Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mauaji ya kutisha – Sehemu ya 5

MAUAJI 5 Pict

UTANGULIZI

Ofisi ya polisi ni ya polisi tu. Unapoingia hata kama huna kosa ni lazima unywee.

“Jina lako tafadhali.” Amour alimuulliza akiwa ameshika  kalamu.

“Naitwa Shefa Ibrahim.”

Amour aliandika jina lake kabla  ya kumuuliza.

“Una umri  gani?”

“Mwezi ujao  nitatimiza miaka ishirini na tisa.”

SASA ENDELEA...


“Unaishi wapi?”

“Sinza.”

“Unafanya kazi gani?”

“Kazi?”

“Ndiyo.”

“Ndiyo niko kwenye mipango ya kazi.”

“Tuache huko, tuje katika hili tukio lililotokea kule Mikocheni, ulilishuhudia?”

“Ndiyo, nililishuhudia.”

“Uliniambia unaishi Sinza, ulifuata nini Mikocheni?”

“Huwa naenda kwa washikaji zangu kupiga stori.”

“Wakati hilo tukio linatokea, ulikuwa wapi?”

“Tulikuwa tumekaa masikani na washikaji wenzangu.”

“Masikani yenu ilipo na mahali lilipotokea tukio hilo kuna umbali gani?”

“Si  mbali sana.”

“Ni  kama  hatua ngapi?”

“Kama hatua hamsini hivi.”

“Sasa hebu eleza ulichoona.”

“Kusema kweli lile gari la yule jamaa huwa tunaliona mara kwa  mara likipita. Yule mshikaji ana kiwanda fulani cha maji, kipo pale pale Mikocheni…”

“Ndiyo.”

“Sasa lile gari lilikuwa linaelekea kwenye kile kiwanda cha maji safi.  Ghafla wakatokea watu watatu mbele  ya gari hilo.”

“Hao watu walitokea wapi?”

“Hatukuona walikotokea. Tuliwashitukia wakiwa wamesimama mbele ya gari hilo.”

“Hilo gari lilikuwa  linakwenda kwa mwendo gani?”

“Lilikuwa linakwenda  taratibu.”

“Baada ya hao watu kuonekana hapo mbele ya gari nini kilitokea?” Inspekta Amour akauliza.

“Lile gari lilisimama halafu yule jamaa aliyekuwa kwenye gari alifungua mlango. Wale watu watatu wakamvamia pale pale kwenye mlango. Tuliona wakisemeshana kisha yule mtu aliyevaa mavazi meusi alitoa kitu kama panga akamchinja yule jamaa.”

“Hebu subiri. Huyo aliyevaa mavazi meusi ndiye yule ambaye inadaiwa shingo yake ilikuwa imechinjwa?”

“Huwezi kuamini lakini ndivyo ilivyokuwa, karibu robo tatu ta shingo ya yule mtu ilikuwa imechinjwa, yaani pale kwenye koo palikuwa pamekatwa kabisa.”

“Sasa kama alikuwa amechinjwa kama  unavyosema, kichwa chake kilikuwaje?”

“Kilikuwa kinaning’inia kama vile kinataka kuanguka.”

“Ndiyo unasema mtu huyo ndiye aliyetoa panga na kumchinja marehemu?”

“Ndiye huyo huyo, yaani tulishangaa sana.”

“Sasa wakati anamchinja, wale watu wengine walikuwa wanafanya nini?”

“Walikuwa wakisaidia kumshika yule jamaa ili achinjwe.”

“Baada ya kumchinja ilikuwaje?”

“Yule mchinjaji akatia mkono kwenye gari na kutoa mkoba fulani akaufungua na kuutazama ndani. Nafikiri ule mkoba ulikuwa una pesa. Baada ya hapo wakatoweka na ule mkoba.”

“Walitoweka vipi?”

“Tuliona hawapo tena mahali pale. Hatukuweza kuona waliondoka vipi. Ilikuwa kama miujiza.”

Inspekta Amour baada ya kuyasikiliza maelezo hayo alinyamaza kimya akafikiri kisha akamuuliza kijana huyo.

“Una hakika kwamba maelezo yako ni sahihi?”

“Nina hakika.”

Kwa vile Amour alikuwa akiyaandika maelezo hayo alimwambia kijana huyo aweke sahihi yake.

Baada ya kijana huyo kuweka sahihi Amour alimwambia.

“Nipatie namba yako ya simu.”

Shefa alimpa namba yake ambayo Amour aliiandika.

“Unaweza kwenda. Mwambie mwenzako mmoja aingie.”

Shefa akainuka na kutoka. Punde tu akaingia kijana mwingine.

“Kaa kwenye kiti.” Amour alimwambia.

Kijana huyo hakupishana sana kiumri na yule aliyetoka.

“Jina lako nani?”

“Naitwa Rich.”

“Rich nani”

“Temba”

“Wewe ni mchaga.”

“Ndiyo.”

Amour alimsalimia kwa kutumia lugha ya kichaga na Rich akamjibu. Wakacheka.

“Wewe pia ni mchaga?”

“Hapana. Niliishi kule kwa miaka mingi.”

Amour alipachika karatasi mpya kwenye jalada, akaandika jina la Rich.

“Una umri gani?”

“Miaka ishirini na tisa.”

“Unaishi wapi?”

“Mikocheni.”

“Unafanya kazi gani?”

“Mimi nasoma chuo cha utumiishi.”

“Enhe hebu na wewe tueleze nini kilitokea hapo Mikocheni.”

Rich alitoa maelezo ambayo hayakutofautiana na maelezo aliyotoa kijana aliyetoka.

“Unadhani wale watu walikuwa kina nani?” Inspekta Amour alkamuuliza.

“Wale walikuwa majambazi.”

“Unazungumzia nini kuhusu yule mtu mnayesema kuwa shingo yake ilikuwa imechinjwa?”

“Sijui yule alikuwa mtu wa aina gani lakini ni kweli shingo yake ilikuwa imechinjwa.”

“Na ndiye unayesema kuwa amemchinja marehemu?”

“Ndiye huyo huyo.”

“Na baada ya kuchukua mkoba uliokuwa ndani ya gari waliondoka ghafla?”

“Ndiyo waliondoka ghafla.”

“Waliondokaje ghafla, hebu nieleze?”

“Yaani wale watu baada ya kufanya kile  kitendo walitupotea tu. Sijui ilikuwaje.”

“Unaamini kwamba walikuwa na miujiza?”

“Yaani ni kama walikuwa na miujiza Fulani.”

“Sawa. Sasa nipatie namba ya simu yako. Ninaweza kukuhitaji tena.”

Richa alitoa namba yake ya simu akampa Inspekta Amour.

“Sawa. Unaweza kwenda. Huyo mwenzako aliyebaki mlilishuhudia pamoja hili tukio?”

“Ndiyo, tulilishihudia pamoja.”

“Nadhani maelezo yake yatakuwa haya haya. Kwa hiyo ukitoka mnaweza kwenda, nisipoteze muda wake bure.”

                                        ************

Nyumbani kwa Almasi tayari kulikuwa kumeshajaa watu. Yeye na mwanawe Martin walikuwa wakikaa Masaki lakini katika mitaa tofauti. Baada ya tukio la  kuuawa Martin, Almasi aliuhamisha msiba nyumbani kwake.

Ndugu, jamaa, marafiki na majirani walikuwa wamekaa vikundi vikundi nje  ya nyumba ya Almasi ambako kuliwekwa viti pamoja  maturubai ya kukinga jua.

Hata hivyo watu wengi walikuwa wamesimama wakionekana kupatwa na sintofahamu kutokana na tukio la kuuawa Martin. Kila mtu ambaye alielezwa jinsi mauaji hayo yalivyotokea alikuwa akishangaa.

Kikubwa kilichowashangaza watu yalikuwa yale  maelezo kwamba mtu aliyemchinja Martin na yeye alikuwa amechinjwa!

“Mtu aliyekatwa koo angewezaje kuwa hai na kumchinja mwenzake?” Hilo ndilo swali ambalo kila mmoja alikuwa akijiuliza bila kupata jibu sahihi.

Ndani ya nyumba ya Almasi kulikuwa na sauti za vilio vya waombolezaji zilizokuwa zikisikika hadi nje.

Mke wa Martin na mama yake Martin ndio waliokuwa wakiongoza kwa kulia. Baadhi ya ndugu na marafiki walikuwa wakiwabembeleza na kuwataka wawe na subira.

Almasi mwenyewe alikuwa amekaa katika moja ya sebule za nyumba yake huku baadhi ya wanawe wengine pamoja na marafiki wakishughulika kukaribisha wageni waliokuwa wakiwasili.

Baadaye msemaji wa familia ya Almasi alitoa tangazo akaeleza kwamba maziko ya marehemu Martin yatafanyika kesho yake hapo hapo Masaki.

Alieleza kwamba mwili wa marehemu utaagwa kuanzia saa tatu asubuhi hadi saa sita na utazikwa saa tisa alasiri.

Kama ilivyokuwa imepangwa, saa tatu asubuhi ya siku iliyofuata mwili wa Martin ulitolewa nje kwa ajili ya kuagwa. Zoezi hilo liliendelea hadi saa sita mchana.

Mpaka inafika saa nane, mwili wa Martin ulikuwa umeshafikishwa makaburini kwa ajili ya kuzikwa. Kila aliyehudhuria maziko ya Martin alikiri kuwa yalikuwa maziko yaliyosikitisha watu wengi.

Si tu kwa vile Martin mwenyewe alikuwa bado kijana na ndiyo kwanza alikuwa amepata mtoto wake wa kiume bali mauaji yaliyomtokea yalikuwa yakikatili sana.

Inspekta Amour ambaye pia alihudhuria maziko ya Martin aliwasha gari lake na kuondoka katika  eneo hilo mara tu Martin alipozikwa.

Alikwenda tena Mikocheni kuangalia mandhari ya mahali alipouawa Martin. Lengo lake lilikuwa ni kutengeneza picha ya mawazo ya jinsi Martin alivyouawa.

Alipofika katika eneo hilo aligundua kulikuwa na kioski cha vinywaji baridi upande wa pili wa barabara  karibu kabisa na mahali ambapo tukio la mauaji hayo lilitokea.

Alisimamisha gari mbele ya kioski hicho akashuka na kwenda kwenye kidirisha cha kioski hicho. Muuzaji alikuwa kijana mmoja aliyekuwa akizungumza kwenye simu lakini alipomuona Amour alikata simu na kumsikiliza.

“Kijana habari ya kazi?” Amour akamuuliza.

“Nzuri. Nikusaidie nini?”

“Nipatie kokakola baridi”

“Unataka  ya kuchukua au ya kunywa hapa hapa?”

“Nataka ya kunywa hapa hapa.”

Kijana akamtolea Inspekta Amour soda ya kokakola kutoka kwenye friji.

Baada ya kuifungua chupa alimpa Inspekta Amour. Amour aliichukua na kugugumia funda moja la kokakola baridi kisha akamtazama kijana huyo.

“Juzi palitokea patashika kubwa katika  eneo lako,” akamwambia.

“Oh! Juzi mzee kulikuwa na hekaheka. Majambazi waliua mtu hapa!” Kijana akadakia.

“Lakini walikuwa majambazi kweli au…?”

“Walikuwa majambazi.”

“Wewe uliwaona?”

“Niliwaona na niliona kila kitu kilichotokea. Wakati huo mimi nilikuwa hapa hapa kwenye kioski change.”

“Mbona kuna watu wanasema sijui eti mmoja  wa hao watu shingo yake ilikuwa imechinjwa?”

“Sasa pale ndio sikuelewa wale watu walikuja  na miujiza gani. Kweli shingo ya mmojawao ilikuwa imechinjwa na huyo jamaa ndiye aliyetoa  panga na kumchinja Yule mhasibu wa kiwanda cha maji safi.”