Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Diarra pokea ushauri huu

DIARRA Pict

Muktasari:

  • Sisi hapa kijiweni pasipo kujali utofauti wa itikadi zetu za kitimu kwa maana ya Uyanga na Usimba, wote tunaamini Diarra kuna kitu amekiongeza kwenye soka letu hapa Tanzania tangu alipojiunga na Yanga hadi sasa.

DJIGUI Diarra ni kipa ambaye kiwango chake bora anachoonyesha uwanjani kimemfanya ajijengee heshima kubwa katika soka la Tanzania.

Sisi hapa kijiweni pasipo kujali utofauti wa itikadi zetu za kitimu kwa maana ya Uyanga na Usimba, wote tunaamini Diarra kuna kitu amekiongeza kwenye soka letu hapa Tanzania tangu alipojiunga na Yanga hadi sasa.

Makipa wenzake hasa wazawa wanacho cha kujifunza na hata vijana wadogo wenye ndoto na matarajio ya kuwa makipa pia wanamuona Diarra kama roli modo wao na wanakua kwa kumtazama yeye.

Sasa kwa hadhi na daraja ambalo Djigui Diarra amejiwekea katika soka letu, yapo mambo hapaswi kuyafanya au kujihusisha nayo mojawapo ni la utovu wa nidhamu wa kuwafokea na kuwasumbua marefa hasa pale anapoona walichokiamua hakinufaishi timu yake.

Mfano ni kama alichokifanya hivi karibuni katika mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Mtibwa Sugar ambapo Yanga ililazimika kutumia nguvu ya ziada kumtuliza baada ya mchezo kisa alitaka kumshambulia mwamuzi wa mchezo.

Marudio ya vitendo kama hivyo yanaweza kuwa na madhara kwa Diarra mwenyewe na klabu yake kiujumla na ndio maana Yanga ililazimika kumpooza siku ile kwa sababu inafahamu athari yake baadaye.

Mchezaji anaweza kufungiwa michezo kadhaa na faini ya fedha jambo ambalo linaweza kuchangia kumshushia heshima na hadhi anayopewa na mailioni ya watu hapa nchini.

Lakini timu inaweza kuathirika kwa kukosa huduma yake muhimu kwa kosa ambalo lingeweza kuepukika na halikuwa na sababu wala ulazima wa kulifanya kwa mchezaji husika. Mfano bora ambao Diarra anauonyesha kwa kiwango bora uwanjani, unapaswa pia kuwa katika suala la nidhamu yake.