Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Utofauti wa Billnass na Nandy, Diamond na Zuchu!

Muktasari:

  • Mbali na muziki, uhusiano wake na mkewe Nandy, ni kati ya mambo yanayofanya jina la Billnass kuzungumzwa kila mara lakini hiyo haijaja bure tu bali kuna kazi kubwa wamefanya. Fahamu zaidi.

HAKUNA ubishi kuwa rapa Billnass ni miongoni mwa wasanii wa rapa ambao wamekuwa na mwendelezo mzuri wa kufanya vizuri katika muziki hasa wa rap katika kipindi cha miaka 10 iliyopita.

Mbali na muziki, uhusiano wake na mkewe Nandy, ni kati ya mambo yanayofanya jina la Billnass kuzungumzwa kila mara lakini hiyo haijaja bure tu bali kuna kazi kubwa wamefanya. Fahamu zaidi.

1. Ingawa Billnass ndiye alitangulia kutoka kimuziki kabla ya mkewe Nandy, hadi sasa rapa huyo hajatoa albamu wala EP, huku Nandy akiwa ameachia albamu moja na EP tatu ambazo zote zilitoka wakiwa tayari wapo katika uhusiano.


2. Billnass ni miongoni mwa watu waliomsaidia Nandy kufanikisha zoezi la kushuti video ya wimbo wake, Leo Leo (2021) akimshirikisha ngwiji wa muziki Afrika kutokea DR Congo, Koffi Olomide.


3. Hadi sasa Billnass ameshinda mara Tuzo za Muziki Tanzania (TMA), huku Nandy akiwa ameshinda mara nne, na wote walianza kushiriki kuanzia msimu wa 2021 baada ya tuzo hizo kurejea tangu ziliposimama mwaka 2015.


4. Ni Jux na G Nako pekee ambao wote wameshirikishwa katika nyimbo za Billnass na Nandy ambao ni mastaa wanandoa wanaofanya vizuri katika Bongofleva kwa sasa.


5. Jux amesikika katika wimbo wa Billnass, Maboss (2024) huku G Nako katika ngoma, Kinamba Namba (2024). Kwa upande wa Nandy, Jux ameshiriki katika wimbo, Sweety (2025), na G Nako, Dah Remix (2024).

6. Hadi sasa Billnass na Nandy ni kati ya mastaa wanandoa ambao wameshirikiana katika nyimbo nyingi zaidi ambazo zinafikia sita. Nyimbo hizo ni Bugana (2019), Do Me (2020), Party (2021), Bye (2022), Totorimi (2024), na Hallo (2026).


7. Mbali na Billnass na Nandy, mastaa wengine wanandoa waliopiga kolabo nyingi ni Diamond Platnumz na Zuchu ambao wameshirikiana katika nyimbo sita pia. Nyimbo hizo ni Litawachoma (2020), Cheche (2020) na Mtasubiri (2022), Raha (2024), Wale Wale (2024) na Inama (2025).


8. Video 10 za Billnass ambazo zinaongozwa kwa kutazamwa YouTube, ni zile ambazo amewashirikisha wanamuziki wenzake kama Jay Melody, Jux, Nandy, Mbosso, Marioo na Mwana FA. Na ni wimbo mmoja tu wa Billnass ambao hajamshirikisha msanii yeyote ambao video yake imeshatazamwa zaidi ya mara milioni 1 YouTube, nao ni Tatizo (2021).


9. Hanipher Daudi maarufu kama Jenipher Kanumba, ndiye staa mkubwa wa kwanza katika filamu Bongo kuonekana katika video ya wimbo wa Billnass (Tatizo), kabla ya hapo rapa huyo alikuwa akiwatumia warembo wengine ila si waigizaji.


10. Billnass ametokea katika video ya Nandy, Napona (2022) bila ya kuwa ameshirikishwa katika wimbo huo, kitu ambacho si kigeni kwa wanamuziki ambao wana uhusiano. Diamond alikuja kufanya kitu kama hicho katika video ya wimbo wa mkewe, Zuchu, Utaniua (2023). Vilevile Vanessa Mdee alifanya hivyo kwa Jux (Sisikii), na Shilole alifanya hivyo kwa Nuh Mziwanda (Msondo Ngoma).