Mauaji ya kutisha - Sehemu ya 32
Muktasari:
- “Potelea mbali. Kama ni kumzika maremehu nitamzika mwenywe. Nendeni” Almasi akajisemea peke yake. Na yeye akaingia kwenye gari lake na kuondoka.
UTANGULIZI
Almasi alipowambia hivyo shemeji zake hao waliingia kwenye gari walilokwenda nalo na kuondoka bila kuaga.
“Potelea mbali. Kama ni kumzika maremehu nitamzika mwenywe. Nendeni” Almasi akajisemea peke yake. Na yeye akaingia kwenye gari lake na kuondoka.
Alipofika kituo cha polisi akalikuta gari la shemeji zake likiwa nje ya kituo.
Alipoingia ndani ya kituo hicho akakutana na watu hao wakizungumza na Inspekta Amour.
Walipomuona akiingia walikatisha mazungumzo. Amour akamwambia Almasi.
“Nimepokea mashitaka yako”
“Mashitaka gani?”
“Kwamba watoto wako pamoja na mke wako wameuawa kwa sababu za kishirikina”
“Sasa ushirikina upi nilioufanya?’
“Ni ushirikina ambao uliufanya kwenye madini miaka iliyopita. Shemeji zako wanadai kuwa hukutimiza mashrti ya waganga na hivyo kusababisha watoto wako pamoja na mke wakokuuawa na majini”
Almasi akatikisa kichwa.
“Si kweli. Mimi nawaomba polisi muendelee na upelelezi wenu. Habari hizi za kishirikina muachane nazo”
“Ni kweli kwamba hatuchunguzi kadhia zenye mtazamo huo na wala madai hayo hayawezikutufanya tukufungulie kesi lakini mazingira ya yale mauaji yanatisha. Kwa mfano wale watu waliomuua mke wako uliwafungia ndani lakini tulipovunja mlango hawakuwemo ndani!”
Maria alliposikia hivyo akachachamaa.
“Sasa ulikataa nini wakati hata polisi wammeona jinsi hao watu walivyotoweka. Bado utasema si ushirikina wako uliomuuua dada yangu?’
Kaka zake nao wakaingilia.
Ikawa mzozo ndani ya kituo cha polisi, ikabidi Inspekta Amour aingilie kati kuwasuluhisha nakuwaweka sawa mpaka wakakubalina kwamba washirkiane kumzika marehemu na baada ya hapo waweke kikao kuzungumzia tatizo lililotokea lakini wazingatie ripoti ya uchunguzi itakayotolewa na polisi.
Baada ya muafaka huo, shemeji zake Almasi waliondoka na kumuacha Almasi akiandikisha maelezo yake. Baada ya hapo akaondoka. Aliporudi nyumbani kwake aliwapigia simu jamaa zake na rafiki zake na kuwajjulisha kuhusu msiba wa mke wake.
Ya Lengo lake lilikuwa kupata watu wa kulala naye pale nyumbani. Alikuwa ameingia uoga wa kulala pake yake. Alihisi kama vile wauaji hao watamfuata usiku na kummaliza na yeye kama alivyoambiwa na mganga kwamba ilibaki roho yake kutoka.
Saa chache baadaye, jamaa na marafiki aliowapigia simu wakaanza kufika nyumbani kwake na kumfariji.
Alipata watu ambao alilala nao hadi asubuhi lakini shemeji zake hawakufika.
SASA MALIZIA
SHEMEJI zake hao walifika asubuhi wakiwa kama wageni. Mwili wa marehemu ulichukuliwa hospitali saa nane mchana. Wakati huo Almasi alikuwa ameshaletewa shilingi milioni kadhaa zikiwa katika sarafu.
Aliziagiza mapema asubuhi kutoka benki na kutoka katika kiwanda chake cha maji safi.
Kwa sababu alikuwa hajui hesabu kamili ya utajiri aliokuwa nao, alikadiria tu kiasi cha pesa cha kwenda kukitosa baharini ili kuokoa maisha yake.
Pesa hizo aliziweka kwenye viroba vitatu vilivyofungwa sawaswa na kuonekana kama viroba vilivyotiwa unga wa sembe. Hata alipoingia navyo nyumbani kwake na kuvihifadhi chumbani kwake hakukuwa na aliyejua kama ni pesa.
Almasi alitaka mwili wa mke wake uzikwe siku ile ile lakini aliona atawashitua watu. Akapanga mazishi yafanyike siku iliyofuata.
Siku ile alikuwa sambamba na marafiki zake wakati wote. Aliogopa kuwa pake yake akihisi kuwa wale wauaji wanaweza kutokea na kumuua.
Hata usku alilala na kundi la watu lakini hakukuwa na aliyejua kuwa mwenzao anajihami asiuawe.
Asubuhi ya siku ile alliyopanga mazishi, shughuli zilianza tangu mapema asubuhi. Marehemu akaenda kuzikwa saa sita mchana.
Saa nane Almasi aliwatoroka rafikizake akaenda kukodi boti akiwa na wafanyakazi wake wawili. Alikuwa amewabebesha vile viroba vya pesa. Boti iliwapeleka mbali kidogo. Alipoona mahali hapo panatosha akawamuru wafanyakazi hao kuanza kuvitupa baharini viroba hivyo.
Kila kiroba kimoja kilipotoswa, Almasi alitikisa kichwa kusikitikia pesa zake.
Zoezi la kumwaga pesa hizo lilipomalizika boti ikarudi ufukweni. Almasi na wafanyakazi wake walitoka kwenye boti wakajipakia kwenye gari na kuondoka.
Sasa kidogo mmoyo wake ulikuwa umetulia lakini taharuki la kuuliwa wanawe na mke wake bado lilikuwa llikimfukuta moyoni.
Pamoja na uchungu wa kutupa pesa zake uchungu wa kuulliwa mke wke ulimuuma zaidi.
Alijiambia hata kama yeye atapona haitakuwa rahisi tena kupata mke kama yule na huenda asiweze tena kupata mke. Shemeji zake wamekuwa wakimuenezea sifa ya ushirikina na uuaji. Katika jiji kama lile la Dar es Salaa, habari zikishaenea kwa watu kila mtu atakunyooshea kidole. Akajiuliza ni mwanamke gani atakayetaka kuolewa na mtu ambaye amedaiwa kutoa kafara wanawe na mke wake ili kupata utajiri?
Akatikisa kichwa chake.
“Si rahisi kkupata mke tena” akajiambia.
Aliuongeza kujiambia hata kama atabahatika kupata mke lakini hatakuwa kama yule ambaye tabia zao zlikuwa zimezoeana na alikuwa akimpenda na kumuamini.
Alifikiria arudi kwa yule mmganmga akamueleze kwamba ameshatoa kafara lile la pesa allilokuwa ameliacha lakini alliona asiende tena kwa mganga huyo ambaye alihisi angeweza kumpa maelezo ya kumtia wasiwasi.
Aliwarudisha wale wafanyakazi wake kisha akarudi nyumbani kwake.
Asubuhi ya siku iliyofuata aliamka asubuhi ili aende ofisini kwake. Wakati anatoka akakutana na shemeji zake waliowasili kwa gari.
Baada ya kusalimiana nao mmojawao alimwambia.
“Tumekuja kwa ajili ya kuweka kile kikao”
“Kikao asubuhi hii jamani, kwani hatuna kazi za kufanya. Mimi naenda kazini. Sina muda wa kufanya kikao muda huu” akawambia.
“Sasa tukufuate saa ngapi?”
“Nina kazi nyingi za kufanya naomba mnipe muda kidogo”
“Tuambie ni lini utakuwa tayari ili tuje tulizungumze lile suala”
Almasi akatikisa kichwa.
“Siwezi kusema kwa sababu hata huo umuhimu wa kikao siuoni tena. Nyie mnaweza kwenda tu”
Almasi alijipakia kwenye gari lake na kuondoka akawaacha shemeji zake hao wakimshangaa.
Ukweli ni kuwa hakukitaka kikao hicho ambacho alihisi kingemuumbua. Vile ambavyo mke wake ameshamzika hakuhitaji tena kuwa na uhusiano na shemeji zake hao.
Alikwenda zake ofisini kwake akafanya kazi hadi saa kumi jioni aliporudi nyumbani. Wakati amekaa sebuleni akiwaza akaona watu watatu wakiingia humo ndani.
Akashituka.
Walikuwa ni wale wauaji waliomuulia wanawe na mke wake.
Alitaka ainuke kwenye sofa awakimbie lakini hakuwa na nguvu za kuinua hata mguu achilia mbali kuinuka na kukimbia. Akajua sasa wakati wake ulikuwa umefika.
“Je mnataka nniini jamani?” akawauliza walipofikamahali allipokaa.
“Tumekuja kkutekeleza sharti letu” Mmoja wa watu hao akamwambia Almasi.
“Sharti gani”
“Uliwaweka dhamana wanao na mkeo kwa ajili ya kupata mali zetu lakini ulishindwa kutimiza masharti yetu. Wanao na mke wako tumeshawachukua. Sasa bado wewe mwenyewe!”
“Nimemwaga pesa jana tu kama nilivyoambiwa!”
“Umechelewa na hesabu yako haikubaliki”
“Naweza kwenda kumwaga pesa zingine”
“Huwezikufaidi utajiri wetu bilakkutimiza masharti tunayoyataka na kwa utaratibu ule ule tuliyokupa!”
“Lakini…lakini…”
“Wewe kubali tu kkuwa unaondoaka!”
Sime ilikwishatolewa. Ikapita kwenye shinho yake kama umeme…
Siku iliyofuata shemeji zake Almasi waliokuwa nna kisasi wakafika tena nyumbani kwa Almasi. Wakiwa sebuleni ndipo walipouona mwili wa Almasi umelala ukiwa umechinjwa. Damu iliyokuwa imeganda ilisambaa kkila mahali.
Nzi walikuwa wameungangania mwili huo hasa kwenye shingo iliyokuwa imechinjwa.
Shemeji zake Almasi walishituka na kushangaa. Kuona Almasi naye ameuawa. Wakatazama kwa mshangao.
“Kaka zangu mmeona wenyewe! Yule aliyetoa roho za wenzake na yake imetolewa!” Maria aliwambia kaka zake hao.
“Tena huyu hakuuawa leo itakuwa ni jana,” mmoja wa kaka zake hao akasema.
“Inaonekana ameuawa jana,” kaka mwingine akaongeza.
“Alidhani yeye angeishi milele, mauti kama yale ya wenzake yamemtookea,” kaka wa kwanza akasema.
“Wale majini wa huu utajiri wake wamemchinja na yeye. Mganga aliwambia kuwa na wewe utakufa. Amekufa kweli jamanni huu utajiri haufai….”
“Sasa twendeni tukatoe ripoti polisi…”