Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Aslay afunguka kuachia Album, amtaja Marioo

ASLAY Pict

Muktasari:

  • Safari hii ameibuka na albamu yake mpya My Way, ambayo inakuja kipindi ambacho pia Marioo anaachia albamu yake, jambo lililoibua mjadala kwa mashabiki wa muziki nchini. 

Mwanamuziki Aslay ni miongoni mwa wasanii wa Bongo Fleva wanaoendelea kubaki katika ushindani kwa muda mrefu kutokana na uwezo wake mkubwa wa kutunga na kuimba nyimbo zinazogusa maisha ya watu.

Safari hii ameibuka na albamu yake mpya My Way, ambayo inakuja kipindi ambacho pia Marioo anaachia albamu yake, jambo lililoibua mjadala kwa mashabiki wa muziki nchini. Katika Dakika 5 ya Mwanaspoti, Aslay amefunguka kuhusu albamu hiyo, ushindani wa muziki na maisha yake ya uswazi

ASLA 04

MWANASPOTI: Kwanza hongera kwa albamu yako mpya ya My Way, ambayo utaiachia May 29, 2026 inaingumziaje?

ASLAY: Nashukuru sana. Hii ni albamu ambayo nimeiandaa kwa muda mrefu na nimeweka hisia zangu nyingi ndani yake. Mashabiki watarajie muziki mzuri, melody nzuri na ujumbe ambao kila mtu anaweza kuuelewa.

ASLA 01

MWANASPOTI: Wengi wamezungumzia kuhusu wewe kuachia albamu kipindi ambacho Marioo naye anaachia yake, hilo unalizungumziaje?

ASLAY: Muziki ni ushindani wa kazi nzuri, lakini si ugomvi. Marioo ni mtu wangu kwenye game, kila mmoja ana muda wake wa kutoa kazi. Kikubwa mashabiki wapate muziki mzuri.


MWANASPOTI: Hiyo haikuwezi kukupa presha kidogo sokoni?

ASLAY: Hapana kabisa. Mimi naamini kwenye kazi yangu na mashabiki wangu. Kila msanii ana audience (mashabiki) yake na mwisho wa siku muziki mzuri ndio hushinda.


MWANASPOTI: Katika My Way umeonekana kugusa sana masuala ya mapenzi na maisha ya kawaida, kwa nini?

ASLAY: Kwa sababu hayo ndiyo maisha halisi ya watu wetu. Mimi napenda kufanya muziki ambao mtu akisikia anaona kabisa unaendana na maisha yake.


MWANASPOTI: Nyimbo gani unahisi zitafanya vizuri zaidi kwenye albamu hiyo?

ASLAY: Kwa sasa naona watu wameanza kupokea vizuri wimbo wa Natulia, Ndo Wewe, Lonely na No Money No Love, lakini naamini kila wimbo una nafasi yake.

ASLA 02

MWANASPOTI: Bado video zako nyingi unazifanyia uswazi na vijijini licha ya mafanikio yako makubwa, kuna sababu gani?

ASLAY: Mimi nimezaliwa uswazi na nimekulia huko, hivyo siwezi kuikimbia asili yangu. Napenda kuonyesha maisha ya kawaida kwa sababu ndiyo uhalisia wangu.


MWANASPOTI: Kuna kipindi ulisema baada ya kutoka Yamoto Band maisha yalikuwa magumu kidogo, leo ukiangalia nyuma unaonaje?

ASLAY: Namshukuru Mungu sana. Kulikuwa na changamoto, lakini niliamini sauti yangu inaweza kunibeba. Leo hii bado nipo na mashabiki wanaendelea kunisupport.


MWANASPOTI: Unatajwa kufanya vizuri hata Afrika Magharibi, hilo linakupa picha gani?

ASLAY: Ni jambo kubwa kwangu. Inaonyesha muziki wetu wa Tanzania unazidi kuvuka mipaka. Bado kuna mipango mingi mizuri mbele.

ASLA 03

MWANASPOTI: Vipi kuhusu maisha yako binafsi ambayo mashabiki hupenda kuyafuatilia?

ASLAY: (Anacheka) Mimi napenda watu wajue zaidi kazi yangu kuliko maisha binafsi, ila muda ukifika baadhi ya vitu vitakuwa wazi.


MWANASPOTI: Mwisho una ujumbe gani kwa mashabiki wako?

ASLAY: Nawashukuru sana kwa support yao kubwa. Waendelee kusikiliza My Way na wategemee mambo makubwa zaidi kutoka kwa Aslay mwaka huu.