Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

MR Midabhangulo: Changamoto za familia zamfungulia milango ya burudani

Muktasari:

  • Kwa mujibu wa simulizi ya maisha yake, alikulia katika familia iliyokabiliwa na changamoto za kiuchumi, hali iliyomfanya aanze kutafuta fursa za kujenga maisha yake kupitia kipaji cha kuchekesha.

MCHEKESHAJI Mr Midabhangulo ameieleza safari yake ya kuingia katika sanaa ya ucheshi ilichangiwa kwa sehemu kubwa na changamoto za kiuchumi na kifamilia alizopitia.

Kwa mujibu wa simulizi ya maisha yake, alikulia katika familia iliyokabiliwa na changamoto za kiuchumi, hali iliyomfanya aanze kutafuta fursa za kujenga maisha yake kupitia kipaji cha kuchekesha.

Changamoto za kifamilia pia zilichangia uamuzi wake wa kujitengenezea utambulisho wa kisanii kwa kutumia jina la Mr Midabhangulo badala ya kutegemea jina la baba yake.

Katika kuendeleza ndoto zake, alihama kutoka Mwanza kwenda Dar es Salaam, ambako aliendelea kutafuta nafasi katika tasnia ya burudani huku akitumia mitandao ya kijamii kusambaza kazi zake na kujenga hadhira.

Akizungumzia nafasi ya majukwaa ya kidijitali katika kukuza vipaji, alisema: “Leo unaweza kutengeneza kitu, kukichapisha na kuwafikia maelfu au hata mamilioni ya watu. Mitandao ya kijamii imetoa nafasi kwa wabunifu kuonyesha vipaji vyao na kujenga hadhira zao wenyewe.”

Mr Midabhangulo amesema anatarajia kuendelea kuboresha maudhui yake na kujenga chapa imara katika tasnia ya burudani, huku akiwashauri vijana wanaotaka kuingia katika sanaa kuwa wavumilivu, wabunifu na wenye kujituma.

Mafanikio yake katika safari hiyo yameanza kuonekana baada ya kununua gari lake la kwanza kupitia kazi ya uchekeshaji na utengenezaji wa maudhui ya kidijitali.

Hatua hiyo ni sehemu ya mafanikio yake katika kutumia kipaji na ubunifu kujipatia kipato, ikionyesha namna mitandao ya kijamii inavyoweza kufungua fursa za kiuchumi kwa wasanii wanaojituma katika tasnia ya burudani.