Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hawa hapa nyota sita Serie A waliopanda thamani

SERIE A Pict

Muktasari:

  • Kama ilivyo kwa moboresho mengi yanayofanyika Septemba na Oktoba, tathmini hii imejikita zaidi kwa wachezaji wachache walioanza msimu kwa kiwango kizuri au ambao hivi karibuni walihama klabu kwa ada kubwa za uhamisho. Kutokana na hilo, hakujawa na mabadiliko makubwa katika kilele cha orodha ya wachezaji wenye thamani kubwa Serie A.

MILAN, ITALIA; BAADA ya ligi mbalimbali Ulaya kurejea zikitokea katika dirisha refu la usajili, Transfermarkt imefanya maboresho ya thamani za soko kwa wachezaji 134 wa Ligi Kuu Italia (Serie A).

Kama ilivyo kwa moboresho mengi yanayofanyika Septemba na Oktoba, tathmini hii imejikita zaidi kwa wachezaji wachache walioanza msimu kwa kiwango kizuri au ambao hivi karibuni walihama klabu kwa ada kubwa za uhamisho. Kutokana na hilo, hakujawa na mabadiliko makubwa katika kilele cha orodha ya wachezaji wenye thamani kubwa Serie A.

Katika kilele hicho Lautaro Martinez wa Inter Milan ana thamani ya Euro 85 milioni akifuatiwa na Nico Paz wa Como mwenye Euro 80 milioni, huku Kenan Yıldız wa Juventus akithaminishwa kwa Pauni 75 milioni. Mabadiliko mengi yametokea chini ya wachezaji hao watatu, huku nyota wawili wa AS Roma wakivutia zaidi sokoni; lakini wengine katika orodha ni hawa hapa chini.

Kone Euro 60 milioni

Mmoja wa waliopanda thamani ni kiungo wa kimataifa wa Ufaransa, Manu Kone, anayekipiga AS Roma na meneja wa Transfermarkt, Jatin Dietl, anasema: “Ubora wa Manu sasa unajulikana vizuri, na siyo bahati kwamba huvutia katika karibu kila dirisha la usajili.”

Kwa mujibu wa Dietl, mchanganyiko wa nguvu, kukokota mpira, kuhimili presha na ushindani katika mipambano unamfanya kuwa kiungo kamili wa kisasa. Kwa muda mrefu kulikuwa na taarifa kwamba Roma huenda ingelazimika kumuuza ili kushughulikia suala lake la mizania ya kifedha, huku hata kiasi cha chini ya thamani yake ya awali kikitajwa. Hata hivyo, Roma ilionyesha msimamo kwa kukataa ofa zilizowasilishwa.

Dietl alisema: “Katika soko la sasa, Euro 60 milioni inaonekana kuwa kiwango cha chini kwa kiungo mwenye wasifu, umri na ubora wake.”

Kutokana na hilo, thamani mpya ya Kone imefikia Pauni 60 milioni, ikiwa ni ongezeko la Pauni 10 milioni kutoka thamani yake ya awali.

Malen Euro 55 milioni

Miongoni mwa walionufaika zaidi na tathmini hiyo ni mwenzake Kone katika kikosi cha AS Roma, Donyell Malen ambaye anaelezwa athari yake kwa timu pinzani Serie A imekuwa kubwa. Malen tayari amefunga zaidi ya mabao 20 kwa Roma, licha ya kujiunga na klabu hiyo katika dirisha la usajili la Januari mwaka jana.

Na iwapo ataendelea kutupia nyavuni atapaswa kuhesabiwa miongoni mwa wanaowania tuzo ya Capocannoniere inayotolewa kwa mfungaji bora wa Serie A. Hata hivyo, umri wake pamoja na ukweli kwamba hakuwahi kushawishi kikamilifu akiwa Ligi Kuu England umezingatiwa katika tathmini hiyo. Thamani ya Malen imeongezeka kwa Euro 10 milioni kutoka milioni 45.

Baturina Euro 55 milioni

Transfermarkt imeongeza thamani za wachezaji kadhaa wa Como, akiwemo Martin Baturina ambaye ameendelea pale alipoishia mwishoni mwa msimu uliopita akikiwasha vilivyo.

Kinachomtofautisha ni namna anavyocheza bila kuonekana mwenye haraka au presha, akipokea mpira katikati ya mistari, kusoma matukio mapema na kutengeneza nafasi bila kulazimisha mchezo. Sasa Baturina ana nafasi ya kuonyesha uwezo wake pia katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Thamani ya Baturina imeongezeka kwa Euro 10 milioni kutoka Euro 45 milioni hadi Euro 55 milioni.

Esposito Euro 50 milioni

Kwa upande wa Inter Milan, jina linaloibuka ni Pio Esposito ambaye kwa sasa anacheza kwa utulivu na kuonyesha uzoefu wa kipeee mbele ya lango anaposhambulia. Nguvu zake za kimwili zinamwezesha kukabiliana na mabeki wa kati, huku uwezo wake wa kumiliki mpira, kutoa pasi za haraka na kuboresha mwendo vikimfanya kuwa zaidi ya mshambuliaji anayesubiri mipira ndani ya boksi. Thamani ya Esposito imeongezeka kwa Euro 5 milioni kutoka Euro 45 milioni hadi 50 milioni.

Ramon Euro 45 milioni

Ongezeko kubwa zaidi kwa upande wa Como limemkuta beki wa kati Jacobo Ramon, ambaye thamani yake imepanda kwa Euro 15 milioni, kutoka Euro 30 milioni hadi Euro 45 milioni, na kwa sasa kwa wengi anaingia miongoni mwa mabeki wanne au watano bora wa kati katika ligi.

Kwa mujibu wa Transfermarkt, Ramon anaonekana kuwa beki wa kisasa mwenye nafasi kubwa ya kuendelea kukua. Wengine Como walioongezeka thamani ni Assane Diao kutoka Euro 5 milioni hadi Euro 35 milioni, Lucas Da Cunha (Euro 10 milioni hadi Euro 30 milioni) na

Luis Milla aliyepanda kutoka Euro 4.5 milioni hadi Euro 8 milioni.

Moreira Euro 45 milioni

Kwa upande mwingine, Diego Moreira wa AC Milan amepanda thamani kutokana zaidi na ada kubwa ya uhamisho aliyonunuliwa sambamba na anachokifanya uwanjani, ambapo kiungo huyo wa kimataifa wa Ubelgiji ameongezeka kwa Euro 20 milioni kutoka Euro 25 milioni hadi 45 milioni. Kilichombeba zaidi ni wasifu unaovutia kutokana na kasi yake ya ghafla, uwezo wa kucheza mmoja dhidi ya mmoja na kubadilika na kucheza kama winga au wing-back upande wowote. Milan imewekeza kwa mchezaji ambaye bado ana miaka 22, hivyo ana nafasi kubwa ya kuendelea kukua.