Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wema Sepetu aweka masharti ya kumuonyesha Baby Olie

Muktasari:

  • Wema ameeleza hayo kupitia Instagram Story yake, baada ya kusema amekuwa akipokea maswali mara kwa mara kutoka kwa mashabiki wanaotaka kujua mtoto huyo yukoje na lini atamuonyesha.

Msanii wa filamu nchini, Wema Sepetu, ameweka wazi msimamo wake kuhusu kumtambulisha hadharani mtoto wake anayemuita Baby Olie, akisema mashabiki watapata nafasi ya kumuona atakapoona muda mwafaka umefika.

Wema ameeleza hayo kupitia Instagram Story yake, baada ya kusema amekuwa akipokea maswali mara kwa mara kutoka kwa mashabiki wanaotaka kujua mtoto huyo yukoje na lini atamuonyesha.

Akijibu maswali hayo, Wema amesisitiza kuwa hataki kushinikizwa kuhusu suala hilo, akieleza kuwa uamuzi wa kumtambulisha mtoto wake ni wake na atauchukua pale atakapojisikia kufanya hivyo.

“Guys, tusipangiane. I will show Baby Olie pale nitakapoona kwamba huu ndio muda sahihi wa kumuonyesha. Don't worry,” amesema Wema.

Ameongeza kuwa mtoto huyo yupo salama na mashabiki hawana sababu ya kuwa na wasiwasi, kwani watapata nafasi ya kumuona wakati utakapofika. Hata hivyo, amewaomba wampe nafasi badala ya kuendelea kumshinikiza.

“Baby Olie yupo, mtamuona muda utakapofika. Naombeni tu msinichinikize. Nitamuonyesha pale nitakapojisikia kufanya hivyo,” amesema.

Wema si msanii wa kwanza kuchukua muda kabla ya kuwaonyesha mashabiki sura za watoto wake. Mwanamuziki Nandy aliwahi kuficha sura ya binti yake, Kenaya, kwa mwaka mmoja kabla ya kumuonyesha kwa mara ya kwanza Agosti 2023, alipokuwa akisherehekea siku yake ya kwanza ya kuzaliwa.

Naye mwanamuziki Vanessa Mdee na mumewe, Rotimi, waliamua kutoweka hadharani sura ya mtoto wao, wakieleza kuwa wanataka kumpa nafasi ya kukua bila kuingizwa mapema katika maisha ya umaarufu.

Vilevile, mwaka 2015, mwanamuziki Diamond Platnumz na Zari Hassan walisubiri siku 40 kabla ya kumtambulisha hadharani binti yao, Princess Tiffah, jambo lililokuwa likisubiriwa kwa hamu na mashabiki wao.

Wema amesisitiza kuwa kwa sasa anataka kufurahia muda wake na mtoto huyo bila kuingiliwa na matarajio ya watu, akieleza kuwa suala la kumuonyesha halipaswi kuwa jambo la kulazimishwa.

“Let me be with my kid, let me just enjoy my kid,” ameongeza.

Kauli hiyo inaweka wazi msimamo wa Wema kuhusu faragha ya mtoto wake, akisisitiza kuwa licha ya shauku ya mashabiki kutaka kumuona Baby Olie, yeye ndiye mwenye uamuzi wa lini na kwa namna gani atamtambulisha hadharani.