Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kajala afunguka kurudi kwa Harmonize

Muktasari:

  • Mwanaspoti na safu hii ya Dakika 5 Na... lilitaka kujua kuhusu yaliyokuwa yanazungumzwa kuhusu wao na endapo kama kuna tetesi za wawili hao kurudiana na Kajala anafunguka kila kitu.

UMRI namba tu, kinachotakiwa ni mapenzi ya kweli. Ndivyo anavyosema Msanii na mrembo, Kajala Masanja baada ya kukumbushiwa uhusiano wake na msanii wa Bongo Fleva, Harmonize.

Mwanaspoti na safu hii ya Dakika 5 Na... lilitaka kujua kuhusu yaliyokuwa yanazungumzwa kuhusu wao na endapo kama kuna tetesi za wawili hao kurudiana na Kajala anafunguka kila kitu.

Kikubwa ni ile ishu ya umri wake na Harmonize na yeye na yamezungumzwa mengi kwa kuwa Kajala ni mkubwa zaidi ya Konde Boy na haikuleta picha nzuri kwa mashabiki wao.

Mwenyewe anakataa na kudai umri ni namba na haina haja ya watu kuwaita wapenzi wa wenzio madogo kwani wao ndio wamependana.

“Kinachoshangaza ni kwa nini wanapenda kuwaita watoto wa wenzao wadogo, kivipi sasa! Mtu akiwa kwenye uhusiano tu utasikia mdogo, hebu waache hiyo tabia. Mtoto mdogo hawezi kuingia kwenye uhusiano hata kidogo.”

Na vipi mpango wa kurudiana? Kuna wanaosema hata uende wapi kwa Konde Boy ndio ulifika na utarudi

“Nafikiri wao ni watabiri wakubwa, haya ngoja tuone wanavyosema, maana wanajua kila kitu kuliko mimi mwenyewe.”

Kuna hii ishu ya kuitwa bibi (umri umeenda)? Mpenzi wako wa sasa anaichukuliaje?

“Ananipenda na kunijali, anawezaje sasa kutonipenda wakati umri wangu unafaa kuitwa bibi na mjukuu ninaye na nina tamba naye.”

Msikie kuhusu yeye na mjukuu wake, ishu ya kuwa naye karibu na madai ya watu kuhusu kumsuka nywele za watu wazima

“Yapo mambo huwezi kuzuia. Mtoto amekuwa na kuhusu kusukwa hakuna shida. Naona kuna wazazi wengi wa mitandaoni.”

“Kikubwa nipo karibu naye licha ya wakati mwingine kuwa mbali. Hata hivyo, kama baba yake anamwona kila siku na anampeleka na kumrudisha kutoka shule ndiyo muhimu. Mimi nampenda sana mjukuu wangu.”

Hivi ndivyo anavyomwona mjukuu wake

“Kwanza kabisa ni mtoto anayenipenda sana na kingine atakuja kuwa mtu mwenye upendo wa hali ya juu na kila siku namwombea kwa Mungu akue katika hilo.”