Zuchu na siri ya nyimbo za mapenzi
Muktasari:
- Zuchu, ambaye yupo chini ya lebo ya WCB Wasafi, wiki iliyopita alitoa wimbo unaoitwa “Bado Nakupenda” ambao mashairi yake yamejaa maneno ya mapenzi. na amekuwa akisifiwa kwa sauti nzuri, uandishi wa nyimbo na uwezo wa kuwasilisha hisia kupitia muziki.
Msanii wa kike wa Bongofleva, Zuchu, ameendelea kuthibitisha nafasi yake katika muziki wa Tanzania kupitia nyimbo zake za mapenzi zinazopendwa na mashabiki wa rika zote.
Zuchu, ambaye yupo chini ya lebo ya WCB Wasafi, wiki iliyopita alitoa wimbo unaoitwa “Bado Nakupenda” ambao mashairi yake yamejaa maneno ya mapenzi. na amekuwa akisifiwa kwa sauti nzuri, uandishi wa nyimbo na uwezo wa kuwasilisha hisia kupitia muziki.
Msanii huyo aliwahi kuzungumza na Mwanaspoti kuhusu mafanikio yake, akisema: “Napenda kuimba kutoka moyoni, ndiyo maana mashabiki wangu wanajiona ndani ya nyimbo zangu, na ninapotoa nyimbo za mapenzi huwa zinafanya vizuri sana.”
Msanii huyo aliongeza kuwa anajifunza kila siku kutoka kwa wasanii wakubwa pamoja na mashabiki wake wanaompa mrejesho wa mara kwa mara.
Mbali na muziki, Zuchu pia amekuwa mfano wa mafanikio kwa wasanii wa kike, akiwahamasisha kujiamini na kusimamia vipaji vyao. Kwa kasi yake ya sasa, ameendelea kujijengea heshima kubwa ndani na nje ya nchi.