Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hata Dladla mwenyewe anamheshimu Barker

DADLA Pict

Muktasari:

  • Na kuna wachambuzi fulani hivi wamekuwa wakimponda Barker tangu alipokuja nchini hadi leo kwamba sio kocha mzuri na hana mbinu hivyo Simba inashinda kwa nguvu na uwezo wa wachezaji.

BAADHI ya ndugu zetu wachambuzi wanapaswa kumpa heshima Steve Barker hata kama hawapendi kufanya hivyo kwa mitazamo yao.

Na kama wanaona ni nyoyo zao zinawakataza kumheshimu Steve Barker basi wafanye angalau kinafiki tu vinginevyo ni kama wanajidhalilisha tu.

Kijiwe kimeona kuna ripoti imetolewa sijui kwamba Kaimu Kocha Mkuu wa Yanga, Simo Dladla yupo katika orodha ya makocha bora 10 Afrika na Barker hayupo.

Na kuna wachambuzi fulani hivi wamekuwa wakimponda Barker tangu alipokuja nchini hadi leo kwamba sio kocha mzuri na hana mbinu hivyo Simba inashinda kwa nguvu na uwezo wa wachezaji.

Hata kama kila mtu ana maoni na mtazamo wake lakini kuna mambo huwa yanaonekana wazi na ukiyapinga basi utakuwa umeamua tu kufanya hivyo na mojawapo ndio kama hilo la kubeza uwezo wa Steve Barker.

Huyo Steve Barker kabla hata hajaja nchini alishapata mafanikio ya kuipeleka timu ya daraja la kawaida ya Stellenbosch katika nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika na akaifanya iwe miongoni mwa timu shindani kule.

Alipokuja hapa hadi leo ameiongoza Simba kutopoteza mechi yoyote ya Ligi Kuu Tanzania Bara na kati ya hizo, mechi 20 ameshinda mfululizo jambo ambalo kiuhalisia sio rahisi.

Halafu katika hali ya kawaida Dladla alikuwa Kocha Msaidizi Yanga inawezekana vipi mechi mbili tu zikatosha kumpa hiyo hadhi ya ubora kumzidi Barker ambaye amepruvu hapa Tanzania na Afrika Kusini akiwa Kocha Mkuu?

Kijiwe kinaamini kwamba hata huyo Simo Dladla anashangaa kupewa sifa za kumzidi mtu kama Barker ambaye kwa huko Afrika Kusini wanamtazama kama mmoja wa vioo vya makocha wanaochipukia kama yeye.