Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Chameleone awaka, hataki kulazimishwa talaka

KINYONGA Pict

Muktasari:

  • Katika moja ya mahojiano aliyofanya,  Chameleone amezungumzia mvutano wa kisheria unaoendelea, akielekeza zaidi katika suala la mali na wosia wake.

MWIMBAJI nguli wa muziki wa Uganda, Joseph Mayanja maarufu kama Jose Chameleone amesema ingawa yeye na mkewe wako katika mchakato wa talaka, lakini hafurahishwi na jinsi anavyolazimishwa kugawana mali.

Katika moja ya mahojiano aliyofanya,  Chameleone amezungumzia mvutano wa kisheria unaoendelea, akielekeza zaidi katika suala la mali na wosia wake.

Amesema, ingawa anakubaliana na wazo la kugawana mali, hajaridhishwa na kulazimishwa kusaini hati za kugawa mali hizo akiwa bado hai na mwenye afya njema.

"Vitu tunavyogombania si vyangu, ni vya watoto wetu. Hata wao wataviacha nyuma na watoto wao wataendelea navyo. Shida yangu ni kwamba wananisukuma, nisaini wosia juu ya mali hizi nikiwa bado hai na mzima wa afya," amesema Chameleone.

Msanii huyo mwenye watoto watano, Abba, Apha, Ama na Zara ameongeza, kama sheria ikimlazimisha kusaini mali zake atafanya hivyo, lakini ameeleza wazi kutoridhika na mchakato huo.

ILIVYOKUWA
Kauli ya Chameleone inakuja baada ya miezi kadhaa mkewe Daniella Atim ambaye wamekuwa katika ndoa kwa takribani miaka 17 kufungua kesi ya talaka Machi mwaka huu.

Katika hati zake, inaelezwa Daniella ambaye tangu 2018 amekuwa akiishi Marekani na watoto amemshutumu mumewe kwa kutelekeza familia, kutotoa msaada na kuachana nao.

Lakini staa huyo wa ngoma Forever, Jamila na Tubonge amepinga madai ya kutelekeza familia, akisema uamuzi wa kuhamia Marekani ulikuwa makubaliano ya pande zote, akieleza amekuwa akiwahudumia watoto wake kwa wakati wote na anaomba nyumba ya Seguku ibaki mali ya familia kwa manufaa ya watoto wao.

Aidha, amedai mkewe amejaribu kuwapotosha watoto dhidi yake na amesisitiza kutaka nafasi ya kuwa karibu nao licha ya changamoto hizi za ndoa.

Jose Chameleone ni miongoni mwa wasanii wa Uganda waliowahi kukubalika Bongo hususan miaka ya 2000 kipindi ambacho Bongo Fleva ilishamiri.

Baadhi ya ngoma zilizofanya vizuri ni pamoja na Shida za Dunia iliyotoka mwaka 2008, Iligusa hisia za mashabiki kwa ujumbe wake wa kijamii na kupendwa na wasikilizaji.

Nyimbo nyingine ni Jamila ya mwaka 2005 ilikuwa moja ya ngoma kali za mapenzi iliyopendwa na vijana wa Bongo.