Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Watakaoshiriki tamasha la pasaka waanza kutajwa, yupo Tumaini Akilimali wa Kenya

Dar es Salaam. Maandalizi ya tamasha la Pasaka yamepamba moto na waimbaji watakaoshiriki wameanza kutajwa wakiwemo wa ndani na nje ya nchi.

Majina ya waimbaji hao yameanikwa  leo Ijumaa Februari 24, 2024 na  Mkurugenzi wa kampuni ya Msama Promotion ambayo ndio waandaaji wa tamasha hilo, Alex Msama alìpozungumza na waandishi wa habari.

Amewataja waimbaji hao ambao tayari wamethibitisha ushiriki wao  kuwa  ni  pamoja na Tumaini Akilimali wa Kenya, Joshua Ngoma wa Rwanda na Masi Masilia wa nchini Congo ambaye huyu ni mara yake ya kwanza kutua Tanzania.

Kwa upande wa waimbaji wa Tanzania yupo Upendo Nkone, Ambwene Masongwe, Joshua Mlelwa na Zabron Singers.

Akielezea kuhusu maandalizi tamasha hilo, Msama  amesema yanaendelea na kuahidi kuwa litakuwa tamasha la kimataifa na kubainisha kuwa wamekuja kivingine baada ya kutofanyika kwake kwa miaka saba.
"Leo tunatambulisha wasanii watakaoshiriki tamasha hilo litakalofanyika Aprili 9 mwaka huu katika uwanja wa uhuru Dar es Salaam.
"Niwaambie tu tamasha litakuwa na waimbaji wengi wa kimataifa ambao hawajawahi kukanyaga hapa Tanzania na waimbaji manguli wa hapa nchini hivyo sio la kukosa," amesma Mkurugenzi huyo .

Hata hivyo amesema bado wapo  kwenye mazungumzo na waimbaji wengine  kutoka nchini Afrika Kusini, Uingereza na Marekani.
"Tunaposema tumerudi tena tunaamaanisha, jiandaeni na tamasha zuri, tamasha la kihistoria,"
Katika taasha hilo Msama amesema pia watazungumzia miaka miwili ya Rais  Samia Suluhu Hassan tangu aingie madarakani ambaye kila wakati amewataka Watanzania kumuombea lakini pia watalitumia kuiombea nchi kuepukana na majanga ya asili  ikiwemo kimbunga matetemeko ya ardhi na mafuriko.

Kwa upande wake mjumbe wa kamati  maandalizi ya tamasha hilo, Emmanuel Mwabisa amesema waimbaji siku hiyo wataimba live na tayari wameshaanza kutuma 'technical reader' zao na kueleza kuwa wanashukuru wamepata kampuni yenye utaalam wa kufunga vyombo vya live