Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Jake anunua ranchi, mabilioni ya pambano la Tyson

JAKE Pict

Muktasari:

  • Jake, katika pambano hilo alivuna zaidi ya Dola 70 milioni, huku Tyson akikunja 90 milioni, ambapo walimalizana kwa kumchapa nmkongwe huyo kwa pointi za majaji.

GEORGIA, MAREKANI: KAMA utani vile! Lakini, huo ndio ukweli. Bondia wa ngumi za maonyesho mitandaoni na mtengeneza maudhui mitandaoni, Jake Paul amenunua ranchi yenye thamani ya Dola 40 milioni (zaidi ya Sh90 bilioni), alizopata kutokana na pambano dhidi ya Mike Tyson, mwaka jana.

Jake, katika pambano hilo alivuna zaidi ya Dola 70 milioni, huku Tyson akikunja 90 milioni, ambapo walimalizana kwa kumchapa nmkongwe huyo kwa pointi za majaji.

Hata hivyo, miezi michache baadaye yaani Desemba 19, mwaka huo alizichapa tena na Anthony Joshua katika pambano ambalo lilimuingizia zaidi ya Dola 60 milioni, lakini likimuacha akiuguza jeraha baada ya taya la kulia kuvunjika na hivyo kumlazimu kutumia takriban wiki mbili akiwa amelazwa hospitali.

JAK 05

Pamoja na maumivu hayo, Jake anayekadiriwa kuwa na utajiri wa Dola100 milioni anaendelea kuwekeza na hivi karibuni alinunua ranchi huko Georgia aliyodai fedha zimetokana na pambano lake dhidi ya Tyson lililopigwa Novemba 17, mwaka juzi, chini ya udhamini wa Netflix.

Kwa mujibu wa bondia huyo aliyeibuka ghafla mwaka jana huko mitandaoni, pesa zilizotokana na pambano hilo amemega kiasi na kununua eneo hilo lenye ukubwa wa ekari 179 ambalo lilikuwa likitumiwa kwa ajili ya ufugaji wa mifugo ya aina mbalimbali ikiwamo ng’ombe, kondoo na nguruwe.

Ndani ya takriban mwezi mmoja ameanza kulifanyia mabadiliko ya kasi, kwani licha ya kuwa na uwanja mdogo wa ndege hivi sasa anakamilisha kujenga barabara za kuendeshea magari ya mashindano kama yale yanayotumiwa kwa mbio za Formula One.

Na katika katika kuonyesha kwamba hana kinyongo kuonyesha mafanikio anayopata kutokana na kile anachokifanya, Jake aliwaalika baadhi ya mashabiki wake kufanya ziara katika ranchi hiyo ambayo amekuwa akiibadilisha kwa kiwango kikubwa.

JAK 04

Tangu amshinde Tyson, Jake ameonekana mara mbili zaidi ulingoni jambo lililoongeza fedha za ukarabati na maendeleo ya ranchi yake, kwani Juni 2025 alipata ushindi wa pointi zote dhidi ya Julio Cesar Chavez Jr kabla ya kupata kipigo kizito kutoka kwa Joshua miezi sita baadaye.

Akiwa bado anaendelea kupona majeraha, Jake aliyebadilika kuwa bondia ameongeza mambo ya kuvutia katika ranchi hiyo anayoiita ‘Paul Reserve’.

“Tutajenga uwanja wa ndege (airstrip) ili ndege ya Global Express ya Paul Air iweze kutua,” alisema wakati akizungumza na baadhi ya mashabiki wake.

JAK 03

“Huu utakuwa uwanja kamili wa kutua ndege unaochukua takribani maili moja na nusu, na tutakuwa na ujenzi wa barabara kamili za mbio za Formula 1 (F1) katika eneo hili lote ambalo ni tambarare. Nina magari mazuri, kila mtu ana magari mazuri, lakini wengi wanayaendesha tu barabarani. Nataka kufanya mambo kinyume.

“Nataka kwanza nijenge barabara ili niweze kuyaendesha magari yangu ipasavyo, kisha niendelee kuongeza idadi ya  magari ikiwa ni pamoja na magari ya mbio zaidi na hata ya mashi-ndano.

“Lakini pia nitaibadilisha hii ranchi kuwa klabu ya wanachama, ambapo watu wanaweza kuwa na nyumba karibu na barabara za mbio za magari, kupaki magari yao kwenye gereji, kuwa na nafasi ya kuishi, kutumia barabara wakati wowote watakapopenda, kutua na kupaa kwa ndege kwenye uwanja wa ndege, na kuunda aina fulani ya klabu ya mashindano ya magari.”

JAK 01

NINI KINGINE?

Ndani ya eneo hilo kuna nyumba nne pamoja na jengo la mikutano lililojengwa. Pia kuna gym ya mazoezi ya ngumi yenye ulingo uliojengwa mahsusi ili Jake ajifunze na kufanya mazoezi akiwa kwenye eneo lake. Vilevile ana majengo ya kuhifadhia vifaa na mahitaji mbalimbali pamoja na kituo chake binafsi cha mafuta kwa ajili ya magari yanayotumika ndani ya ranchi. Eneo hilo pia lina sehemu nyingi za michezo mbalimbali ikiwamo ya majini, hivyo Paul na wageni wake watakuwa na vitu vingi vya kuwaburudisha.

JAK 02

KWA NINI RANCHI?

Jake alikuwa tayari amenunua jumba la kifahari lenye thamani ya Pauni 13 milioni huko Puerto Rico 2023, lakini alikuwa na ndoto ya kumiliki ranchi kwa zaidi ya miaka 15.

Alitimiza ndoto hiyo mwaka jana kwa kununua mali hiyo na hapa anadai: “Kulikuwa na mambo kadhaa muhimu niliyohitaji katika uwekezaji huu wa ndoto yangu. Kwanza, nilitaka iwe karibu na ziwa ambako unaweza kufanya lolote, kuendesha jet ski na kujifurahisha. Pia nilitaka kujenga uwanja wa ndege, hivyo ilihitaji ardhi tambarare ya kutosha kutua ndege kubwa na pia kujenga barabara za magari ya mbio.

“Katika maeneo mengi kama Tennessee, kuna mabonde mengi na hakuna ardhi ya kutosha tambarare,” anasema.

“Zaidi ya hayo, sikutaka hali ya hewa iwe baridi. Nimewahi kwenda kwenye ranchi ya kaka yangu ambayo ipo milimani. Hali ya hewa hubadilika kila dakika na miezi mingi kuna baridi kwa hadi miezi sita.”