Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Q Chief yuko hivi kwa Diamond, Ali Kiba

Q CHIEF Pict

Muktasari:

  • Q Chief amesemsa amefikia kiwango ambacho haoni msanii mwingine nchini anayeweza kumzidi katika eneo hilo, akiwataja mastaa wakubwa akiwamo Diamond Platnumz na Ali Kiba.

HAKUNA wa kumfunika! Ndivyo anavyojiamini msanii mkongwe wa Bongo Fleva, Abubakary Katwira ‘Q Chief’, anapozungumzia uwezo wake wa kuimba moja kwa moja (live).


Q Chief amesemsa amefikia kiwango ambacho haoni msanii mwingine nchini anayeweza kumzidi katika eneo hilo, akiwataja mastaa wakubwa akiwamo Diamond Platnumz na Ali Kiba.

Akizungumza na Mwanaspoti maeneo ya Sinza kwa Remmy, Q Chief amesemsa kumtaja msanii mmoja mmoja kama anayeweza kumshinda kwenye uimbaji wa moja kwa moja ni sawa na kumshusha thamani yake.

“Sasa hivi nilipofikia, ndugu  yangu, mpango wa kunitajia msanii mmoja mmoja kwamba nitamfunika ni kunishusha daraja na thamani yangu. Chukua Diamond, Ali Kiba, Marioo, Jay Melody, wakiweza kunifunika, nitaamini kweli Tanzania kuna wasanii,” amesemsa.

Q Chief amesemsa kujiamini huko kunatokana na kipaji alichojaliwa na Mungu, akisisitiza uwezo wa kuimba live si jambo analolazimisha bali ni sehemu ya kipaji chake.

Hata hivyo, anaamini ukimwweka jukwaani na mastaa hao, bado ana uwezo wa kusimama mwenyewe na kuonyesha kile anachokiamini kuwa ni ubora wake mkubwa.

Kwa hiyo, Diamond, Ali Kiba, Marioo na Jay Melody wanaweza kuwa na majina makubwa, lakini kwa Q Chief, kwenye eneo la kuimba live, bado hajapata anayemfikia.