Ozil ajipa uhakika kutua Manchester United
Muktasari:
- Mshambuliaji wa Arsenal, ameweka wazi kwamba mkataba wake ukiisha tu anatarajia kujiunga na kikosi cha Jose Mourinho, Manchester United.
Mkataba wa mshambuliaji Mesut Ozil unatarajiwa kuisha mwishoni mwa msimu huu na anataka kuwa chini ya kocha Jose Mourinho. Ozil alisisitiza kwamba kwa sasa moyo wake ameuelekeza Manchester United.
Sportsmail liliweka wazi kwamba kuna taarifa kwamba tayari Ozil amewambia rafiki zake kuwa anaamini Kocha Mourinho atamhamisha kwenye kipindi cha usajili wa kiangazi.
Hata hivyo habari mbaya kwa Arsenal ni kuwa, hata kama uongozi unahitaji kumbakiza kikosini hapo, mshambuliaji huyo hayupo tayari kukaa mezani na kujadiliana suala la kuongeza mkataba.