Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

JUX: Ndoa imenipa msukumo mpya wa nyimbo za mapenzi

JUX Pict

Muktasari:

  • Jux amesema maisha anayoyaishi ndani ya ndoa yamemrahisishia kupata hisia na maneno ya kuandika, tofauti na kipindi ambacho alikuwa akiimba kuhusu mapenzi kutokana na mitazamo na uzoefu wa nje.

MUIMBAJI wa Bongo Fleva, Juma Jux, amesema ndoa yake na mwanamitindo wa Nigeria, Priscilla Ojo, imempa msukumo mpya katika kuandika nyimbo za mapenzi.

Jux amesema maisha anayoyaishi ndani ya ndoa yamemrahisishia kupata hisia na maneno ya kuandika, tofauti na kipindi ambacho alikuwa akiimba kuhusu mapenzi kutokana na mitazamo na uzoefu wa nje.

Akizungumza wakati wa mahojiano kwenye hafla ya AFRIMMA jijini Dallas, Marekani, Jux amesema kuwa na mke kumempa mazingira mazuri zaidi ya kutengeneza muziki wa aina hiyo.

AFRIM 03

"Nimeoa mke wangu mrembo, kunafanya iwe rahisi zaidi kuandika mistari ya kimapenzi ambayo watu wote tunaipenda,” amesema Jux.

Kauli hiyo imekuja wakati Jux akiendelea kuonyesha upande wake wa kimapenzi kupitia muziki, huku baadhi ya kazi zake zikihusishwa moja kwa moja na safari yake ya mapenzi na Priscilla.

Miongoni mwa nyimbo hizo ni “God Design”, aliyomshirikisha msanii wa Nigeria, Phyno, ambayo ilitoka katika kipindi cha harusi yake na Priscilla na kubeba ladha ya mapenzi.


AFRIM 05

Jux pia ameendelea na upande huo kupitia wimbo “Si Mimi”, akiongeza kwenye orodha ya nyimbo zinazomweka katika nafasi yake ya kawaida kama msanii anayependa kuzungumzia mapenzi na mahusiano.

Hivi sasa Jux mapenzi si mada anayoiangalia kwa mbali pekee, bali ni sehemu ya maisha yake. Ndoa imempa uzoefu mpya ambao anaweza kuugeuza kuwa mawazo, hisia na hatimaye kuwa nyimbo.

Hivyo, wakati mashabiki wakisubiri kazi zake zinazofuata, Jux anaonekana kuwa na chanzo kipya cha simulizi za maisha ya ndoa yenyewe, jambo ambalo linaweza kufanya nyimbo zake za mapenzi kuwa na mguso tofauti.

Februari 7, 2025, Jux na Priscilla walifunga ndoa Mbezi Beach, Dar es Salaam, baada ya hapo zikafuatia sherehe kadhaa za harusi yao hiyo iliyohudhuriwa na watu mbalimbali.