Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Baada ya miaka 25, ni zamu ya England?

ZAMU Pict

Muktasari:

  • Katika misimu mitatu iliyopita waliopita na tuzo hiyo ni Ousmane Dembele (Ufaransa 2025), Rodri (Hispania (2024) na Lione Messi (Argentina 2023), ambao wamo katika orodha ya nyota 30 waliovuka kikwazo cha awali.

PARIS, UFARANSA: TUZO za mchezaji bora Ulaya maarufu Ballon D'or kwa mwaka huu zinatarajiwa kutolewa mwishoni mwa mwezi ujao, Oktoba 26, ambapo mastaa wote walioibeba katika misimu mitatu ya karibuni wamo ndani wakiwania tena kuinyakua.

Katika misimu mitatu iliyopita waliopita na tuzo hiyo ni Ousmane Dembele (Ufaransa 2025), Rodri (Hispania (2024) na Lione Messi (Argentina 2023), ambao wamo katika orodha ya nyota 30 waliovuka kikwazo cha awali. Kinachoulizwa ni je England ambayo ina Jude Bellingham, Declan Rice na Harry Kane itafurukuta baada ya miaka 25 tangu alipobeba Michael Owen 2001?


ZAM 04

1. Harry Kane

Hata ukizingatia kiwango bora cha ufungaji mabao katika Bundesliga, mabao yake 61 katika mechi 51 alizoichezea Bayern msimu uliopita hayatoi picha kamili ya mchango wake kwa ujumla, ukizingatia uwezo wake wa kutengeneza nafasi na kumiliki mpira. Kane alizuiwa kimkakati katika mechi za baadaye za England kwenye Kombe la Dunia, lakini alikuwa hawezi kuzuilika hadi hatua ya 16 bora, akihitimisha mwaka bora zaidi wa maisha yake ya soka hadi sasa. Kama si sasa, basi ni lini?


ZAM 06

2. Rodri

Ana hoja inayofanana na ile iliyomsaidia kushinda tuzo hii 2024 kwani bado ndiye injini ya Hispania kwenye ufanisi. Safari hii, hata hivyo, hakuwa na mafanikio Ligi Kuu England kuimarisha nafasi yake, baada ya kampeni ya mwisho ya Manchester City katika Uwanja wa Etihad kukosa mvuto. Hata hivyo akiichezea Hispania ameshinda Kombe la Dunia.


ZAM 03

3. Kylian Mbappe

Mbappe na kocha wake Real Madrid, Jose Mourinho wameanzisha kampeni kubwa ya kutaka Mfaransa huyo kushinda Ballon d’Or yake ya kwanza. Alikuwa mgumu zaidi kuzuilika katika msimu wake wa pili nchini Hispania, akifunga mabao 40 katika mechi 42 za La Liga na Ligi ya Mabingwa. Kuhusu mchango wake katika kulazimisha mashambulizi ni bora usizungumze. Ni wachezaji wachache waliovutia na kutawala kama Mbappe kwenye Kombe la Dunia 2026 ambako alishinda Kiatu cha Dhahabu. Hata hivyo, ukosefu wa mafanikio ya timu unaweza kudhoofisha nafasi yake hasa ukizingatia mafanikio ya muda mrefu ya Real Madrid.


ZAM 01

4. Lamine Yamal

Mwingine kutoka katika kikosi cha mabingwa wa Kombe la Dunia, Hispania ingawa majeraha yalipunguza mchango wake ni huyu. Hata hivyo, alikuwa na bora zaidi katika msimu wake wa tatu akiwa mchezaji wa kawaida Barcelona, akihusika katika mabao 41 kwenye mashindano yote katika mechi 45.


ZAM 05

5. Lionel Messi

Messi huenda angekuwa juu zaidi iwapo Argentina ingeshinda Kombe la Dunia 2026 kwa sababu alikuwa moyo na roho ya kampeni yao. Hata hivyo, mchezo mbaya wa fainali zaidi kutokana na wachezaji wenzake, unapunguza nguvu ya matumaini yake ya kushinda Ballon d’Or ya tisa. Pia anaathiriwa na ukweli kwamba hachezi katika moja ya klabu kubwa za Ulaya, ingawa Inter Miami ilishinda ubingwa wa Ligi Kuu Marekani (MLS). Uwepo wake kwenye namba 17 kwenye orodha ya wanaowania Ballon d’Or bado unastahili.


ZAM 07

6. Michael Olise

Nani angejua kwamba safu ya ushambuliaji ya Bayern Munich yenye kusisimua zaidi katika miaka ya hivi karibuni ingeongozwa na wachezaji waliosajiliwa kutoka Tottenham Hotspur na Crystal Palace? Olise ni mshambuliaji wa kiwango cha juu ambaye amekuwa akifurahia zaidi kuwa mpangaji wa mashambulizi wakati wa mabadiliko ya mchezo na karibu na theluthi ya mwisho ya uwanja. Hispania ilifunga kwa ustadi njia zake za pasi katika Kombe la Dunia 2026 akiwa na Ufaransa na kumtoa katika mchezo wa nusu fainali, lakini pasi zake mbili za mwisho katika mchezo wa kuwania nafasi ya tatu zilimfanya awe kinara wa kipengele hicho kwenye fainali hizo. Je, huu ni mwaka bora zaidi wa maisha yake ya soka au ni ushahidi kwamba amejiwekea kiwango kipya?


ZAM 02

7. Erling Haaland

Hata wakati Man City ilipoyumba mwishoni mwa msimu uliopita, lakini ulikuwa mwingine wa kuongeza heshima yake inayozidi kukua kama mmoja wa washambuliaji bora wa kizazi chochote. Alitumia vizuri kurejea kwa Norway kwenye Kombe la Dunia 2026 akimaliza akiwa mfungaji bora wa tatu akifungana na wachezaji wengine akiwa na mabao saba, licha ya timu yake kutolewa katika robo fainali.


ZAM 08

8. Jude Bellingham

Uamuzi wa Birmingham City kustaafisha jezi yake wakati maisha yake ya soka yalikuwa ndiyo yanaanza umeonekana kuwa sahihi zaidi kadiri muda unavyokwenda. Ni mchezaji wa nyakati bora aliyeunda ushirikiano wa kipekee na Kane kwenye Kombe la Dunia 2026 wakibadilishana majukumu ya kuwa mashujaa kuelekea nusu fainali. Mabao na pasi zake za mwisho zilishuka katika msimu wake wa tatu uliopita Real Madrid ingawa wachezaji wengi walikuwa na kiwango cha chini.


ZAM 09

9. Ousmane Dembele

Akiwa hana makelele mengi yanayowazunguka wapinzani wake, Dembele bado ni tishio lenye ustadi kwa PSG na Ufaransa. Takwimu zake PSG zilishuka kutoka msimu uliopita wa kushinda tuzo kutokana na mabao 35 katika mechi 53 hadi 20 katika mechi 40. Ushirikiano wake na Mbappe na Olise kwa Ufaransa kwenye Kombe la Dunia 2026 ulikuwa miongoni mwa mashambulizi hatari zaidi ambayo soka la kimataifa limewahi kuyaona. Kama siyo kitu kingine, Dembele anaweza kuthibitisha kwamba hakushinda tuzo hiyo msimu mmoja tu kwa bahati, bali ni mashine bora.


ZAM 10

10. Khvicha Kvaratskhelia

Kwa kuangalia muda anaocheza PSG, ni wachezaji wachache wenye ufanisi zaidi katika michezo mikubwa. Kwa bahati mbaya, ubabe wa klabu yake kwenye mashindano ya ndani unamaanisha anaweza kupumzishwa zaidi kuliko wachezaji wenzake wengi wenye majina makubwa, akiwa amecheza dakika 1,479 tu za Ligue 1 katika mechi 28. Kutokuwepo kwa Georgia kwenye Kombe la Dunia 2026 pia kunapunguza ushahidi wa kuimarisha hoja ya kubeba tuzo. Hata hivyo, kiwango chake cha kuvutia katika hatua za mtoano za Ligi ya Mabingwa Ulaya kilimfanya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 kufikia ubora wa kipekee.


NA WENGINE WALIOPO KWENYE ORODHA…

Nyota wengine wanaoweza kufanya kweli ni Declan Rice (England/Arsenal), Bruno Fernandes (Ureno/Manchester United), Pau Cubarsí (Hispania/Barcelona), Fabian Ruiz (Hispania/PSG), Vitinha (Ureno/PSG), Luis Diaz (Colombia/Bayern Munich), Gabriel Magalhaes (Brazil/Arsenal) na  Nuno Mendes (Ureno/PSG).

Wengine ni Lautaro Martinez (Argentina/Inter Milan), William Saliba (Ufaransa/Arsenal), Achraf Hakimi (Morocco/PSG), Vinicius Junior (Brazil/Real Madrid), Dayot Upamecano (Ufaransa/Bayern Munich), Marc Cucurella (Hispania/Chelsea/Real Madrid), Joao Neves (Ureno/PSG), Willian Pacho (Ecuador/PSG), Ferran Torres (Hispania/Barcelona/PSG), Marquinhos (Brazil/PSG), Julian Quinones (Mexico/Al Qadsiah) na Sadio Mane  (Senegal/Al Nassr).