Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hongera Nado madai yako yalikuwa sahihi

NADO Pict

Muktasari:

  • Kuna timu mojawapo kubwa nchini tofauti na Azam ambayo wambea wanatujuza ilikuwa imekaa mkao wa kula imchukue iwapo atashindwana na klabu yake.

TUNASIKIA sikia tu hapa kijiweni Iddy Nado alichelewa sana kukubaliana na Azam FC kwa ajili ya kusaini mkataba mpya.

Baada ya mkataba wake uliopita kumalizika kijiwe kimenasa za ndaani, mabosi wa Azam FC walimuita mezani wakiwa na mkataba mpya lakini Nado hakuridhika na hela aliyowekewa mwanzoni.

Kuna timu mojawapo kubwa nchini tofauti na Azam ambayo wambea wanatujuza ilikuwa imekaa mkao wa kula imchukue iwapo atashindwana na klabu yake.

Hata hivyo, mambo yalijipa na Nado akaanguka saini ya kuendelea kuitumikia Azam FC na sisi hatujui kama ndio alipewa mzigo huo aliokuwa anautaka au vinginevyo lakini muhimu amebakia.

Sasa mchezaji anapodai ongezeko la mshahara au dau la kusaini, anapaswa pia anachokifanya uwanjani kiendane au kikaribiane na kile anachotaka ili kuwepo na thamani ya fedha ya huduma yake kwa timu.

Sio tu kiwango chenyewe cha kuungaunga na hauna mchango wowote mkubwa kwenye timu halafu unalilia mkataba mnono. Hiyo haiwezekani.

Sasa kijiwe kinampongeza Iddy Nado kwa vile ndani ya muda mfupi amethibitisha kwa vitendo alikuwa ana haki kuomba Azam FC impe mzigo mrefu wakati wa majadiliano ya mkataba mpya.

Nado ndiye ameifanya Azam FC leo hii iwe na furaha ya kuingia hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika na isingekuwepo pengine leo stori ingekuwa tofauti na labda Azam FC isingesonga mbele.

Katika hatua ambayo Azam FC wametoka kucheza, mechi ya kwanza ugenini Misri dhidi ya ZED FC, Nado ndiye aliyefunga bao la kusawazisha na katika mechi ya marudiano hapa Dar es Salaam ndio alifunga bao pekee la ushindi.