Prime
Azam vs Simba boli litapigwa kotekote
LIGI Kuu Bara ina timu 16 zinazozalisha mechi 480 kwa msimu. Ndani ya msimu huo, kuna mechi sita za hadhi ya juu zenye daraja A zinazozikutanisha Simba, Yanga na Azam; hapa ndipo ushindani wa kiufundi, ujanja wa mchezaji mmoja mmoja na ubora wa timu kwa ujumla huonekana wazi.
Mwishoni mwa wiki hii, macho yote yataelekezwa Chamazi Complex, ambapo Azam watakuwa wenyeji wa Simba katika moja ya mechi hizo kubwa. Ikumbukwe kwamba katika mchezo wa mzunguko wa kwanza uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa, Simba walipokea kichapo cha mabao 2-0 kutoka kwa Azam.
Matokeo hayo yanaweza kuwa rejea muhimu kuelekea pambano hili jipya, hasa tukitazama namna Azam walivyojijengea utambulisho wa kiuchezaji katika mechi kubwa msimu huu. Chini ya kocha wao, Florent Ibenge, Azam wamekuwa timu iliyokamilika kiufundi, wakiwa imara wanapokuwa na mpira na hata wanapoukosa.
Bila mpira, Azam hutumia mbinu mbili kwa nyakati tofauti au hata kwa wakati mmoja. Kwanza, huweka presha kali wanapokabiliana na timu zinazoanza mashambulizi kwa mipira ya kutenga. Lengo ni kuwalazimisha wapinzani kufanya makosa katika maeneo yao au kupiga mipira mirefu isiyo na malengo, mbinu waliyoitumia vizuri dhidi ya Yanga.
Pili, wanaruhusu mpinzani aanze mashambulizi bila presha ya moja kwa moja, lakini humvutia taratibu hadi kwenye mtego wao. Hapa ndipo wanapokuwa hatari zaidi, wakibadilika haraka kutoka kujilinda kwenda kushambulia. Kiungo Feisal Salum amekuwa mhimili mkubwa katika tafsiri ya haraka ya matukio haya akichangia kwa kiasi kikubwa mabao na pasi za mwisho.
Azam hutumia mfumo wa 4-2-3-1, ambao umekuwa hatari zaidi kupitia maeneo ya pembeni. Walinzi wao wa pembeni, Lusajo Mwaikenda na Paschal Msindo, wamekuwa na mchango mkubwa katika kuvunja ngome za wapinzani. Ushirikiano wao na mawinga unawapa uwezo wa kutoa upana au kuingia ndani kati ya mabeki wa mpinzani.
Katika ujenzi wa mashambulizi kutoka nyuma, mabeki kama Yoro Diaby hutumia pasi za chini kuvunja mistari ya ulinzi, huku Twalibu Nuru akitoa pasi ndefu za kubadili mwelekeo wa mashambulizi. Huu ndio msingi wa uimara wa Azam wanapokuwa na mpira.
Kwa upande wa Simba, mchezo uliopita uliwaonyesha udhaifu mkubwa wa kiulinzi, hasa waliposhambuliwa kwa kasi kipindi cha pili. Hata hivyo, mabadiliko ya kikosi na mbinu yaliyofanywa dirisha dogo yameongeza uimara na kujiamini kwa timu hiyo.
Ushirikiano wa viungo wakabaji, Yusuph Kagoma na Alassane Kante, umeimarisha uwezo wa timu kuzima mashambulizi ya kushtukiza. Simba pia hutumia mfumo wa 4-2-3-1, wakitegemea zaidi utatu wa Clatous Chama, Anicet Oura na Libase Gueye kama silaha kuu ya ushambuliaji.
Upande wa kushoto, unaohusisha Nickson Kibabage, Oura na Chama, umekuwa nguzo ya mashambulizi yao, huku upande wa kulia ukitumika kwa matukio machache lakini yenye maamuzi makubwa.
Mechi hii inaweza kuamuliwa na nani atatawala maeneo ya pembeni. Mapambano kati ya Lusajo dhidi ya Oura, pamoja na Libase dhidi ya Msindo, yanaweza kuwa na ushawishi mkubwa. Vilevile, Shomari Kapombe na Idd Seleman ‘Nado’ watakuwa na jukumu la kuhakikisha upande wao hauwi dhaifu.
Hili ndilo eneo ambalo linaweza kutoa mshindi; timu itakayoweza kulimiliki na kuwalazimisha wapinzani kucheza kwa kujihami zaidi itakuwa na nafasi kubwa ya kuibuka na ushindi.
Benchi la ufundi la Simba, chini ya kocha Steve Becker, linaamini katika kumiliki mpira kwa muda mrefu na kuutawala mchezo. Kwa upande mwingine, Ibenge anaamini zaidi katika mpito wa haraka kupokonya mpira na kushambulia kwa kasi.
Swali kubwa linabaki; je, Simba wataingia kwenye mtego wa Ibenge, au Azam watashindwa kujibu maswali ya ubunifu kutoka kwa Oura na Libase? Majibu yote yatapatikana baada ya dakika 90 za pambano kali pale Chamazi.
a yake na Mwanaspoti, Litagawe anasimulia safari yake katika mchezo huo ilivyomfungulia milango mingine ya kimaisha na kuwa chanzo kikuu cha kujipatia pesa za kujikimu.
Kocha huyo na pro anasema kama ilivyo ndoto ya vijana wengi kutamani kuwa na mali zao basi kupitia gofu baadhi ya vitu alivyovifanya ni kujenga na kufanya mambo mengine makubwa.
“Mchezo huo unachezwa na watu wa aina tofauti, haubagui umri wa mtu ndiyo maana nafundisha na kucheza pia, umenikutanisha na watu tofauti ambao ni sababu ya fursa mbalimbali ninazozifanya katika maisha,” anasema kocha huyo na kuongeza:
“Umenikutanisha na wafanyabiashara wa makampuni tofauti hivyo kuna biashara za jumla na rejareja ninazozifanya, yote hayo ni matunda ya gofu kuwa sehemu ya maisha yangu ya kila siku.”
Mbali na kucheza na kufundisha pia ni mtaalamu wa kutengeneza viwanja vya gofu kama anavyoelezea: “Mchezaji wa gofu lazima ajifunze mambo mengi sana, mojawapo ninachokifanya mimi ni mtaalamu wa kutengeneza viwanja vya kuchezea gofu,” anasema kocha huyo na kuongeza:
“Pia mimi ni mtaalamu wa kutengeneza bustani za kisasa katika majumba ya watu, mahoteli, kampuni na sehemu mbalimbali jambo linalonisaidia kupata pesa.”
Japokuwa amecheza kwa muda mrefu anakiri hajawahi kuchukua Tanzania One ila ametwaa mataji makubwa katika mashindano mbalimbali: “Nina mataji mengi ni ngumu kuyakumbuka yote pia nimepata zawadi nyingi sana.”
Anataja baadhi ya mataji aliyowahi kuyachukua kama Dan Open 1998 alishika nafasi ya kwanza, Morogoro Open 2002 nafasi ya tatu, Arusha Open 2005 nafasi ya tatu, Moshi Open 2006 nafasi ya pili, Tanga Open 2007 nafasi ya pili na Tanzania Open 2009 nafasi ya sita.
Anasema: “Kwa mashindano ya nje kama ya East Africa Challenge ya 2006 nilimaliza nafasi ya pili yalifanyika Burundi, Uganda Open 2001 nafasi ya tano, hayo ni baadhi ya mataji niliyoyachukua.”
VIJANA 180 WAMEPITA KWAKE
Anasema ameibua vipaji vingi zaidi ya vijana 180 wamepita mikononi mwake hasa katika mkoa wa Dar es Salaam.
“Nitumie fursa hii kuiomba serikali ianzishe programu za kudumu za mchezo wa gofu mashuleni kwa sababu unatengeneza ajira nyingi kwa vijana katika nyanja mbalimbali pengine tofauti na michezo mingine inayolimiti umri,” anasema kocha huyo.
“Jambo la kwanza tunaamini gofu ni koneksheni kwa sababu unakukutanisha na watu mbalimbali hivyo mtu akiwa na elimu yake ni rahisi kupata koneksheni ya kazi ndiyo maana nauona umuhimu wa kuwepo programu za kudumu kuanzia shuleni.
“Mbali na mchezo huo kutengeneza ajira pia unajenga afya kwani unaweza kutembea ndani ya uwanja kwa takribani masaa matatu unakutana na miti wakati mwingine wanyama, hiyo pia inasaidia afya ya akili, unaongeza upana wa kufikiri kwa sababu unatumia hesabu, unapanua mawazo ya kimaisha kwa kukutanisha na watu tofauti.”
Mbali na wachezaji unawapa ajira makedi kwa maana ya watu wanaobeba mabegi ya wachezaji, wapo wanaosafisha viwanja, kwa kifupi ni mchezo unaoweza kuwapa ajira mamia ya watu.
“Naamini wanahabari wakizidi kuuandika namna ulivyo na faida kubwa serikali itauona kwa jicho la kipekee kwa ajili ya kuandaa ajira za vijana kuliko wengi wanavyoona mpira wa miguu pekee ndiyo unaowabeba,” anasema kocha huyo ambaye nje ya gofu anacheza tenisi na kuogelea.
Akizungumzia ratiba yake kwa siku ili kufanikisha malengo ya kuhakikisha mchezo huo unabaki kuwa sehemu ya maisha yake, kocha huyo amesema haipiti siku bila kujishughulisha na gofu.
“Ratiba yangu kwa siku katika kazi ya gofu kabla ya kufanya mazoezi binafsi naanza kuwafundisha wanafunzi, baada ya hapo naanza kujifua kwa mazoezi ya kunipa ufiti. Hiyo imenisaidia zaidi kwa sababu muda wangu mwingi natumia katika mchezo huo na nimeziona faida nyingi sana katika maisha yangu,” anasema.
UPRO UNAPATIKANA HIVI
Anasema kuwa kuwa mchezaji wa kulipwa (pro) ni kazi na ni kipimo cha juu katika mchezo, lakini lazima awe mchezaji aliyefikia viwango vya kimataifa (handicap).
“Ili uitwe pro unapimwa kwa viwango vya kimataifa hadi upitie mchezo wa darasa kubwa, vigezo vya handicap ni 0-1-2-3 hii ina maana watu wasiodaiwa na uwanja kwa kupiga mipigo ya mpira inayotakiwa au kupiga chini yake pia awe mchezaji wa timu ya taifa ya Tanzania,” anasema kocha huyo ambaye ni shabiki wa Yanga na nje anaishabikia FC Barcelona.
Kwa Rodrick pia amekuwa akipambana ili kufika mbali zaidi kupitia gofu suala ambalo anaamini ipo siku mambo yatamwendea vizuri. “Pamoja na kutimiza malengo mbalimbali katika maisha yangu ila kubwa zaidi ni kufundisha klabu kubwa za gofu Tanzania mbali na watoto ninaowafundisha kwa sasa ambao wanafurahia mafunzo ninayowapa,” anasema.