Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Diamond amvamia Trey Songz jukwaani

New Content Item (1)

Muktasari:

  • Trey Songz alikuwa akifanya onyesho lake la kwanza nchini Tanzania akiwakutanisha mashabiki na muziki wake wa R&B katika usiku uliojaa burudani.

Staa wa Bongofleva, Diamond Platnumz, amewashangaza mashabiki kwenye Tamasha la Imbeju Sauti Moja lililofanyika Viwanja vya Posta, Dar es Salaam, baada ya kutokea jukwaani wakati staa wa R&B kutoka Marekani, Trey Songz, akiendelea kutoa burudani.

Trey Songz alikuwa akifanya onyesho lake la kwanza nchini Tanzania akiwakutanisha mashabiki na muziki wake wa R&B katika usiku uliojaa burudani.

Hata hivyo, hali ilibadilika ghafla Diamond alipopanda jukwaani na kusababisha umati kulipuka kwa shangwe huku baadhi ya mashabiki wakianza kumuita kwa sauti “Simba! Simba!”

Kupanda kwa Diamond hakukuishia kwenye kusalimiana na Trey Songz, kwani wawili hao walitumia nafasi hiyo kuwapa mashabiki burudani ya kipekee kwa kutumbuiza pamoja wimbo wao mpya unaoitwa ‘Big Money’ ambao bado haujatoka rasmi.

Ilikuwa mara ya kwanza kwa Diamond na Trey Songz kuonekana wakitumbuiza pamoja nchini Tanzania, jambo lililoongeza uzito wa tukio hilo kutokana na kuwa collabo hiyo imekuwa ikisubiriwa na mashabiki.

Diamond alionekana kujiamini jukwaani kama kawaida yake, akimpa sapoti Trey Songz na kuungana naye katika sehemu mbalimbali za wimbo huo.

Uwezo wake wa kuichangamsha hadhira uliendelea kuonekana, huku mashabiki wakipaza sauti kila alipokuwa akichukua nafasi kwenye performance.

Kwa upande wake, Trey Songz alionekana kufurahia uwepo wa Diamond jukwaani, huku msanii huyo wa Marekani akishuhudia moja kwa moja namna Diamond anavyoweza kubadilisha hali ya jukwaa ndani ya muda mfupi.

Katika baadhi ya vipande vya performance hiyo, Trey alimwachia Diamond nafasi huku akiendelea kushiriki kwa kuunga sauti.

Tukio hilo limeongeza hamu ya mashabiki kutaka kusikia ‘Big Money’ ikiwa imekamilika na kutolewa rasmi. Performance hiyo ya Imbeju Sauti Moja imebaki kuwa miongoni mwa matukio yaliyoangaliwa zaidi katika usiku ambao Trey Songz aliweka historia ya kutumbuiza Tanzania kwa mara ya kwanza.