Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Diamond: Nilitoa zaidi ya Sh4 bilioni kununua ndege, nikatapeliwa

Baada ya kutua Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga leo Oktoba 29, staa wa bongoflava Diamond Platnumz amefunguka kuhusu ishu ya ndege yake binafsi (private jet) aliyotaka kununua.

"Ishu ya ndege yangu ina mambo kidogo, nilinunua jet nimelipa fedha nimetapeliwa, nilimpigia Waziri Mbarawa (Waziri wa Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa) alinisaidia, kaka yangu Hamza ( Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Hamza Johari) alinisaidia na sasa serikali nzima inanisaidia kupata haki yangu, nililipa fedha nyingi, kianzio zaidi ya bilioni ila niliowawatumia wananiletea ujanja ujanja," amesema Diamond Platnumz

Diamond amekuwa akitumia ndege binafsi katika safari zake za ndani na nje ya nchi.