Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ally Star kuzikwa kesho Kilosa

ALLY Pict

Muktasari:

  • Ally Star amefariki dunia leo Jumanne Februari 3, 2026 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam, alipokuwa akipatiwa matibabu.

ALIYEKUWA mwimbaji nyota wa taarabu, Ally Star, anatarajiwa kuzikwa kesho Jumatano Februari 4, 2026 nyumbani kwao Wilaya ya Kilosa, Mkoa wa Morogoro.

Ally Star amefariki dunia leo Jumanne Februari 3, 2026 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam, alipokuwa akipatiwa matibabu.

Akizungumza na Mwanaspoti, Mkurugenzi wa TOT, Khadija Kopa ambaye pia ni muimbaji wa taarabu, amesema safari ya kwenda Kilosa itaanza kesho saa 2 asubuhi na mazishi yatafanyika mara tu baada ya kuwasili.

"Ally Star atazikwa kesho nyumbani kwao Kilosa Kichangani, hivyo safari itaanzia Hospitali ya Muhimbili ambapo waombelezaji wote watakutana hapo kuanzia saa 1 asubuhi, na atazikwa mara tu tutakapofika Kilosa," amesema Khadija Kopa.

Enzi za uhai wake, Ally Star aliiambia Mwanaspoti kuwa, mwili wake ulikuwa unapiga shoti kama umeme, hali ambayo ilikuwa ikimpa maumivu makali na kudhoofisha mwili wake.

Katika maisha ya muziki, Ally Star aliimba nyimbo maarufu kama Zumbukuku, Limbukeni, Natanga na Njia, Hauvumi Lakini Umo na nyingine nyingi.

Ally Star aliwahi pia kuzitumikia bendi kama Muungano Cultural Troupe, Orchestra King Kikii Double O na Bima Modern Taarab.