Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Diamond akiri 'kumwibia' T.I.D

DIAMOND Pict

Muktasari:

  • Kauli za wasanii hao wawili zimeonyesha namna heshima ilivyoendelea kuwepo kati ya kizazi cha zamani na cha sasa kwenye muziki wa Tanzania, huku mashabiki wengi wakitamani kuwaona siku moja wakifanya kazi ya pamoja studio.

MSANII wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz ameibua gumzo mitandaoni baada ya kukiri amejifunza na hata 'kumuibia' vitu vingi kimuziki msanii mkongwe T.I.D ambaye amemtaja kama mmoja wa role model wake kwenye muziki.

Diamond amesema T.I.D ni miongoni mwa wasanii walioweka msingi mkubwa wa muziki wa kizazi cha sasa na kuna mambo mengi aliyokuwa akiyafuatilia kutoka kwake tangu zamani ili kujijenga kisanii.

“T.I.D ni role model wangu, ana roho nzuri sana na kwenye career yangu nimemwibia vitu vingi sana,” amesema Diamond Platnumz.

DIAMO 02

Mbali na hilo, Diamond alifunguka moja ya nyimbo ambazo bado anazikubali zaidi kutoka kwa T.I.D ni wimbo wa ‘Nyota’, akisema ulikuwa na ubora mkubwa wa kimuziki na ujumbe uliowagusa watu wengi kipindi hicho.

Kauli hiyo ya Diamond imewafurahisha mashabiki wengi wa muziki wa Bongo Fleva ambao wamekuwa wakiamini T.I.D ni mmoja wa wasanii waliofungua njia kwa kizazi cha sasa kutokana na mchango wake mkubwa kwenye ukuaji wa muziki wa Tanzania.

Kwa upande wake, T.I.D alimwaga sifa kwa Diamond Platnumz akisema amefanya kazi kubwa sana kuikuza Bongo Fleva na kuifikisha kwenye kiwango cha kimataifa kutokana na muziki na biashara zake.

DIAMO 01

“Diamond kwa sasa ni kama kipande cha keki ambacho kila mtu anataka kukitumia. Amefanya kazi kubwa sana kwenye muziki,” amesema T.I.D.

Kauli za wasanii hao wawili zimeonyesha namna heshima ilivyoendelea kuwepo kati ya kizazi cha zamani na cha sasa kwenye muziki wa Tanzania, huku mashabiki wengi wakitamani kuwaona siku moja wakifanya kazi ya pamoja studio.