Miaka miwili ya ndoa... Bilinas ajivunia mtoto
Muktasari:
- Akizungumza na Mwanaspoti, Billnass amesema katika miaka hiyo miwili kuna vingi vya kujivunia ila kikubwa ni kumshukuru Mungu kwa kupata mtoto wa kike mzuri na anayempenda.
Mapenzi ya kweli hayasemwi ila yanajieleza yenyewe na hujionesha ukweli hasa kwa wapendanao kweli kweli. Leo ni miaka miwili imetimia tangu msanii William Lyimo 'Billnass' na nyota wa muziki wa Bongo Fleva, Faustina Mfinanga 'Nandy' walipofunga ndoa Julai 16, 2022 katika kanisa la KKKT Mbezi Beach, Dar es Salaam.
Akizungumza na Mwanaspoti, Billnass amesema katika miaka hiyo miwili kuna vingi vya kujivunia ila kikubwa ni kumshukuru Mungu kwa kupata mtoto wa kike mzuri na anayempenda.
Tunashukuru Mungu kwa kila jema alilotujaalia hadi muda huu, pumzi ya uhai ndiyo kitu kikubwa kuliko vyote, na leo nina furaha kubwa na kujivunia kutimiza miaka miwili kwenye ndoa na mke wangu Faustina Mfinanga 'Nandy', kubwa zaidi ya mafanikio ni kujivunia pia kupata mtoto wa kike ninayempenda sana.
"Ni safari ndefu isiyokuwa na kikomo, hii kumbukumbu ya ndoa yetu mke wangu upendo na uvumilivu alionionyesha kwa kipindi hiki chote sina cha kusema zaidi ya shukrani, Mungu atubariki sisi na familia yetu. Nampenda zaidi na nitaendelea kumpenda na kumjali hadi mwisho wa maisha yangu duniani kwani najijua mimi ni zaidi ya pasua kichwa ila milima na mabonde, vizingiti na mito, maziwa bahari kwa uwezo wake Mungu tu tutavuka," alisema.
Kwa upande wa Nandy, aliandika kwenye mtandao wa kijamii; "Mume wangu, miaka miwili ya ndoa yetu imekuwa fundisho kubwa kwangu kujua upendo ni kitu muhimu sana, uwepo wako umerahisisha maisha yangu na ya kipenzi chako NAYA, jua tu tunakupenda sana. Ninachokuomba, najua wanaume mmeumbiwa kupepesa macho japo sio mwanamume wangu wewe 😝😂 (joke) popote uendapo, chochote ufanyacho jua una watu wanakupenda na kukuhitaji sana, kuyashinda majaribu now days ni rahisi sababu kila kitu kishapitwa na wakati na wakati wenyewe ndo sasa kuonyesha mfano na kuwa mifano bora kwa watu wenye mapenzi ya kweli, kuwa vijana wakiamua inawezekana. Mungu wangu atulinde nitimize ahadi ya watoto wako 10 NAKUPENDA PY @billnass
HAPPY ANNIVERSARY MY LOVE ❤️."
Mwanaspoti linawapa hongera wanandoa hawa na kuwaombea mema zaidi kwenye uhusiano wao.