Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

EPL utamu umerudi ni wikiendi ya vicheko, vilio

EPL Pict

Muktasari:

  • Hadi sasa, Manchester City ndiyo timu pekee iliyoshinda mechi zote baada ya Arsenal kufungwa mabao 3-0 na Brighton, ambayo sasa inashika nafasi ya tatu.

LONDON, ENGLAND: LIGI Kuu England inarejea baada ya mapumziko ya mechi za kimataifa, huku utabiri wa mechi za raundi ya sita za msimu wa 2026/27 ukitolewa na baadhi ya mitandao ya ubashiri ikiwamo Opta.

Hadi sasa, Manchester City ndiyo timu pekee iliyoshinda mechi zote baada ya Arsenal kufungwa mabao 3-0 na Brighton, ambayo sasa inashika nafasi ya tatu.

Brentford, Leeds United, Liverpool na Everton bado hazijapoteza, huku Tottenham Hotspur ikiwa mkiani mwa msimamo.

Tottenham bado haijashinda ligi msimu huu, ingawa ilifunga mabao yake ya kwanza katika kipigo cha 3-2 dhidi ya Aston Villa.

Fulham na Bournemouth nazo bado hazijashinda, ilhali Coventry City ilipata ushindi wake wa kwanza kabla ya mapumziko.

Kuelekea mechi za wikiendi hii Arsenal ndiyo inayopendelewa zaidi kushinda raundi ya sita, ikiwa na uwezekano wa asilimia 68.9 dhidi ya Leeds United.

Everton ina uwezekano wa asilimia 45.7 wa kuifunga Hull City ugenini, huku Newcastle na Manchester City nazo zikitabiriwa ushindi ugenini.

Kwa asilimia 28.8, mchezo wa Crystal Palace dhidi ya Nottingham Forest una uwezekano mkubwa zaidi wa kuisha kwa sare.


EP 01

ARSENAL VS LEEDS UNITED

Arsenal itarejea uwanjani leo Jumamosi ikilenga kurekebisha makosa baada ya kipigo cha mabao 3-0 dhidi ya Brighton.

Hicho kilikuwa kipigo chake kikubwa zaidi tangu Mei 2023, ilipofungwa na Brighton kwa matokeo hayo.

Tangu mwanzoni mwa 2024, Arsenal imepoteza mechi mbili mfululizo za ligi mara moja tu, Aprili 2026.

Arsenal imeshinda mechi tisa kati ya 10 zilizopita dhidi ya Leeds, huku nyingine ikiisha kwa sare.

Leeds imeshinda mchezo mmoja kati ya 17 iliyopita ya ligi ikiwa ugenini dhidi ya mabingwa watetezi.

Arsenal inapewa uwezekano wa asilimia 68.9 wa kushinda dhidi ya 13.7 za Leeds. Hata hivyo, Leeds imeanza msimu bila kupoteza mechi tano za mwanzo ikishinda mara mbili na sare tatu.


EP 02

ASTON VILLA VS BRENTFORD

Aston Villa, inayopewa asilimia 47.8 za ushindi itaikaribisha Brentford yenye uwezekano wa asilimia 26.2.

Brentford haijapoteza mechi saba zilizopita za ligi ya daraja la juu na inalenga kushinda dhidi ya Villa kwa mara ya tatu mfululizo katika ligi. Villa imepoteza mchezo mmoja kati ya 11 iliyocheza nyumbani dhidi ya Brentford.

Hata hivyo, msimu huu imerekodi mashuti 48, ikiwamo yaliyolenga lango 12 na miguso 81 ndani ya eneo la hatari la wapinzani, idadi ndogo zaidi katika mashindano hayo.


EP 03

CHELSEA VS BOURNEMOUTH

Chelsea ya Xabi Alonso inalenga kumaliza mfululizo wa mechi tatu bila ushindi katika mashindano yote.

Katika mechi tano za ligi chini ya Alonso, Chelsea imefunga mabao 10 na kuruhusu 12. Chelsea inapewa uwezekano wa asilimia 51.8 wa kushinda dhidi ya Bournemouth ikiwa haijapoteza mechi tisa zilizopita dhidi ya Bournemouth katika ligi ya daraja la juu ikishinda mara nne na sare tano.


EP 03 (1)

IPSWICH VS FULHAM

Ipswich inapewa uwezekano wa asilimia 44.8 wa kushinda dhidi ya Fulham. Hata hivyo, haijashinda mechi saba zilizopita za ligi dhidi ya Fulham.

Fulham nayo haijashinda katika mechi zake nne za ligi ya daraja la juu dhidi ya Ipswich, ikiwa na sare tatu na kipigo kimoja.

Kwa ujumla Fulham imepoteza mchezo mmoja kati ya 15 iliyopita Ligi Kuu England dhidi ya timu zilizopanda daraja, ikiwa na ushindi mara tisa na sare tano.


EP 05

SUNDERLAND VS BRIGHTON

Brighton imeshinda mechi mbili za mwisho kwa jumla ya mabao 8-0. Inaongoza ligi kwa mipira 56 iliyopokonya wapinzani katika maeneo ya juu, huku ikiwa na umiliki wa mpira wa asilimia 64.8.

Brighton inapewa uwezekano wa asilimia 41.3 wa kushinda dhidi ya asilimia 33.1 za Sunderland, ambayo imepoteza mechi mbili mfululizo.


EP 06

MAN UNITED VS TOTTENHAM

Manchester United imekusanya pointi tano katika mechi tano za mwanzo, ikiwa na wastani wa pointi moja kwa kila mchezo.

Tottenham nayo imekusanya pointi 18 pekee mwaka 2026 miongoni mwa timu ambazo hazijawahi kushuka daraja tangu zilipopanda Ligi Kuu England.

Katika mecho baina ya timu hizo mbili Man United inapewa asilimia 54.1 wa kushinda, huku Tottenham ikiwa na 22.3.


EP 07

PALACE VS NOTTINGHAM

Mchezo huo una uwezekano wa asilimia 28.8 wa kuisha kwa sare. Crystal Palace inapewa asilimia 36.3 ya ushindi, huku Nottingham Forest ikiwa na 34.9.

Forest imepoteza mchezo mmoja kati ya saba iliyocheza ugenini katika ligi, ikiwa na ushindi mara nne na sare mbili. Pia imefunga angalau mabao mawili katika kila mechi hizo saba.


EP 08

HULL CITY VS EVERTON

Hull City ndiyo timu pekee ambayo bado haijaruhusu bao nyumbani katika ligi hiyo msimu huu ambapo umiliki wake wa mpira wa asilimia 32.3 ndiyo wa chini zaidi kurekodiwa katika msimu mmoja tangu 2003/04.  Everton haijashinda mechi zake saba zilizopita za ugenini, lakini inapewa uwezekano wa asilimia 45.7 wa kushinda dhidi ya 28.4 za Hull City.


EP 09

LIVERPOOL VS MAN CITY

Manchester City itatembelea Anfield, kesho Jumapili, baada ya kupatikana na hatia ya kukiuka kanuni za kifedha za Ligi Kuu England kati ya 2009 na 2018.

City inapewa uwezekano wa asilimia 40.7 wa kushinda, Liverpool asilimia 34.6, ilhali sare ikiwa na uwezekano wa asilimia 24.7. Liverpool haijapoteza mechi tano za mwanzo, ingawa imetoka sare mara tatu.


EP 10

COVENTRY VS NEWCASTLE UNITED

Coventry City ya kocha Frank Lampard itacheza nyumbani, keshokutwa Jumatatu dhidi ya Newcastle United ambapo inapewa uwezekano wa asilimia 29.8 wa kushinda, huku Newcastle ikiwa na 44.8.

Kocha wa Newcastle United, Matthias Jaissle, amekusanya pointi nane katika mechi zake tano za mwanzo, idadi kubwa zaidi kwa kocha mpya wa klabu hiyo katika kipindi hicho tangu Alan Pardew alipokusanya tisa Januari 2011.