Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Christian Bella afunguka kuhusu “Ex”

BELLA Pict

Muktasari:

  • Wimbo huo uliotoka Agosti 21, 2026, umeambatana na video rasmi ambayo tayari imewekwa kwenye ukurasa wa YouTube wa Christian Bella, ukiwa ni miongoni mwa kazi zake mpya anazoendelea kuzisukuma kwa mashabiki wake.

MWANAMUZIKI wa dansi na rumba nchini, Christian Bella ameachia kazi mpya inayokwenda kwa jina la Ex, huku akigusa maisha ya mahusiano yanayofika ukingoni kutokana na tabia za mmoja wa wapenzi katika uhusiano.

Wimbo huo uliotoka Agosti 21, 2026, umeambatana na video rasmi ambayo tayari imewekwa kwenye ukurasa wa YouTube wa Christian Bella, ukiwa ni miongoni mwa kazi zake mpya anazoendelea kuzisukuma kwa mashabiki wake.

BELL 01

Si wimbo wa ex wangu

Kutokana na jina la wimbo huo, Ex, msikilizaji anaweza kudhani kuwa Bella ameamua kutumia muziki kueleza yaliyompata katika uhusiano fulani uliopita.

Hata hivyo, Bella analiambia Mwanaspoti tofauti na ambavyo baadhi ya mashabiki wanaweza kufikiria, hakumtungia wimbo huo mtu aliyewahi kuwa mpenzi wake.

“Sijamtungia ex wangu huu wimbo. Nimeutunga kutokana na mazingira yaliyopo ndani ya mahusiano ya watu. Kuna mambo mengi ambayo watu wanapitia kwenye mahusiano yao na nimechukua mazingira hayo kuyaweka kwenye muziki,” anasema Bella.

Kauli hiyo inafanya Ex kuwa zaidi ya simulizi ya mtu mmoja, kwani Bella ameamua kugusa jambo ambalo linatokea kwenye mahusiano ya watu mbalimbali, watu kuanza kwa mapenzi, lakini baadaye tabia na changamoto mbalimbali kuwafanya wafikie hatua ya kuachana.

BELL 07

Tabia zinavyogeuza penzi kuwa “Ex”

Katika Ex, Bella anaingia kwenye upande wa mahusiano ambayo hayana utulivu, akigusa tabia zinazoweza kumchosha mwenza na hatimaye kumfanya afikie uamuzi wa kuondoka.

Hii ndiyo sehemu ambayo wimbo huo unaweza kuwagusa watu wengi, kwa sababu neno “ex” lenyewe limezoeleka katika maisha ya mahusiano ya sasa.

Mtu ambaye jana alikuwa mpenzi, leo anaweza kuwa kumbukumbu kutokana na tofauti zilizoshindikana kutatuliwa.

Bella, kwa kutumia ladha yake ya rhumba, amechukua mazingira hayo na kuyafanya kuwa simulizi ya kimuziki. Hivyo, badala ya kuimba tu kuhusu mapenzi matamu, safari hii ameamua kuangalia upande mwingine wa penzi ule unaofika mwisho.

BELL 03

Video nayo yazidi kuipa nguvu

Mbali na wimbo, Bella ameupa uzito pia upande wa picha kupitia video rasmi ya Ex, ambayo imewekwa kwenye YouTube yake.

Video hiyo inafanya kazi pamoja na ujumbe wa wimbo, huku jina Ex likiwa sehemu kubwa ya mvuto wa kazi hiyo. Kwa sasa, Ex imeorodheshwa kama single yake mpya ya 2026 kwenye majukwaa ya muziki, huku Apple Music ikiweka Agosti 21 kama tarehe rasmi ya kutolewa.

Bella pia alikuwa ameshaanza kuipa kazi hiyo presha kabla ya kutoka, akitumia mitandao yake kutangaza ujio wa “New Rhumba” na kuwapa mashabiki ishara kwamba alikuwa akija na Ex.

Hivyo, kwa mashabiki waliokuwa wakisubiri kazi hiyo, sasa wana nafasi ya kusikiliza na kuitazama video yake huku wakitafsiri ujumbe uliopo kwa namna yao.

BELL 02

Bella bado anaichangamsha rhumba

Ex inakuja katika kipindi ambacho Bella anaendelea kujenga safari yake kwenye muziki wa rhumba na dansi akiwa pia kiongozi wa Malaika Band.

Historia yake katika muziki imekuwa ndefu, baada ya kurejea mwaka 2013, alianzisha Malaika na kuendelea kutoa kazi zilizomsaidia kuimarisha nafasi yake katika muziki wa Tanzania.

Ukurasa rasmi wa Bella kwenye YouTube pia unamtambulisha kama msanii anayejulikana kwa uwezo wake wa kutumbuiza jukwaani akiwa na Malaika Band, huku akiwa ametoa nyimbo mbalimbali na kushinda tuzo katika safari yake ya muziki.

BELL 06

Sasa kupitia Ex, Bella anaendelea na mtindo wake wa kusimulia maisha kwa kutumia muziki, safari hii akipeleka mashabiki kwenye upande wa mahusiano ambao wengi wanaweza kuuelewa.

Na kwa kuwa mwenyewe ameshaweka wazi kuwa hakumtungia ex wake, swali linabaki kwa mashabiki wanaoisikiliza kazi hiyo: Bella ameimba kuhusu nani?

Jibu lake ni moja, mazingira ya mahusiano ya watu ndiyo yaliyompa msukumo wa kuja na “Ex”.