Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Geita Gold angalieni msimamo wa Ligi Kuu

GEITA Pict

Muktasari:

  • Fountain Gate inayoshika mkia na Pamba Jiji iliyo katika nafasi ya 15 kwenye msimamo wa ligi, kila moja mmeipita kwa tofauti ya pointi mbili maana zenyewe kila moja ina pointi tano.

WANETU wa Geita Gold kabla ya yote angalieni msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu halafu kijiwe kiwaambie jambo.

Mpo nafasi ya 12 katika msimamo baada ya mechi nane mlizocheza mkiwa na pointi saba tu mlizopata kwa kushinda mechi mbili na kutoka sare moja.

Haya kuna timu nne tu ambazo mmezipita hadi sasa ambazo ni Fountain Gate, Pamba Jiji, Kagera Sugar na TRA United.

Fountain Gate inayoshika mkia na Pamba Jiji iliyo katika nafasi ya 15 kwenye msimamo wa ligi, kila moja mmeipita kwa tofauti ya pointi mbili maana zenyewe kila moja ina pointi tano.

Kagera Sugar iliyo nafasi ya 14 na TRA United iliyopo katika nafasi ya 15, kila moja mmeipita kwa pointi moja kwa vile kila timu ina pointi sita.

Hapa kijiweni tuliwaambia muangalie kwanza msimamo wa ligi kwa sababu tunahisi labda mnajiona mko salama kwa vile hamko katika nafasi mbili za mwisho ambazo timu zinazomaliza hapo zinashuka daraja moja kwa moja au nafasi ya 14 na 13 ambazo timu zitakazomaliza hapo zitacheza mchujo.

Sasa kiuhalisia hamko salama na mkiendeleza kupoteza pointi mtajikuta mnapishana na hizo timu mlizozitangulia kwa zenyewe kusogea juu na nyie kushuka chini.

Hayo mambo yenu ya kucheza mechi tano mfululizo bila kupata ushindi sio jambo la kulichukulia poa na mkiruhusu liendelee muda sio mrefu mtaanza kupambana kujinasua kutoka chini au hata kushuka daraja kabisa.

Kuna wenzenu walichukulia poa msimamo wa ligi huko nyuma na yakawakuta ya kuwakuta. Nyie msithubutu kujichanganya.