Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yanga kwa Pedro, Moalin kuna kitu wanatuficha

NONDO Pict


KUNA wakati unawasikia watu wakiuzungumzia mpira wetu unajiuliza wanachokizungumza wanakijua kwa uhalisia au ni nadharia inayotokana na kusoma maandishi au kusikiliza maneno matamu ya wajuzi wa kuzungumza.


Wengine huenda mbali na kukubaliana na nadharia inayowaambia ligi yetu ni namba tano au sita barani Afrika bila kutazama vigezo vinavyotumika, hii haina tofauti ya mzazi aliyemkumbatia na kumpa zawadi mwanae kwa kuwa wa kwanza darasani kwake kwa wastani wa sitini huku mzazi mwingine akimfokea mwanae kwa kuwa wa kumi darasani kwake kwa kupata wastani wa themanini.


Kiuhalisia kuna vitu vingi vinaenda kwa nguvu ya dua, havina mtiririko sahihi.

Yanga wametoa taarifa kwa umma kuhusu tathmini yao ya mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Bara msimu huu 2025-2026 kutokana na mwenendo usioridhisha kulingana na daraja la ushindani walilolitengeneza kwa misimu minne iliyopita.

NOND 01

Sababu zimetajwa nyingi ikiwemo aina ya uchezaji kwa timu yao chini ya kocha aliyepo ikionekana kutokuendana na ile iliyozoeleka kutumiwa na timu yao.

Sasa utajiuliza kama timu ina aina yake ya uchezaji maana yake hata sajili zilizingatia mahitaji ya aina hiyo ya uchezaji, nani aliyemleta mwalimu asiyeendana na aina ya uchezaji wa Yanga.

Inawezekana hata wachezaji waliosajiliwa na kuachwa kutokana na kutofikia matarajio walikwamishwa na aina ya uchezaji inayotumika na timu kwa msimu huu.

Ambacho kinashangaza zaidi baada ya kugundua upungufu huo kwenye benchi la ufundi wameongeza kocha wakimtambulisha kama msaidizi ambaye jukumu lake litakuwa kubadilisha aina ya uchezaji ili kusaidia pia kuinua viwango vya baadhi ya wachezaji.

NOND 02

Unajiuliza kwenye kuchagua aina ya uchezaji nani mwenye jukumu, kocha mkuu au msaidizi? Jukumu la kocha msaidizi ni kushauri au kutoa muongozo?

Kama Abdihamid Moalin anakuja kutatua tatizo ambalo Pedro Goncalves alilishindwa kwa nini bado yuko kazini? Nini kimejificha, kwa nini asikabidhiwe timu Moalin na bechi lake kama yeye ndiye tiba ya changamoto za kimbinu timu inazopitia kiwanjani.

Kila mwalimu anaamini kwa namna yake kulingana na mafanikio aliyoyapata, anachokiweza kukisimamia na kukielezea kwa kukivunjavunja (details) mpaka mchezaji aelewe leo hii umbadilishe na kujaribu kumtoa kwenye anachokiamini, basi hakutakuwa na maelewano labda kama huko ndani walioko wanajua nani atakuwa na jukumu la kusimamia aina ya uchezaji huku mwingine akisubiri mwisho wa mwezi apokee mshahara.

NOND 03

Kuna mahali taarifa kwa umma imetuachia maswali mengi na kutuonyesha udhaifu wa kiutendaji ndani ya klabu.

Kama timu ina Mkurungenzi wa Ufundi inalalamika kocha haendani na aina yao ya uchezaji, je kazi yake nini? Utagundua vyeo vingi kwenye klabu zetu ni vya kwenye karatasi, kiuhalisia havitekelezi majukumu yao ndio maana nashauri wanaoujadili mpira wetu waujadili kwenye uhalisia na sio karatasi zinavyosomeka.

Kwa ujumla, soka letu linahitaji kuhamia kwenye uhalisia badala ya kuendeshwa na nadharia au hisia. Ni muhimu kuangalia mifumo ya uendeshaji, uwajibikaji wa viongozi, na namna uamuzi unavyofanyika ndani ya klabu.

NOND 04

Bila kufanya hivyo, tutaendelea kujidanganya kwa mafanikio ya muda mfupi huku tukipuuzia msingi imara wa maendeleo ya muda mrefu.

Wadau wa soka wanapaswa kuchambua mambo kwa kina, kwa kutumia vigezo sahihi na kuelewa muktadha mzima badala ya kuridhika na kauli zinazovutia lakini zisizo na uzito wa kiuhalisia.