Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Diamond alivyo na deni kubwa kolabo kimataifa

Muktasari:

  • Mastaa kama Snoop Dogg, Busta Rhymes, Akon, Wiz Khalifa, Trey Songz na Wizkid, ni miongoni mwa wale ambao Diamond alishaweka wazi kuwa amerekodi nao lakini hadi sasa haijulikani ni lini kazi hizo zitatoka au hazitokuja kuachiwa kabisa.

STAA wa Bongofleva, Diamond Platnumz amewahi kudokeza ujio wa kolabo kadhaa na mastaa wakubwa duniani lakini miaka inazidi kusonga bila ngoma hizo kusikika licha ya mashabiki kuonyesha utayari kufuatia matangazo yake.

Mastaa kama Snoop Dogg, Busta Rhymes, Akon, Wiz Khalifa, Trey Songz na Wizkid, ni miongoni mwa wale ambao Diamond alishaweka wazi kuwa amerekodi nao lakini hadi sasa haijulikani ni lini kazi hizo zitatoka au hazitokuja kuachiwa kabisa.

Baada ya kuhudhuria hafla ya utoaji wa tuzo za BET 2021 ambapo aliwaniwa kipenge cha Best International Act, Diamond alionekana studio na wasanii wakubwa wa Marekani kama Busta Rhymes, Snoop Dogg, Akon na Wiz Khalifa.

Wakati huo Diamond alichukua muda mrefu Marekani huku kurasa za mitandao ya kijamii ya lebo yake ya WCB Wasafi, zikitoa taarifa kila wakati jinsi msanii huyo alivyokuwa akikutana na wasanii wa huko na kurekodi. 

Hata hivyo, walichofanya studio hadi sasa hakijasikika, mashabiki wengi waliotarajiwa kolabo hizo zingesikika kwenye Extended Playlist (EP) yake Diamond, First of All (FOA) iliyotoka Machi 2022 lakini haikuwa hivyo hata kwa ngoma zilizofuata baadaa ya hapo.

Meneja wa Diamond, Sallam SK alisema walipanga msanii huyo hasimshirikishe msanii yeyote katika EP hiyo, hivyo hata waliopata nafasi hiyo kama Zuchu na Mbosso ilikuwa basi tu!, ila kolabo zaidi zitakuwa kwenye albamu yake ijayo ambayo hadi sasa haijatoka.

Mashabiki wengi walitamani kumsikia Diamond akiimba na Snoop Dogg, rapa aliyepata umaarufu baada ya kushirikishwa na Dr. Dre katika wimbo, Deep Cover (1992) na baadaye kwenye albamu ya kwanza ya Dre, The Chronic (1992) .

Baada ya kusaini Death Row Records, Snoop Dogg alitoa albamu yake ya kwanza, Doggystyle (1993) ambayo ilitayarishwa na Dr. Dre, huku ukiuza nakala 800,000 katika wiki yake ya kwanza sokoni, na hadi sasa ameuza zaidi ya albamu milioni 35 duniani kote.

Baada hilo kupita, mnamo Agosti mwaka huu Diamond akaonekana Zanzibar akishuti video na mwanamuziki mwingine wa Marekani, Trey Songz ambaye alikuja nchini kufanya, pia Diamond aliachia kionjo cha wimbo huo unatajwa kwenda kwa jina la Big Money.

Lakini wimbo huo ulianza kurekodiwa mwaka uliopita baada ya Diamond kwenda Marekani kwa ajili ya shughuli zake za kimuziki, hivyo Trey Songz alipokuja Bongo ikawa ni zamu ya kushuti video yake.

Kutokana na hilo, mashabiki wengi walitegemea wimbo huo ungetoka mapema lakini hadi wakati huu kimya huku mwanamuziki huyo akiendelea kuachia nyimbo zake nyingine hasa za Amapiano ambazo amekuwa akishirikiana na wanamuziki wa Afrika Kusini.

Utakumbuka mara ya mwisho Diamond kufanya kazi na msanii mkubwa wa Marekani ni pale aliposikika katika wimbo wa Ciara, Low (2025) uliojumuishwa katika toleo la pili la albamu (Deluxe edition) ya nane ya mwanamuziki huyo iitwayo 'Cici' ambayo ilitoka Agosti 22, 2025.

Hiyo ilikuwa ni albamu ya pili ya msanii wa kike kutokea nchini Marekani kwa Diamond kupata nafasi ya kuwepo ndani yake. Awali, mwanzilishi huyo wa WCB Wasafi alisikika katika albamu ya saba yake Alicia Keys (Alicia) ambapo alishirikishwa katika wimbo, Wasted Energy (2020).

Na hapo awali Diamond aliwashirikisha wasanii wa Marekani wakiwemo Ne-Yo (Marry You), Rick Ross (Waka), Omarion (African Beauty), na Jason Derulo (Komasava), ambapo wimbo huo uliingia chati ya Billboard U.S. Afrobeats Songs.

Mwaka 2019, staa wa Nigeria, Wizkid aliletwa na Diamond Tanzania kufanya show ambapo alitumbuiza katika tamasha la Wasafi Festival, baada ya hapo wawili hao walienda Zanzibar ambapo alielezwa walienda kushuti video ya wimbo wao.

Wakati huo tayari Diamond alikuwa ameshafanya kazi na wasanii wengi wa Nigeria akiwemo Davido, P-Square, Mr. Flavour, Tiwa Savage, Iyanya, Teni na kadhalika.

Utakumbuka pia Diamond ni shabiki wa Wizkid, mathalani wimbo wa Diamond 'Jeje' ambao ulitoka rasmi Machi 21, 2020 kwa kiasi imechukua vitu kutoka kwa ule ya Wizkid 'Joro' uliyotoka Septemba 30, 2019.

Meneja wa Diamond na WCB Wasafi kwa ujumla, alisema nyimbo hizo zinafanana kiasi kutokana zote mbili zimetengenezwa na mtayarishaji mmoja, Kelpvibe wa Nigeria. Pia wimbo wa Diamond 'Loyal' kutoka katika EP yake ya kwanza, First of All (2022), umefanana sana na ule wa Wizkid, Essence (2020) akimshirikisha Tems, mshindi wa Grammy mbili kutokea Nigeria pia.

Mtayarishaji S2kizzy alikiri kuwa walipata wazo au hamasa ya kutengeneza wimbo huo kufuatia 'Essence' kufanya vizuri zaidi duniani ambapo ilikuja kushinda tuzo zaidi ya 20 ikiwemo BET 2022 kama Wimbo Bora wa Kushirikiana na pia kuwania Grammy.