Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Familia ya Jux, Priscilla kivutio

FAMILIA Pict

Muktasari:

  • Ukaribu huo umeendelea kuzua gumzo kwa mashabiki wa mastaa, hasa kutokana na namna uhusiano wa wifi na shemeji unavyofuatiliwa kwa karibu kwenye mitandao ya kijamii.

FAMILIA ya msanii wa Bongo Fleva, Juma Jux imeendelea kuonekana kuwa karibu na mke wake, Priscilla Ojo, huku dada yake Jux, Fatma Mkambala, akiwa miongoni mwa watu wanaoonekana kumuunga mkono.

Ukaribu huo umeendelea kuzua gumzo kwa mashabiki wa mastaa, hasa kutokana na namna uhusiano wa wifi na shemeji unavyofuatiliwa kwa karibu kwenye mitandao ya kijamii.

Katika familia nyingi, uhusiano kati ya mke na ndugu wa mume unaweza kuwa na changamoto zake. Hata hivyo, kwa upande wa familia ya Jux, kinachoonekana hadharani ni picha tofauti; watu hao wawili wamekuwa wakionyesha ukaribu, kuheshimiana na kufurahia pamoja matukio mbalimbali ya kifamilia.

Hivi karibuni, video ya Priscilla iliibua gumzo baada ya kuulizwa kama anaweza kuzungumza Kiswahili. Katika majibu yake, alishindwa kutamka neno hilo kwa usahihi na kusema “Kiswalala,” jambo lililomfanya wifi yake, Fatma, kucheka na baadhi ya watu kuweka coments za kufarahishwa na maisha yao ya ukaribu.

JU 01

“Wanavutia sana, wanapenda kuwa pamoja muda mwingi lakini pia nahisi wanapeana na fursa, hili ni jambo jema sana,’’ aliandika Lucy Kameela.

Kwa upande wa Fatma, ukaribu wake na Priscilla unaweza pia kutafsiriwa kama sehemu ya kumpokea na kumkaribisha mwanamke huyo katika familia baada ya kuwa mke wa kaka yake.

Tofauti na ukaribu unaoonekana kati ya Fatma na Priscilla, uhusiano wa Zuchu na wifi yake, Esma Platnumz uliwahi kuwa gumzo kubwa kwenye mitandao ya kijamii.

Kulikuwa na mijadala mbalimbali iliyowafanya baadhi ya mashabiki kuamini huenda wawili hao hawakuwa kwenye ukurasa mmoja, lakini baadaye waliweka wazi kuwa hawana shida

JU 02

Ndiyo maana ukaribu wa Fatma na Priscilla unaonekana kuwa tofauti na simulizi hizo. Agosti 29, 2026, katika kumbukumbu ya kuzaliwa ya Rakeem, wawili hao walionekana wakicheza na kufurahia pamoja.

Fatma pia amekuwa miongoni mwa watu wanaomuunga mkono Priscilla katika biashara yake ya Pricy Luxe.