Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Miss Tanzania kufanyika Desemba 19

Muktasari:

  • Mratibu wa Miss Tanzania, Lamata Mwendamseke amesema kuwa warembo wanatoka kanda saba za Tanzania na maandalizi ya kambi hiyo yamekamilika.

JUMLA ya warembo 24 wataingia kambini kesho Ijumaa kujiandaa kuwania taji la Miss Tanzania 2026, shindano ambalo limepangwa kufanyika Desemba 19, 2026 jijini Dar es Salaam.

Mratibu wa Miss Tanzania, Lamata Mwendamseke amesema kuwa warembo wanatoka kanda saba za Tanzania na maandalizi ya kambi hiyo yamekamilika.

Lamata amesema kuwa wakiwa kambini, warembo hao watafundishwa mambo mbalimbali  kwani moja ya malengo yake makubwa ni kuona warembo hao wanafanikiwa hata baada ya mashindano kumalizika.

 “Miss Tanzania ni zaidi ya shindano la urembo. Ni jukwaa linalokuza kujiamini, uongozi, uwajibikaji wa kijamii na uzalendo kwa wanawake vijana,” alisema Lamata. Alisema kuwa shughuli zote za warembo hao zitaonyeshwa kwenye king’amuzi cha DStv ambao ni washirika wao wakuu. Alifafanua kuwawatakuwa na vipindi vitatu kwa siku ya Ijumaa, Jumamosi na Jumapili kupitia chaneli ya Maisha Magic Bongo.

“Nimejiandaa kuleta mapinduzi wa sanaa ya urembo nchini kwa vitendo, hivyo Watanzania watashuhudia msisimko, maandalizi, changamoto, urafiki, vipindi vya malezi, pamoja na matukio ya kusisimua yanayoifanya safari ya Miss Tanzania kuwa ya kipekee,” alisema Lamata.

Kwa upande wake Mkuu wa Maisha Magic Bongo, Evelyn Byaruhanga, alisema watazamaji wanatarajia kupata uzoefu wa kipekee unaovuka mfumo wa kawaida wa mashindano ya urembo.

“Lengo letu ni kuwapeleka watazamaji zaidi ya yale wanayoyaona jukwaani. Kupitia matangazo yetu, watazamaji watashuhudia msisimko, maandalizi, changamoto, urafiki, vipindi vya malezi, pamoja na matukio ya kusisimua yanayoifanya safari ya Miss Tanzania kuwa ya kipekee.  Tumeandaa mashindano haya katika mfumo wa kipindi cha televisheni chenye mvuto mkubwa ambacho kinasherehekea washiriki na simulizi zao huku kikionesha utofauti, utamaduni na uzuri wa Tanzania.”

Katika kipindi chote cha wiki tano za matangazo, watazamaji watafurahia vipindi vilivyotayarishwa kwa ubora wa hali ya juu vikifuatilia kila hatua ya mashindano, ikiwemo usaili na uteuzi wa washiriki wa kanda, kambi za mafunzo, vikao vya ushauri na malezi, shughuli za kijamii, maandalizi nyuma ya pazia, kuondolewa kwa washiriki na simulizi mbalimbali za kutia moyo.

Mfululizo huu utatoa mwonekano wa kipekee wa kile kinachohitajika kushindania moja ya mataji yenye heshima kubwa nchini Tanzania. Wakati huohuo, Afisa Mtendaji Mkuu wa MultiChoice Tanzania, Sophie Tchatchoua wanajisikia fahari kubwa kuwa sehemu ya kuendeleza Sanaa ya urembo Tanzania.

 “Kupitia kampeni yetu ya Tumewasikiliza, tuliahidi kuwasikiliza wateja wetu na kuwapatia maudhui wanayoyapenda zaidi. Watanzania wameendelea kutuambia kuwa wanahitaji maudhui zaidi ya ndani, simulizi halisi za Kitanzania na fursa nyingi zaidi za kusherehekea vipaji vya nyumbani. Kuileta Miss Tanzania kwenye DStv ni mwitikio wa moja kwa moja wa maoni hayo.”