Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Fumbo la bingwa aliyenuna kwenye runinga

PUMZI Pict


Kombe la Dunia linaendelea huko Amerika Kaskazini huku mabingwa mara nne, Italia, wakiangalia kwenye TV.


Kwa kushindwa kwao kufuzu mwaka huu, Italia wanakuwa nchi pekee iliyowahi kuwa bingwa, lakini wanakosekana kwenye mashindano hayo.


Nchi zingine zote ambazo zikiwahi kuwa mabingwa, zilifuzu na kushiriki mwaka huu.

Hii inakuwa safari ya tatu mfululizo kwa Italia kushindwa kufuzu Kombe la Dunia.


2018 - URUSI

Walishindwa kufuzu kupitia njia ya kawaida ya makundi kwa kuzidiwa na Hispania.

Wakaangukia nafasi ya pili iliyowafanya washiriki mechi za mchujo, nako wakashindwa kwa kutolewa na Sweden.


2022 - QATAR

Walishindwa tena kufuzu kupitia njia ya kawaida ya makundi kwa kuzidiwa na Uswisi kwenye kundi C.

Wakaangukia nafasi ya pili iliyowafanya wacheze mechi za mchujo...wakatolewa na vibonde Macedonia Kaskazini.


2026 - AMERIKA KASKAZINI

Walishindwa tena kufuzu kupitia njia ya kawaida kwa kuzidiwa na Norway kwenye kundi I.

Wakaangukia nafasi ya pili iliyowafanya wacheze mechi za mchujo...wakatolewa na Bosnia & Herzegovina.

Gattuso huyo ambaye ni mmoja wa wachezaji wa Italia walioshinda Kombe la Dunia 2006 nchini Ujerumani, akalalamikia mfumo mpya wa FIFA wa kufuzu Kombe la Dunia kwamba ndio kikwazo kwao.

Akasema wakati yeye anacheza, mshindi wa pili wa kundi alikuwa anafuzu moja kwa moja...lakini sasa ni lazima apitie mchujo.

Akaenda mbali hadi kulalamikia nafasi za Afrika, kwamba ndizo zimeiponza Italia.

Akasema zamani Afrika ilikuwa inatoa timu mbili (kabla ya 1994) na baadaye timu 3 (1994), lakini sasa inatoa timu 9.

Halafu wana nafasi moja ya mchujo dhidi ya mabara mengine...nafasi zinaweza kuwa kumi.

Alisema timu za Afrika hazina uwezo hivyo kuipa Afrika nafasi nyingi ni kuleta timu dhaifu badala ya kutoka nafasi nyingi kwa Ulaya ambako timu nyingi ni bora.


AFRIKA IMEMJIBU UWANJANI

Baada ya mechi za hatua ya makundi kumalizika, Afrika ndio bara lililoongoza kuvusha timu nyingi kwenda hatua ya mtoano, kwa uwiano wa idadi ya timu zilizoshiriki.


AFRIKA

Timu zilikuwa kumi. Timu tisa zimefuzu hatua ya 32 bora, sawa na asilimia 90.


AMERIKA KUSINI

Timu zilikuwa sita, zikafuzu tano kwa hatua ya 32 bora...sawa na asilimia  83.33


ULAYA

Timu zilikuwa 16, zikafuzu 13 kwa hatua ya 32 bora...sawa na asilimia 81.25


AMERIKA KASKAZINI, KATI, NA CARIBBEAN

Timu zilikuwa 6, zikafuzu 3 kwa hatua ya 32 bora...sawa na asilimia 50.


ASIA

Timu zilikuwa 9, zikafuzu 2 tu kwa hatua ya 32 bora...sawa na asilimia 22.22

Bila shaka huko aliko muda huu aidha anajutia kwa kauli yake au amenuna kwa hasira za kibaguzi na akili za kikoloni. Mawazo kama ya Gattuso yanaitwa Eurocentric...yaani kuona Ulaya inastahili zaidi kila kitu, na iko juu zaidi ya kila kitu.


Huo ndio ukoloni...ndio ubaguzi.

Gattuso ambaye wakati anacheza alikuwa mmoja wa viungo wagumu, amegeuka kuwa kocha laini zaidi kihisia kiasi cha kushindwa kudhibiti mdomo wake. Wakati yeye anabwabwaja mdomoni, Afrika imechagua kumjibu uwanjani.