Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mwili wa Sekidia kuagwa Jumatatu, kuzikwa Jumatano Tanga

KIFO Pict

Muktasari:

  • Mwili wa mwanamuziki huyo utaagwa kwanza jijini Dar es Salaam kabla ya kusafirishwa kwenda Mkuzi, Muheza, Tanga kwa ajili ya mazishi.

MWANAMUZIKI mkongwe wa dansi nchini, Andrew Sekidia, aliyefariki dunia Novemba 27, 2026, anatarajiwa kuzikwa Jumatano, Desemba 2, 2026, mkoani Tanga.

Mwili wa mwanamuziki huyo utaagwa kwanza jijini Dar es Salaam kabla ya kusafirishwa kwenda Mkuzi, Muheza, Tanga kwa ajili ya mazishi.

Akizungumza na Mwanaspoti nyumbani kwa mama wa marehemu, Kimara Baruti, ambako msiba upo, dada wa marehemu, aliyefahamika kwa jina la Betty, amesema familia imepanga ratiba ya kuuaga mwili huo ikiwashirikisha wakazi wa Dar es Salaam na ndugu wa mkoani Tanga.

Amesema Jumatatu, Novemba 30, 2026 mwili wa Sekidia utaagwa katika Uwanja wa Shule ya Msingi Ubungo, nyuma ya Ubungo Plaza, kuanzia saa sita mchana.

Uamuzi wa kuagwa eneo hilo umetokana na ombi la wakazi wa Ubungo, ambako marehemu alizaliwa na kukulia, wakitaka kupata nafasi ya kumuaga kwa mara ya mwisho.

Baada ya shughuli hiyo, mwili utapelekwa nyumbani kwao Kimara Baruti ambako utalala kabla ya safari ya kwenda Tanga.

Betty amesema Jumanne, Desemba 1, 2026 baadaya chakula, mwili utaondolewa nyumbani na kupelekwa Kanisa la Anglikana Ubungo Msewe kwa ajili ya ibada, kabla ya safari ya kuelekea Mkuzi, Muheza, Tanga.

“Jumatatu atakuwa anaagwa Ubungo kuanzia saa sita mchana, kwa sababu amezaliwa na kukulia Ubungo, watu wa huko wameomba aagwe eneo hilo ili wengi wapate nafasi ya kumuaga. Baada ya hapo mwili utakwenda nyumbani Kimara Baruti, Jumanne baada ya chakula tutaondoka kwenda Kanisa la Anglikana Ubungo Msewe kwa ibada, kisha safari ya Tanga,” amesema Betty.

Kifo cha Sekidia kimeacha simanzi kwa ndugu, jamaa, mashabiki na wadau wa muziki wa dansi, kutokana na mchango wake katika muziki huo nchini.