Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Khadija Kopa ataja jina la mtoto wa Diamond, Zuchu

Muktasari:

  • Khadija, ambaye ni mama mzazi wa Zuchu, amesema amefurahishwa na jina hilo, hasa kwa sababu mtoto huyo amepewa jina la mama mzazi wa Diamond Platnumz.

MALKIA wa muziki wa taarabu, Khadija Kopa, ametaja jina la mtoto wa Diamond Platnumz na Zuchu kuwa ni Sandra, wakati akizungumza katika hafla ya 40 ya mtoto huyo inayofanyika leo Septemba 12, 2026 kwenye Ukumbi wa Saint Laurent Garden, Kawe, Dar es Salaam.

Khadija, ambaye ni mama mzazi wa Zuchu, amesema amefurahishwa na jina hilo, hasa kwa sababu mtoto huyo amepewa jina la mama mzazi wa Diamond Platnumz.

Akizungumza katika hafla hiyo, Khadija amesema: “Mtoto anaitwa Sandra. Mimi nimejisikia furaha sana mtoto kupewa jina la mama yake mzazi baba yake, Diamond Platnumz. Ni jambo zuri sana.”

Kutajwa kwa jina hilo kunakuja baada ya jina la mtoto huyo kuwa miongoni mwa mambo yaliyokuwa yakisubiriwa kufahamika rasmi na mashabiki wa Diamond na Zuchu tangu kuzaliwa kwake Agosti 2, 2026.

Jina hilo pia liliwahi kuibuka kwenye mitandao ya kijamii, huku baadhi ya watu wakimtaja mtoto huyo kama Sandra, lakini hakukuwa na uthibitisho wa wazi kutoka kwa wazazi wake kuhusu jina hilo.

Safari hii, kauli ya Khadija Kopa imeongeza uzito katika mjadala huo, kwani jina hilo limetajwa na mama mzazi wa Zuchu mwenyewe akiwa katika hafla ya 40 ya mjukuu wake.

Hafla hiyo imewakutanisha ndugu, marafiki na watu mbalimbali wa karibu na familia ya Diamond na Zuchu katika ukumbi wa Saint Laurent Garden, huku ujio wa mtoto huyo ukiendelea kuwa gumzo katika ulimwengu wa burudani.