Prime
Kisa mtoto, usaliti, ndoa ya Hamisa, Aziz Ki gumzo
MJADALA mpya kwa sasa mitandaoni ni kuhusu ndoa ya Hamisa Mobetto na Stephane Aziz Ki na wengi wanajadili kuhusu tuhuma za usaliti na ishu ya mtoto ingawa hakuna ushahidi uliotolewa kuhusu madai hayo.
Baadhi ya watumiaji wa mitandao wanadai kutopata mtoto hadi sasa huenda kukachangia mjadala huo, huku wengine wakirejea madai ya mara kwa mara kuhusu usaliti.
Mashabiki wamegawanyika, wengine wakisema kila siku huibuka mada mpya kuhusu wawili hao, huku wakisisitiza kuwa ukweli wa maisha yao unafahamika na wahusika pekee.
"Watu wanabadilisha tu mada kila siku, leo mtoto, kesho usaliti. Mwisho wa siku ukweli wanaujua wao wenyewe," ameandika mmoja wa watumiaji wa mitandao ya kijamii.
Hadi sasa Hamisa Mobetto na Stephane Aziz Ki hawajatoa kauli yoyote kuhusu madai hayo, jambo linaloendelea kuongeza mijadala na tafsiri tofauti kutoka kwa mashabiki.
Licha ya gumzo hilo, Hamisa ameendelea na shughuli zake za biashara na burudani, huku Aziz Ki akiendelea na majukumu yake ya soka.
Wawili hao walifunga ndoa Februari 16, 2025 katika hafla iliyovuta hisia za wengi na kuendelea kuwa gumzo hadi sasa. Tangu wakati huo, kila taarifa inayowahusu imekuwa ikifuatiliwa kwa karibu na mashabiki.
Kwa sasa hakuna taarifa rasmi zinazothibitisha madai yanayosambaa, hivyo mjadala unaendelea kutawaliwa na maoni na uvumi wa mitandaoni huku wengi wakisubiri iwapo wahusika wataamua kuzungumzia suala hilo.