Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Albam ya Chinga yazua gumzo

CHINGa Pict

Muktasari:

  • Chinga alisema albamu hiyo itakuwa na ladha tofauti za muziki pamoja na simulizi zinazogusa maisha, akilenga kuwapa mashabiki wake burudani yenye maudhui na mitindo mbalimbali.

MWANAMUZIKI wa Bongo Fleva, Ibrah ‘Chinga’ ametangaza ujio wa albam yake iliyopewa jina la ‘1B’, itakayokuwa na jumla ya nyimbo 50.

Chinga alisema albamu hiyo itakuwa na ladha tofauti za muziki pamoja na simulizi zinazogusa maisha, akilenga kuwapa mashabiki wake burudani yenye maudhui na mitindo mbalimbali.

Hata hivyo, tangazo hilo limezua mshangao miongoni mwa mashabiki, wasanii na wadau wa muziki kutokana na idadi kubwa ya nyimbo zitakazokuwamo kwenye albamu hiyo.

Katika ukurasa wake wa Instagram, Ibraah alisema albamu hiyo itakuwa na nyimbo zinazozungumzia mapenzi, maumivu ya kuachwa, maisha ya kila siku, pamoja na nyimbo za burudani na mitaani.

Ibraah alifichua albamu hiyo itahusisha ushirikiano na Wasanii mbalimbali, wakiwemo Phina, Chid Benz, King Kaka, Dully Sykes na Paato, pamoja na Wasanii wengine watano.

Pia alisema albamu hiyo si mkusanyiko wa nyimbo pekee, bali ni uzoefu wa kipekee wa kimuziki, huku akiwataka Mashabiki wake kuchagua nyimbo tatu zinazowavutia zaidi katika orodha aliyotangaza.

Kwa upande wa wasanii wengine wa Bongo Fleva, idadi ya nyimbo 50 zilizotangazwa na Chinga inazidi ile iliyowahi kuwekwa kwenye baadhi ya albamu za majina makubwa katika muziki wa Bongo Fleva.

Jux aliachia albamu yake ya King of Hearts mwaka 2022 ikiwa na nyimbo 16, Alikiba aliachia albamu yake ya Only One King mwaka 2021 ikiwa na nyimbo 16, Harmonize naye aliachia  albamu yake ya mwisho Septemba 4, 2026,  aliyoiita’31’ ikiwa na jumla ya nyimbo 14.

Kwa upande wa wasanii wa kike, Zuchu alitoa albamu ya Peace and Money Desemba 2024 iliyokuwa na nyimbo 13, huku Nandy akiwa na albamu ya The African Princess iliyotoka mwaka 2018 ikiwa na nyimbo 10.

Ujio wa Albam hiyo inakuwa miongoni mwa kazi inayovuta hisia za mashabiki na wadau wa Bongo Fleva, wakisubiri kuona namna msanii huyo atakavyowasilisha kazi yenye idadi hiyo kubwa ya nyimbo.