Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rushayna apeperusha bendera ya Tanzania Ufaransa

RUSHAYNA pict

Muktasari:

  • Ni safari mpya ya Rushayna katika tasnia ya filamu, ambaye sasa anapata nafasi ya kuonesha kazi yake mbele ya watazamaji na wadau wa filamu kutoka mataifa mbalimbali kupitia tamasha hilo linalojikita katika kutangaza ubunifu wa watengenezaji wa filamu wa Afrika na Caribbean.

MUIGIZAJI na mtayarishaji wa filamu nchini Tanzania Rushayna Salum, amepata nafasi ya kuiwakilisha filamu ya Tanzania katika jukwaa la kimataifa baada ya kazi yake ya Romantic Rose kuchaguliwa kushiriki Tamasha la LAfrique Fait Son Cinema 'AFSC', linalofanyika nchini Ufaransa.

Ni safari mpya ya Rushayna katika tasnia ya filamu, ambaye sasa anapata nafasi ya kuonesha kazi yake mbele ya watazamaji na wadau wa filamu kutoka mataifa mbalimbali kupitia tamasha hilo linalojikita katika kutangaza ubunifu wa watengenezaji wa filamu wa Afrika na Caribbean.

Kwa mujibu wa ratiba ya maonesho, Filamu hiyo ilipangiwa kuoneshwa Jumatatu, Novemba 9, 2026, usiku, katika Ukumbi wa Ecole Internationale de Creation Audiovisuelle et de Réalisation (EICAR), uliopo Ivry-sur-Seine, nchini Ufaransa.


RUSH 01

FILAMU 56 ZAINGIA KINYANG'ANYIRO

Katika toleo la nane la tamasha la AFSC, lililopangwa kufanyika Novemba 5-14, 2026, kamati ya maandalizi ilitangaza filamu 56 kutoka nchi 24 zilizochaguliwa kati ya kazi zaidi ya 300 zilizowasilishwa.

Katika kundi la filamu ndefu za kubuni, Romantic Rose imeingia pamoja na kazi nyingine 12 kutoka mataifa mbalimbali, ikiwemo Zimbabwe, Gabon, Cameroon, Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Ushiriki huo unaipa filamu ya Rushayna nafasi ya kuonekana katika jukwaa linalokutanisha watengenezaji wa filamu wenye mitazamo na uzoefu tofauti.


RUSH 02

UBUNTU AWARDS ZASUBIRIWA

Mbali na maonesho ya filamu, tamasha hilo lina tuzo zinazojulikana kama Ubuntu Awards, zinazolenga kutambua ubora wa kazi na mchango wa wadau mbalimbali katika tasnia ya filamu.

Miongoni mwa tuzo hizo ni Ubuntu de Diamant ya filamu bora ndefu ya kubuni, filamu fupi bora, makala bora, mwigizaji bora wa kiume na wa kike, mtayarishaji bora wa filamu ndefu, mwandishi bora wa script na tuzo ya watazamaji.

Kwa kuwa Romantic Rose imechaguliwa katika kundi la filamu ndefu za kubuni, inakuwa sehemu ya kinyang'anyiro cha tuzo ya Ubuntu de Diamant katika kundi hilo.


RUSH 03

TANZANIA INASUBIRI HATUA INAYOFUATA

Safari ya Romantic Rose haijaishia kupata nafasi ya kuoneshwa Ufaransa, kwani kupitia ujumbe wake ameweka wazi kuwa baada ya hatua hiyo wanatarajia kurejea nyumbani Tanzania na kuendelea na safari ya kuifikisha filamu hiyo kwa watazamaji wa ndani.

Sasa kinachosubiriwa ni mapokezi ya kazi hiyo nchini Ufaransa, matokeo ya ushiriki wake katika tuzo za Ubuntu Awards na mipango ya Rushayna ya kuifikisha katika masoko mengine ya kimataifa.