Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Pande mbili za maisha ya Lil Wayne!

LIL W Pict

Muktasari:

  • Picha linaanza mwaka 1997, ambapo Lil Wayne anaanza rasmi muziki baada ya rapa wa kundi la Hip Hop la Big Tymers, Birdman kumsanini Cash Money Records na kuwa msanii mdongo zaidi katika lebo hiyo kwa wakati huo.

MUZIKI ni upande wa kwanza wa wanamuziki wa Hip Hop kutokea Marekani, Lil Wayne, 44, na familia na mahusiano ni upande mwingine wa rapa huyo ambaye mtindo wake wa maisha tangu akiwa kijana mambo ni mchaka mchaka!

Picha linaanza mwaka 1997, ambapo Lil Wayne anaanza rasmi muziki baada ya rapa wa kundi la Hip Hop la Big Tymers, Birdman kumsanini Cash Money Records na kuwa msanii mdongo zaidi katika lebo hiyo kwa wakati huo.

Chini ya Cash Money jina la Lil Wayne lilitambulika duniani na kupewa heshima na mashabiki wengi, alipata umaarufu zaidi baada ya kuachia albamu yake ya nne, Tha Carter (2004).

Takribani miaka minane baadaye, akaja na albamu yake ya sita, Tha Carter III (2008) ambayo ilipokelewa vizuri ikiuza nakala zaidi ya milioni 1 ndani ya wiki moja katika sokoni la Marekani pekee.

LIL 01

Nyimbo zake maarufu kama A Milli, Got Money na Lollipop, zilitoka katika albamu hiyo na wimbo wa Lollipop ulishinda tuzo ya Grammy kama Wimbo Bora ya Rap, huku pia ukiwa ni wimbo wake wa kwanza kushika nafasi ya kwanza katika chati ya Billboard Hot 100.

Baada ya miaka mingi ya mafanikio katika muziki, Lil Wayne alikuja kuanzisha Young Money Entertainment (YMCMB), iliyokuwa chini ya Cash Money kuanzia mwaka 2005 hadi 2018.

Young Money ndio iliwatoa Drake, Tyga na Nicki Minaj, rapa aliyefunika na ngoma yake, Anaconda (2014) iliyoweka rekodi ikiwa video ya kwanza ya msanii wa kike wa Hip Hop kutazamwa mara bilioni 1 YouTube.

Katika mahojiano na Billboard mnamo Agosti 2023, Lil Wayne amesema ni faraja kuona ameshawishi vijana wengi duniani kuingia katika muziki na hata wale ambao wanaonekana kuiga mtindo wake wa muziki sio kitu kinachomchukiza.

LIL 02

Lil Wayne aliwataja Lil Uzi Vert, Travis Scott, Trippie Redd na Young Thug kama wasanii ambao kwa kiasi kikubwa aliwashawishi kufanya muziki na ndio sababu wanafanana naye.

“Wakati fulani watu huniuliza jinsi ninavyohisi kuhusu kila mtu anayefanana na mimi kimuziki, kila mtu huchora tattoo kama mimi n.k,  hiyo ni kama kuona mtoto wako akitoka nje ya nyumba yako na kuonekana kafanana na wewe, unahisi vizuri. 

“Kwa hivyo ushawishi unaonekana dhahiri kwa sababu najua kwa kweli mimi sikupata sura hii kutoka kwa mtu yeyote, hakukuwa na mtu ambaye alinishawishi kuwa hivi, nilikimbilia tu kuonekana kama nilivyo.” amesema Lil Wayne.

Akiwa akiwa anaendelea kusimamia wasanii wa Young Money Entertainment kama Mkurugenzi Mtendaji, Lil Wayne amesema bado hajaona cha kumuondoa katika muziki.

LIL 03

“Ninajaribu tu kuwa bora zaidi, nafanya kazi na kuendelea kusonga mbele, kamwe sitaacha, nafanya kwa maadili, mipango na urahisi, hakuna zaidi ya hapo, sifanyi chochote zaidi ya muziki wangu,” Lil Wayne  aliiambia Billboard.

Hadi sasa Lil Wayne ameuza rekodi zaidi ya milioni 200 duniani kote zikiwemo nakala za albamu milioni 95, ameshinda tuzo tano za Grammy, tuzo 11 za BET, tuzo nne za Billboard, tuzo mbili za MTV VMA na kadhalika.

Muda mfupi baada ya kujiunga na Cash Money Records, Lil Wayne na mpenzi wake wa wakati huo, Toya Johnson, walijaliwa kupata mtoto wao wa kwanza, Reginae Carter ambaye alizaliwa Novemba 29, 1998.

Kipindi hicho Lil Wayne akiwa na miaka 16, na alikuwa bado ni mwanafunzi wa sekondari. Alikuja kufunga ndoa na Toya mwaka 2004 ingawa waliachana kwa talaka mwaka 2006, na hadi sasa hii ndio ndoa pekee aliyowahi kufunga rapa huyo katika maisha yake.

Reginae ambaye sasa ana umri wa miaka 29, tayari amehitimu Chuo Kikuu cha Clark Atlanta na anafuata nyayo za wazazi wake kama mwigizaji, mwanamuziki na mwandishi. Amecheza filamu kama Dear Santa, I Need a Date and Pride and Prejudice: Atlanta na kadhalika.

LIL 02 (1)

Vilevile ameshiriki vipindi vya televisheni kama Growing Up Hip Hop Atlanta na T.I. na Tiny: Friends and Family Hustle ambacho mama yake pia anaigiza, ameandika kitabu kimoja, Paparazzi Princesses, huku akiwa sehemu ya kundi la muziki, OMG Girlz.

Kwa ujumla, Lil Wayne ni baba wa watoto wanne kutoka kwa wanawake wanne tofauti, ambao wote ameachana nao, huku watoto wake wawili wakizaliwa ndani ya mwaka mmoja, 2009.

Watoto wake ni Reginae Carter (1998) aliyezaa na mwigizaji Toya Johnson, Dwayne Carter III (2008) aliyezaa na mtangazaji Sarah Vivan, Kameron Carter (2009) aliyezaa na mtangazaji Lauren London, na Neal Carter (2009) aliyezaa na mwanamuziki Nivea.

Mnano Septemba, Lil Wayne aliripotiwa kumchumbia kwa siri binti mwenye umri wa miaka 20 kutokea jimbo la Indiana nchini Marekani. Kwa mujibu wa TMZ, rapa huyo alimchumbia kimya kimya mrembo huyo mapema mwaka huu, na tayari mipango ya kufunga ndoa inaelezwa imeshaanza.