Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Cheikh Toure akaze sana pale Yanga

TOURE Pict

Muktasari:

  • Wameimbwa sana wakati wa usajili lakini sisi watu wa mpira hapa kijiweni tulikuwa tunasubiri ligi ianze ili tutoe maoni yetu.

WALE Ibrahima Cheikh Toure na Farouk Komara wanapaswa kukaza sana pale katika kikosi cha Yanga msimu huu.

Wameimbwa sana wakati wa usajili lakini sisi watu wa mpira hapa kijiweni tulikuwa tunasubiri ligi ianze ili tutoe maoni yetu.

Kwa wale watu wa mbele waliosajiliwa na Yanga mchezaji anayetakiwa kuonyesha kweli ni yule Cheikh Toure sijui ambaye katoka Saudi Arabia.

Mpira ni mchezo unaochezwa hadharani bwana. Yule jamaa japo huko alipotoka inaonekana amefunga sana magoli, lakini kwa hapa atapata tabu maana anapewa muda mfupi wa kucheza.

Na sisi hapa kijiweni tunamuelewa sana Kocha yule Mgqithi kwa wale watatu anaowapanga pale mbele, hakuna ambaye anaweza kuwekwa nje na Toure.

Yule Toure ilipaswa aonyeshe kiwango bora mara mbili zaidi ya kile cha Shalulile katika kila anapopata nafasi ili kumchongea kocha.

Halafu kuna yule beki Faruk Komara ambaye ambaye alipangwa ile mechi na Aigles Du Congo na kuchomesha bao mojawapo ambalo Yanga ilifungwa siku ile.

Sasa bora angekuwa mshambuliaji labda kocha angekuwa anamfikiria kumuingiza mara moja moja lakini kwa beki mbele ya Mwamnyeto, Bacca na Dick Job sijui kama atatoboa.

Inabidi wale wachezaji wafanye kazi hasa maana Yanga ina wachezaji wengi wazuri.