Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Faida saba za alovera kwenye ngozi

Muktasari:

  • Mmea huo ni mualovera maarufu kama Alovera, ambao umekuwa ukitumika kwa muda mrefu katika utunzaji wa ngozi kutokana na ute wake wenye maji mengi na viambato mbalimbali vinavyoweza kusaidia kuitunza ngozi.

UNAWEZA kutumia fedha nyingi kununua mafuta ya kulainisha ngozi, krimu za kuondoa madoa na bidhaa za urembo, lakini wakati mwingine suluhisho la baadhi ya changamoto ndogo za ngozi linapatikana kwenye mmea unaoweza kuupata hata nyumbani.

Mmea huo ni mualovera maarufu kama Alovera, ambao umekuwa ukitumika kwa muda mrefu katika utunzaji wa ngozi kutokana na ute wake wenye maji mengi na viambato mbalimbali vinavyoweza kusaidia kuitunza ngozi.

Wapo wanaoutumia kupaka usoni, mikononi, miguuni na sehemu nyingine za mwili wakiamini unaweza kusaidia kuondoa chunusi, madoa meusi, ukavu na hata kufanya ngozi ing’ae. Lakini je, ni faida zipi ambazo zinaungwa mkono na ushahidi wa kisayansi na zipi ni imani zinazohitaji uthibitisho zaidi?

Kwa mujibu wa wataalamu wa ngozi, Alovera ina viambato vinavyoweza kuwa na mchango katika kutuliza ngozi, kuongeza unyevunyevu na kupunguza baadhi ya dalili za muwasho. Jeli yake ina takribani asilimia 99 ya maji, huku sehemu iliyobaki ikiwa na sukari, vitamini, madini na viambato vingine.

Utafiti uliochapishwa mwaka 2024 katika jarida la Journal of Burn Care & Research, uliochambua majaribio tisa ya kitabibu, ulionyesha kuwa matumizi ya Alovera yalipunguza muda wa kupona kwa wagonjwa wenye majeraha ya kuungua kwa kiwango cha pili kwa wastani wa siku 3.76 ikilinganishwa na baadhi ya matibabu mengine ya kupaka.

Hizi hapa faida nane za mwalovera ambazo unapaswa kuzifahamu.


1. KULAINISHA NGOZI

Miongoni mwa faida zinazotajwa za mwalovera ni uwezo wake wa kusaidia kuongeza unyevunyevu kwenye ngozi. Ute wake una maji mengi ambayo husaidia ngozi isikauke na kuwa na hali ya kukakamaa.

Unapotumia Alovera, inaweza kusaidia kuifanya ngozi kuwa laini na yenye unyevunyevu zaidi. Hii ni faida kwa watu wenye ngozi kavu wanaotafuta bidhaa nyepesi ya kujipaka.


2. HUTULIZA NGOZI   YENYE MUWASHO

Mwalovera una viambato vinavyoweza kusaidia kupunguza uchochezi na kutuliza ngozi yenye muwasho mdogo.

Mtu anayesumbuliwa na muwasho unaotokana na ukavu au bidhaa fulani za urembo anaweza kupata nafuu kwa kutumia bidhaa inayofaa yenye Alovera. Hata hivyo, muwasho unaoendelea unahitaji uchunguzi wa kitabibu ili kujua chanzo chake.


3. HUPUNGUZA CHUNUSI

Taarifa za Taasisi ya Taifa ya Afya ya Nyongeza na Tiba Jumuishi ya Marekani (NCCIH) zinaeleza kuwa tafiti ndogo mbili zimeonyesha uwezekano wa ute wa Alovera, ikitumika pamoja na matibabu mengine, kusaidia kuboresha chunusi.

Hata hivyo, mwalovera pekee haujathibitishwa kuwa tiba ya kuondoa chunusi zote.

4. HUSAIDIA NGOZI ILIYOATHIRIWA NA JUA

Unapokaa muda mrefu juani, ngozi inaweza kupata wekundu, joto na maumivu kutokana na mionzi ya jua.

Ute wa  Alovera unasaidia kutuliza ngozi yenye usumbufu unaotokana na kuungua na jua kwa  kiwango kidogo. Inaweza kutoa hali ya ubaridi na kusaidia ngozi kupata unyevunyevu. Hata hivyo, haitoi kinga dhidi ya mionzi ya jua na haiwezi kuchukua nafasi ya mafuta ya kujikinga na jua (sunscreen).


5. KUPUNGUZA MUDA WA KUPOA KWA MAJERAHA YA KUUNGUA

Hii ni miongoni mwa faida ambazo zina ushahidi wa kitabibu unaovutia zaidi.

Utafiti wa mwaka 2024 uliochapishwa katika Journal of Burn Care & Research ulichambua majaribio tisa ya kitabibu na kubaini kuwa Alovera ilipunguza muda wa kupona kwa majeraha ya kuungua kwa kiwango cha pili kwa wastani wa siku 3.76 ikilinganishwa na baadhi ya bidhaa nyingine zilizotumika kwenye majaribio hayo.

Hata hivyo, majeraha makubwa ya kuungua yanahitaji huduma ya hospitali na si vizuri kujitibu nyumbani kwa kutumia mmea huo.


6. HUSAIDIA KUTULIZA NGOZI ILIYOATHIRIKA NA MATIBABU

Baadhi ya wagonjwa wanaopata matibabu ya mionzi wanaweza kupata mabadiliko kwenye ngozi, ikiwamo ukavu, wekundu na muwasho.

Alovera imefanyiwa tafiti kuhusu uwezo wake wa kusaidia ngozi katika hali hiyo. Wagonjwa wanashauriwa kutumia bidhaa za ngozi kwa maelekezo ya wataalamu wanaowahudumia.


8. KUBORESHA MWONEKANO WA NGOZI KAVU

Mwalovera unaweza kusaidia ngozi iliyopoteza unyevunyevu na kuifanya ionekane yenye ulaini zaidi.

Unapopaka jeli yake, husaidia kuongeza unyevunyevu na kupunguza hali ya ngozi kuwa na ukakasi unaotokana na ukavu.

USHAURI WA DAKTARI

Daktari wa ngozi Dorcas Natse anashauri kuwa matumizi ya mwalovera yanapaswa kuzingatia aina ya ngozi na tatizo linalotakiwa kutatuliwa.

“Ni muhimu kutumia ute safi uliotengenezwa kwa matumizi ya ngozi na kujaribu kiasi kidogo kwenye sehemu ya ngozi kabla ya kuipaka mwili mzima. Baadhi ya watu wanaweza kupata mzio unaojitokeza kwa wekundu, kuwashwa, vipele au hisia za kuungua baada ya kutumia Aloe vera.