Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yanga, Simba zaingia kimyakimya Dar

Muktasari:

  • Miamba hiyo imetumia usafiri tofauti kuingia Dar wakitokea katika kambi zao za kujiandaa na mchezo huo

Dar es Salaam. Kumekucha baada ya kulikimbia jiji kwa wiki moja hatimaye Yanga  na Simba zimeingia Dar es Salaam kwa njia tofauti.

Yanga ikitokea Morogoro iliingia Dar es Salaam mapema asubuhi yale wakitumia usafiri wa basi lao na kujificha hotelini wakati Simba wakitokea Zanzibar walitua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius  Nyerere saa 3:45 asubuhi.

Simba itakuwa mgeni wa Yanga hapo kesho kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara utakaochezwa Uwanja wa Uhuru, saa 10:00 jioni.

Mashabiki wachache wa timu hiyo walijitokeza kwenye uwanja huo wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (Terminal 1) wakijisifu kwa kusema kesho lazima wakae.