Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Drake aipa kisogo Grammy 2027, hizi ndizo sababu

Muktasari:

  • Albamu hizo ambazo ulikuwa mradi wake wa kwanza baada ya bifu lake la Kendrick Lamar, zinaendelea kufanya vizuri kwenye chati za muziki pamoja mitandao ya kusikiliza muziki (digital streaming).

Rapa kutokea Canada, Drake amepanga kutowasilisha albamu zake tatu zilizotoka mwaka huu katika mchakato wa kupata utezi wa kuwania tuzo za Grammy 2027. Albamu hizo ni Iceman, Habibti na Maid of Honour, ambazo zilitoka kwa pamoja mnamo Mei.


Albamu hizo ambazo ulikuwa mradi wake wa kwanza baada ya bifu lake la Kendrick Lamar, zinaendelea kufanya vizuri kwenye chati za muziki pamoja mitandao ya kusikiliza muziki (digital streaming).


Kati ya hizo tatu, albamu ya Iceman ndio imefanya vizuri zaidi ikiweka rekodi ya kukaa kwa muda mrefu zaidi nafasi ya kwanza kwenye chati ya Billboard Top R&B/Hip-Hop Albums, na kuvunja rekodi ya albamu yake, Take Care (2011) ambayo ilikaa nafasi ya kwanza kwa wiki 12.


Hata hivyo, Drake mwenyewe alishadokeza kuhusu uamuzi wake huo kupitia wimbo wa mwisho wa albamu yake, Iceman (2026) unaoitwa ‘Make Them Know’ ambapo anasikika akisema; Albamu hii, kamwe sitaiwasilisha.


Drake, mkali wa kibao cha Hotline Bling (2016), hii si mara ya kwanza kutowasilisha albamu zake Grammy, tuzo ambazo amewahi kushinda mara 5 baada ya kutajwa kuwania mara 51.


Kwa mujibu wa Billboard, uamuzi huo unakuja wakati Drake akirejea kwenye vichwa vya habari kupitia bifu lake na Kendrick Lamar, huku pia akiendelea na mgogoro wa kisheria dhidi ya kampuni ya muziki ya Universal Music Group (UMG).

Drake anaishutumu kampuni hiyo kwa kuupa promosheni kubwa wimbo wa Kendrick Lamar, Not Like Us (2024) ambao uliweka rekodi ya kushinda tuzo 5 za Grammy. Drake anadai wimbo huo una maneno ya kumkashifu na kuharibu sifa yake.


Hata hivyo, jaji wa mahakama alitupilia mbali kesi hiyo mwaka jana lakini timu ya Drake ikakata rufaa dhidi ya uamuzi huo. Rufaa hiyo zinatarajiwa kuanza kusikilizwa mnamo Desemba mwaka huu.


Lakini kabla ya kuibuka kwa bifu na Kendrick Lamar, tayari Drake alikuwa ameshasusia Grammy mara kadhaa kupitia albamu zake tatu. Albamu za Drake ambazo hazikuwasilisha katika mchakato wa kuwania Grammy ni pamoja na More Life (2017), Certified Lover Boy (2021), na Honestly, Nevermind (2022).


Hata hivyo, albamu yake ya pamoja na rapa 21 Savage, Her Loss (2022), iliwasilishwa kuwania tuzo za Grammy 2024 lakini ilishindwa kufua davu katika kipengele cha Albamu Bora ya Rap, ambapo ushindi ulienda kwa Killer Mike kupitia albamu yake ya sita, Michael (2023).