ya uwanja.

Tottenham Hotspur pia inawatumia mabeki wake wa pembeni katika maeneo ya juu sana ya uwanja. Katika sehemu kubwa ya msimu huu, nafasi ya beki wa kulia imekuwa ikichezwa na Archie Gray, huku Andy Robertson akicheza upande wa kushoto.

Bila shaka, kuchambua mchango wa mchezaji hakupaswi kuishia katika kile anachokifanya akiwa na mpira pekee. Kupitia mfumo wa Opta Vision, unaweza pia kufuatilia kile anachokifanya wakati timu yake haina mpira. Gray anastahili kuangaliwa zaidi kutokana na uwezo wake mkubwa wa kufanya kazi uwanjani. Anaongoza mabeki wa pembeni wa ligi hiyi kwa idadi ya mbio za kuingia ndani (underlapping runs), akiwa na jumla ya mbio 23, sawa na wastani wa 2.9 kwa kila dakika 90.

Pia anashika nafasi ya nne kwa mbio za kupita nje ya mchezaji mwenzake (overlapping runs), akiwa na wastani wa 1.8 kwa kila dakika 90.

Takwimu hizo zinaonyesha faida ya kumtumia mchezaji mwenye mwelekeo wa kushambulia katika nafasi ya beki wa pembeni. Gray anaonyesha ubora, kasi na uwezo wa kupanda mbele ya mpira ili kutoa chaguo jingine la mashambulizi katika eneo la mwisho la uwanja. Robertson naye siyo mchezaji wa kupuuzwa katika upande wa pili wa uwanja.

PATA 05

Ingawa raia huyo wa Scotland ana umri wa miaka 32, bado anashika nafasi ya saba kwa mbio za kuingia ndani ya uwanja, akiwa na wastani wa 1.4 kwa kila dakika 90. Pia yumo katika 20 bora kwa mbio za kupita kando ya mchezaji mwenzake, akiwa na wastani wa 1.1.

Zaidi ya hapo, amepokea pasi nyingi zaidi zinazoishia katika eneo la mwisho la uwanja kuliko beki mwingine yeyote wa pembeni katika ligi hiyo msimu huu, akiwa na jumla ya pasi 159.

Huenda ikawa jambo la kushangaza kuona mabeki wa pembeni wa Coventry City wakicheza katika maeneo ya juu kiasi hicho, ikizingatiwa kuwa timu hiyo haijatawala sana umiliki wa mpira.

Coventry ina wastani wa umiliki wa mpira wa asilimia 39.1, ikiwa ya pili kutoka mwisho kwa takwimu hiyo. Pia huanzisha mashambulizi yake kutoka maeneo ya chini ya uwanja kwa wastani wa mita 40.2 kutoka langoni, ikiwa nafasi ya sita kutoka mwisho.

Hata hivyo, mbinu hiyo iliwasaidia vizuri katika Championship msimu uliopita ambapo walikuwa na wastani wa mita 56.8 kwa eneo la juu ambalo mabeki wao walikuwa wakigusa mpira, ikiwa ni takwimu ya sita kwa ukubwa.

Kocha Frank Lampard pia amekuwa akitumia mfumo wa mabeki watano katika baadhi ya mechi. Mfumo huo unawafanya wing-back wake kucheza katika maeneo ya juu zaidi ya uwanja.

Lakini, pia amekuwa jasiri kwa kuisogeza mbele safu yake ya ulinzi kwa ujumla. Coventry imewatega wapinzani wake kuotea mara 30, ikiwa timu ya pili kwa kufanya hivyo mara nyingi zaidi hadi sasa.

Hali hiyo imewapa Milan van Ewijk na Jay Dasilva nafasi ya kupanda mbele kupitia maeneo ya pembeni. Wachezaji hao wawili kila mmoja ametengeneza nafasi nane za kufunga, huku Jack Rudoni akiwa ndiye pekee aliyewaacha nyuma akiwa na nafasi 12 alizozitengeneza kwa Coventry.

Dasilva ni mchezaji muhimu zaidi katika upande wa kushoto. Anagusa mpira katika maeneo ya juu zaidi ya uwanja kuliko beki mwingine yeyote wa pembeni katika ligi hiyo.

Aidha, asilimia 42.2 ya nafasi zote za wazi za kufunga ambazo Coventry imezitengeneza zimetokea upande wake, ikiwa ni kiwango cha juu zaidi kwa timu yoyote ya ligi hiyo.


PATA 02

WING-BACK DHIDI YA FULL-BACK

Inaeleweka kuona mabeki wa pembeni wa Nottingham Forest na Leeds United wakigusa mpira katika maeneo ya juu ya uwanja, kwa kuwa timu hizo ni miongoni mwa zinazotumia zaidi mfumo wa wing-back. Timu hizo ni mbili kati ya nne pekee zinazotumia zaidi mfumo wa wing-back, huku mfumo wa mabeki watatu au watano kwa ujumla ukiendelea kuwa nadra katika Ligi Kuu England ya sasa.

Kwa upande wa Leeds, Jayden Bogle amekuwa na mchango mkubwa katika mashambulizi akiwa na  mbio nyingi zaidi zinazoishia ndani ya eneo la hatari la wapinzani kuliko beki mwingine yeyote wa pembeni msimu huu.

Ana wastani wa mbio 3.9 kwa kila dakika 90, kiwango cha pili kwa ukubwa katika ligi hiyo. Anayemzidi ni Nico O’Reilly wa Man City, ambaye amecheza asilimia 54.3 pekee ya dakika zake akiwa katika nafasi ya beki wa pembeni.

Wakati huohuo, Crystal Palace inapitia kipindi cha kumpoteza mchezaji wake muhimu, Daniel Munoz. Licha ya kutumia mfumo wa wing-back pekee, timu hiyo imeshuka kutoka kuwa na wastani wa nafasi za juu zaidi za mabeki wake wa pembeni katika ligi hiyo msimu huu hadi kuwa chini ya wastani wa ligi hiyo msimu huu.

PATA 04

Munoz alikuwa akifanya kazi kubwa ya kupanda na kushuka katika upande wa kulia wa uwanja msimu uliopita. Kutokuwepo kwake kumeathiri wazi uwezo wa Palace kumsukuma wing-back wake wa upande wa kulia kucheza katika maeneo ya juu na pembeni mwa uwanja.

Raia huyo wa Colombia sasa yupo Nottingham Forest pamoja na aliyekuwa kocha wake, Oliver Glasner. Nottingham Forest imepanda kutoka nafasi ya tano kutoka mwisho kwa wastani wa maeneo ambayo mabeki wake wa pembeni walikuwa wakigusa mpira hadi nafasi ya nne kwa kuwa na wastani wa juu zaidi.

Mabadiliko hayo hayajasababishwa na Munoz pekee, lakini kuwa na mchezaji anayeweza kufanya mbio nyingi na zenye nguvu katika muda wote wa mchezo kunasaidia sana. Munoz anashika nafasi ya pili nyuma ya Leif Davis wa Ipswich Town kwa wastani wa urefu wa mbio anazofanya wakati timu yake haina mpira.

Hatuwezi kuzungumzia mabeki wa pembeni wenye ubora na kasi kubwa katika ligi hiyo bila kumtaja Adrien Truffert, ambaye ameendelea na kiwango alichomalizia msimu uliopita.

Raia huyo wa Ufaransa ndiye mfalme wa mbio za kupita nje ya mchezaji mwenzake (overlapping runs), akiwa amefanya mbio 23, idadi kubwa zaidi kuliko beki mwingine yeyote wa pembeni katika ligi hiyo. Hiyo ni baada ya msimu uliopita kufanya karibu mara mbili ya mbio hizo kuliko mchezaji mwingine yeyote katika ligi nzima.

Ingawa kocha wake wa zamani, Andoni Iraola, ameondoka, Truffert bado amepewa uhuru huohuo wa kupanda kwa kasi katika mashambulizi chini ya kocha mpya wa Bournemouth, Marco Rose.


PATA 03

KUENDELEZA MFUMO AU KUBADILIKA?

Iraola sasa yupo Liverpool, na mabeki wake wa pembeni ni miongoni mwa wawili wenye majukumu yanayotofautiana zaidi katika ligi hiyo. Milos Kerkez, kama alivyokuwa akifanya alipokuwa Bournemouth chini ya Iraola, amepewa uhuru wa kupanda mbele na ni miongoni mwa mabeki wanaofanya mara nyingi mbio za kupita kando ya mchezaji mwenzake. Hadi sasa amefanya mara 15.

Katika upande mwingine, Ronald Araujo, ambaye awali alikuwa beki wa kati kabla ya kubadilishiwa nafasi, anatekeleza majukumu ya tahadhari zaidi katika ulinzi. Manchester City nayo ni timu inayovutia kuifuatilia.

Licha ya kuwa na wastani mkubwa zaidi wa umiliki wa mpira katika ligi hiyo, asilimia 65.4, kuwa na pasi nyingi zaidi kwa kila mchezo kuliko timu nyingine yoyote (566), na kuongoza kwa utawala wa maeneo ya uwanja unaopimwa kwa takwimu, kikosi hicho cha Enzo Maresca hakiwatumii mabeki wake wa pembeni katika maeneo ya juu ili kuendeleza utawala huo.