Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Lyakuka aweka mipango mipya Transit Camp

LYAKUKA Pict

Muktasari:

  • Lyakuka aliyejiunga na timu hiyo akichukua nafasi iliyoachwa wazi na Vicent Barnabas aliyeifundisha msimu wa 2025-2026, ameiongoza katika mechi nane msimu huu, akishinda nne, sare moja na kupoteza tatu, ikishika nafasi ya tano na pointi 13.

BAADA ya Said Lyakuka kurejea tena kukifundisha kikosi cha maafande wa Transit Camp, kocha huyo amesema anachotaka ni kuendelea kuonyesha imani kwa uongozi wa timu hiyo uliomuamini wa kuhakikisha wanafanya vizuri na kutimiza malengo yao.

Akizungumza na Mwanaspoti, Lyakuka amesema haikuwa kazi ngumu wakati uongozi wa timu hiyo ulipomuhitaji arejee ndani ya kikosi hicho, jambo ambalo anataka kuendelea kuonyesha imani ya kukipigania ili kutimiza malengo ya kucheza Ligi Kuu.

"Ushindani ni mkubwa sana kwa sababu kila timu ina malengo iliyojiwekea kama ilivyokuwa pia na sisi, gepu la pointi kati ya inayoshika nafasi ya kwanza hadi ya 10, sio kubwa, jambo linaloonyesha ni lazima tujipange vizuri," amesema Lyakuka.

Kocha huyo aliyerejea tena Transit Camp baada ya kuifundisha mara ya mwisho msimu wa 2023-2024 na kumaliza nafasi ya 13 na pointi 27, amesema hadi sasa kumekuwa na maendeleo mazuri ya mchezaji mmoja mmoja, jambo linalompa matumaini makubwa.

Lyakuka aliyejiunga na timu hiyo akichukua nafasi iliyoachwa wazi na Vicent Barnabas aliyeifundisha msimu wa 2025-2026, ameiongoza katika mechi nane msimu huu, akishinda nne, sare moja na kupoteza tatu, ikishika nafasi ya tano na pointi 13.