Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wema, Lulu Diva  sasa wafikia pabaya

UGOMVI Pict

Muktasari:

  • Wakizungumza kwa nyakati tofauti wasanii hawa wamesema ni bora urafiki wao usirudi tena kwani wamechoka kuishi kiunafki, hawa hapa wanafunguka:

UGOMVI unaoendelea wa wasanii wa Bongo Movies, Wema Sepetu na Lulu Diva sasa umefika pabaya kila mmoja akitema nyongo kivyake.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wasanii hawa wamesema ni bora urafiki wao usirudi tena kwani wamechoka kuishi kiunafki, hawa hapa wanafunguka:

UGO 04

Wema Sepetu

"Nimechoka kuficha ficha ukweli kwamba mimi na Diva tumegombana, unajua unafiki mimi siuwezi na mficha maradhi humuumbua, haiwezekani kitu kinikere halafu nionyeshe niko sawa, ukweli siko sawa na Diva na naona saa hizi imefika mwisho, maana kuishi na rafiki ambaye yuko karibu sana na adui yako unafiki huo siuwezi, mimi na Whozu tumegombana, halafu Diva ndio amezidi kuwa karibu naye, sikatai kama wasiongee ila kuna baadhi ya vitu inatakiwa awe naye mbali, lakini yeye ndio amekuwa karibu kupitiliza tofauti na mwanzo.

"Sasa hiyo ni nini kama sio unafki? Si ni bora nikae mbali na huyo mtu, maana sioni urafiki wetu kama ni mwema, ila nashukuru nimejifunza kitu na sitarudia tena kuwa kama hiki kilichotokea," amesema Wema Sepetu.

UGO 03

Lulu Diva:

"Aisee, mimi nimechoka na urafiki huu na siuwezi tena, yaani mtu akigombana na mtu basi na mimi nigombane naye huyo mtu kisa urafiki, hapana kwa kweli, nimechoka kugombana na watu bila sababu, au kununiana na watu bila sababu, hii imefika mwisho ni bora kila mmoja afanye mambo yake tu," amesema Lulu.

Hata hivyo, Lulu kwenye akaunti yake ya Instagram, juzi ameandika ujumbe kuhusu ugomvi wake huu na Wema, baada ya madai kwamba Lulu Diva anamzunguka Wema na kuanza uhusiano na Whozu, ambaye alikuwa mpenzi wa Wema. Aliandika:

"Whozu ni mwanamuziki kama mimi na zaidi ya yote ni rafiki niliyefahamiana naye siku nyingi kabla ya yeye (Whozu) kuwa katika uhusiano na "rafiki yangu" (Wema Sepetu). Kwa bahati nzuri rafiki zangu hao wawili walianza uhusiano, nikafurahi sana, bahati mbaya katika kutofautiana kwao (ni kawaida kwenye uhusiano) kila mmoja ni kama alitaka niwe upande wake na mimi SIKUFANYA HIVYO, wote ni rafiki zangu.

UGO 01

Kilichotokea mara ya mwisho, mimi nilikuwa katika kupishana na rafiki yangu (Wema Sepetu) na katika wakati huo nadhani hakuwa sawa sana na mpenzi wake Whozu. Nafikiri rafiki huyu alitarajia mimi na Whozu hatutakuwa katika maelewano kwa sababu zao.

"Kwa ufupi, mimi na Whozu hatukuwahi kuwa na uhusiano au jambo lolote la kimapenzi. Urafiki huu haukuja baada ya uhusiano wake, hivyo hauwezi kufa kwasababu zinazohusiana na hilo la uhusiano wao, labda kama Whozu angekuwa amefanya jambo baya kama kumpiga mtu au lingine la kiunyanyasaji

"Mimi na aliyekuwa "rafiki yangu" (Wema) tulipishana kwasababu ya mambo mengine kabisa ambayo sioni haja ya kuyaelezea mtandaoni, hata hili nimelazimika kwasababu naona jina langu linashambuliwa, hili la Whozu naona kama ni kunitafutia ubaya tu mbele ya jamii kama inavyosemwa kwamba ukitaka kumuua mbwa unampa jina baya.

"Mwisho...urafiki unaweza kufa, lakini usiwe mwanzo wa uadui kila mtu aendelee na maisha yake bila sisi kutafutana ubaya," aliandika Lulu Diva.

UGO 02

Tujikumbushe

Wema na Diva, hii sio mara ya kwanza kugombana, na wamekuwa marafiki wa muda mrefu sana, na urafiki wao wamekuwa wakigombana walikuwa ni wa siri kukubali kwa watu kuwa wamegomba na baadaye kuumaliza ugomvi wao kimya kimya.

Na mara nyingi ugomvi wao huo, ulihusishwa na madai ya usaliti kuwa Diva anamzunguka Wema na kutoka kimapenzi na Whozu.

Licha ya Wema na Diva urafiki wao mara kadhaa huingia kwenye ugomvi kama ilivyo kawaida kwa marafiki wengine wa kike, ila kwa sasa hivi imekuwa tofauti kidogo baada ya Diva kuamua kuandika ujumbe huo hadharani na Wema ukimuuliza anaweka wazi kuwa wamegombana ila chanzo hasa wanakijua wao wenyewe.

Hata hivyo, waliowahi kuwa marafiki wa Wema kabla ya Diva, wakiwamo mastaa wenzie urafiki wao uliposambaratika wengi wao walidai kwamba Wema akitofautiana na mtu anataka na wewe umnunie huyo mtu hata kama huna ugomvi naye, kitu ambacho hawakukubaliana nacho.