Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Fei Toto amewaacha mbali sana wazawa

AKILI - FEI Pict

Muktasari:

  • Tangu alipojiunga na timu hiyo amekuwa akifanya mambo makubwa tena kwa muendelezo tofauti na wenzake ambao amewapiku kwa ukubwa sana na takwimu zinazungumza.

KUNA kiumbe mmoja anawachonganisha sana wachezaji wenzake pale Azam FC. Anaitwa Feisal Salum ‘Fei Toto’.

Tangu alipojiunga na timu hiyo amekuwa akifanya mambo makubwa tena kwa muendelezo tofauti na wenzake ambao amewapiku kwa ukubwa sana na takwimu zinazungumza.

Kwa mfano tu, msimu huu ndiye mchezaji anayeongoza kwa kuhusika na idadi kubwa ya mabao katika Ligi Kuu ya NBC akihusika na mabao 11.

Mgawanyo wa mabao hayo ni matano yakiwa ni yale aliyofunga na mabao mengine matano ni yale aliyozalisha kwa kupiga pasi za mwisho kwa lugha ya kigeni zinaitwa asisti.

Msimu uliopita alihusika na mabao 19, akifumania nyavu mara sita na kupiga pasi 13 za mwisho ambazo zilimfanya awe kinara wa kupiga asisti katika Ligi Kuu na akishika naasi ya tatu kwa kuhusika na idadi kubwa ya mabao.

Katika msimu wa 2023/2025, Feisal alifunga mabao 19 na kupiga pasi za mwisho saba kwa maana kiujumla alihusika na mabao 26.

Hizi ni takwimu ambazo hakuna mchezaji mwingine wa Azam FC au mzawa anayecheza kwenye ligi yetu ambaye angalau kajaribu kuzifikia au anaonekana ana dalili kuwa anaweza akabishana na Zanzibar Finest.

Kwa bahati mbaya kutofanya vizuri kwa Azam FC kwenye Ligi, kunaminya fursa kwa Fei Toto kuteka mijadala ya soka nchini kwa vile wengi wanajikuta wanalazimika kujadili Azam FC kutofanya vizuri huku wakimsahau Feisal.

Kama Azam ingekuwa inatamba kwenye ligi yetu, pengine Fei Toto angezoa sifa hadi nyingine zingemwagika.